marcs
JF-Expert Member
- Nov 2, 2016
- 1,066
- 572
Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji imebatilisha uamuzi wa kamati ya masaa 72 kwa kuipa simba pointi 3 na kuzirudisha kwa kagera
Akitangaza uamuzi huo katibu mkuu wa TFF selestine mwesigwa amesema kamati ya sheria imebaini mapungufu kadhaa katika maamuzi ya kamati ya saa 72 kwa kwanza rufaa ya simba kukatwa nje ya wakati lakini pia haikulipa ada ya sh 300,000
Mbali ma hivyo mwesigwa amesema kamati ya saa 72 ilipokutana iliruhusu watu wasio wajumbe wa kamati kushiriki kufanya uamuzi kitu ambacho ni kosa
Mbali na uamuzuzi huo kamati imeitaka TFF kuwachukulia hatua baadhi ya watendaji wa bodi kwa kupotosha kamati ya saa 72
Source muungwana