GE2025 Kagera: Viongozi wa CHADEMA washikiliwa na Polisi kwa kuchochea vurugu

GE2025 Kagera: Viongozi wa CHADEMA washikiliwa na Polisi kwa kuchochea vurugu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewakamata baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za kuhusika na kupanga mikutano na maandamano kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Brasius Chatanda, amethibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini ukweli wa madai hayo

Soma pia: Jeshi la Polisi lajipanga kudhibiti vurugu siku ya Uchaguzi

1761398146360.png

Amesema “Ni kweli tunawashikilia viongozi hawa pamoja na wanachama wengine watatu wa chama, wanatuhumiwa kuchochea machafuko ya umma kwa kuandaa maandamano, ni miongoni mwa watu 17 tuliowashikilia katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi,” alisema Kamanda Chatanda.

Imeelezwa viongozi hao wanadaiwa kuhusika katika kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kushiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Kamanda Chatanda amesema hatua zaidi zitachukuliwa mara baada ya uchunguzi kukamilika. Jeshi hilo pia limewataka wananchi kuwa watulivu na kufuata sheria wakati wa kipindi hiki cha kisiasa.
 
Msajili anatakiwa kukifuta chama hiki ambacho badala ya kushiriki uchaguzi kinachochea vurugu
 
Msajili anatakiwa kukifuta chama hiki ambacho badala ya kushiriki uchaguzi kinachochea vurugu
Tafsiri ya kuchochea vurugu ni ipi mjinga wao?

Halafu msajili alisharudisha kadi ya CCM.?

Wapi katika katiba pameandikwa maandamano ni vurugu?
 
Back
Top Bottom