Kagera: Mkoa Usiojua Mgao wa umeme ukoje, wenye viwanda hamieni Kagera!

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Pamoja na nchi kulalamikia mgao wa umeme unaoendelea baadhi ya watu walioishi hapa Kagera kwa muda mrefu wanashangaa nikiwemo mimi niliyehamia mwaka mmoja uliopita Kutoona hata siku moja ukiacha tatizo la kiufundi eti umeme wa mgao!! Huku masaa yote umeme upo tu. Ikabidi niulize inakuwaje? Nikaambiwa aaahhh umeme wa hapa unatoka hapo nchi jirani Uganda japo bili unalipia Tanesco. Sasa nikaanza kufikiri kuwa hao wenye viwanda mbaimbali waliosotisha uzalishaji sababu ya kukosa umeme, walete huku mitambo yao maana umeme full time loh!! Kazi yao iwe ni kusafirisha mali ghafi au kufanya taratibu ya kuzizalisha hapa, maana mkoa huu almost kila zao kwa mfano wale wa mafuta, linaota isipokuwa watu wa huku wavivu ile mbaya. Ardhi ina maji kibao lakini loh!! nani alime mpunga, mpaka wasukuma wachache ndo wameshtukia dili wanaanza kulima na wanavuna mpunga mnene kinoma. Ebwanae mwenye Capital aje tufanye business. Huku natoa tahadhari kwa mgombea yeyote katika ahadi zake asiongelee kuwa kuna kero ya umeme labda kuufikisha mahali usipo. Pia nimeshangaa hadi migombani umeme unawaka, nyumba chache tu kwenye kijiji ambacho kuna nshomile aliyeko out au Proffessors, umeme utakwenda tu loh. Haya jamani njooni huku muwekeze maana utadhani sio Tanzania hapa!!!!>
 
Sumbawanga umeme unatoka Zambia, hawajui mgao ni nini
Mtwara na Lindi wanatumia umeme wa gas wa Artumas, hawajui mgao ni nini
Ruvuma na wilaya zake wanatumia umeme wa jenerator, hawajui mgao ni nini
 
Pamoja na nchi kulalamikia mgao wa umeme unaoendelea baadhi ya watu walioishi hapa Kagera kwa muda mrefu wanashangaa nikiwemo mimi niliyehamia mwaka mmoja uliopita Kutoona hata siku moja ukiacha tatizo la kiufundi eti umeme wa mgao!! Huku masaa yote umeme upo tu. Ikabidi niulize inakuwaje? Nikaambiwa aaahhh umeme wa hapa unatoka hapo nchi jirani Uganda japo bili unalipia Tanesco. Sasa nikaanza kufikiri kuwa hao wenye viwanda mbaimbali waliosotisha uzalishaji sababu ya kukosa umeme, walete huku mitambo yao maana umeme full time loh!! Kazi yao iwe ni kusafirisha mali ghafi au kufanya taratibu ya kuzizalisha hapa, maana mkoa huu almost kila zao kwa mfano wale wa mafuta, linaota isipokuwa watu wa huku wavivu ile mbaya. Ardhi ina maji kibao lakini loh!! nani alime mpunga, mpaka wasukuma wachache ndo wameshtukia dili wanaanza kulima na wanavuna mpunga mnene kinoma. Ebwanae mwenye Capital aje tufanye business. Huku natoa tahadhari kwa mgombea yeyote katika ahadi zake asiongelee kuwa kuna kero ya umeme labda kuufikisha mahali usipo. Pia nimeshangaa hadi migombani umeme unawaka, nyumba chache tu kwenye kijiji ambacho kuna nshomile aliyeko out au Proffessors, umeme utakwenda tu loh. Haya jamani njooni huku muwekeze maana utadhani sio Tanzania hapa!!!!>

My take
Mimi niko Kagera.napenda ujue jambo moja tu,hizo furaha za uwepo umeme wa uhakika kwa sasa katika mkoa huo ni za muda tu,ipo siku tutalia kilio cha kusaga meno na tutawalilia wenzetu wa mikoa ya jirani walioko katika grid ya taifa.
Kwa nini:Kagera inategemea umeme kutoka uganda ambapo unatokana na mkataba baina ya nchi hizo mbili uliofanywa na Mwl Nyerere miaka hiyo.Hivyo mkataba huo ukiisha basi Kagera itakuwa gizani kwani grid ya taifa haijafika hapa.

Kumbuka taarifa za karibuni ni kuwa kumeanza chokochoko nchini humo,wakilalama kwamba inakuwaje wao (uganda) wakoe umeme kwa baadhi ya siku huku umeme wanawagawaia watanzania(kagera).Ikitokea mkataba huo ukvunjwa Twafaa!

Kumbuka "Nguo ya kuazima................................."

Byabato

safi sana Ta Muganyizi nimekupata kukaribisha wawekezaji na wenye viwanda kuja kuwekeza hapo mkoani kagera maana ni kweli kabisa huko hawajui makali ya mgao wa umeme unaondelea na haufahamiki hutaisha lini.Kama mwandishi wa mashairi Shabani Robert katika kitabu chake cha DIWANI YA MLOKA katika moja ya mashiri yake linalosema karibu watanzania kusini nami nasema twende watanzania tukawekeze mkoani Kagera.

Nimekupata Ta muganyizi - kutoka Iringa.
 
Back
Top Bottom