We jMali... Kwa taharifa yako unabahati sana hauko huku na mungu akusaidie ubakie huko huko, hizo sumu zako huku zingekucost sana.
Jumapili wenzako ni siku ya kwenda kanisani au kutembelea/kutembelewana ndugu/majamaa, chakushangaza ndugu yangu wewe; ndio siku yako kuu yakuharibu na kunadi ukabila? Kwa hiyo ntaongeza kukupata live Jumapili? Kanisani ntaacha; nisalie nyumbani, nikifanikiwa kukutowa pepo wabaya kama wanzako walio rudi makwao na hivi wanakula bata tu, nina imani mbele ya mungu itakuwa ni sara isiyo nakifani.
Rwanda unayo fikilia/pendekeza, siyo hivyo! Huku kwenu nidhamu sio jambo la hiari bali ni an obligation kwa kila mkazi/mgeni wa Rwanda. Na hilo jambo nililishuhudia mwaka 1995 nilipoenda kumpokea mgeni, ndugu yetu kabisa wakitanzania, kipindi hicho bado Kagame hajatuletea 4G network, ikabidi mgeni wetu tumuelekeze Parking ya malori yanayotokea nchi za nje, kufika pale tukakuta mzee ana kesi ya kusingiziwa kufungua mlango wa Gari yake na kumgonga mwanajeshi aliye vaa kiraia, kusudi tu atoe kidogo dogo, kutuona ilikuwa kama sherehe, akaanza kutuambia jinsi matatizo yalivyompata, kajaribu kuonga lkn mwanajeshi anataka pesa kubwa, ingawa nilikuwa na Baba yangu mzazi, ushenzi wa yule mwanajeshi ulinifanya nimpe makofi ya harakaharaka na kwa bahati mbaya/nzuri kulikuwa na patrol ya wanajeshi, kutuona tu wakaja, waka mruhusu mdingi apeleke mgeni wake nyumbani kwanza, halafu arudi kufwatilia kesi, yule mgeni hata hakukubali basi tukaenda wote kituoni, wote tukajieleza kwa bahati nzuri kumbe yule jamaa alikuwa kajipatia week end kutoka kambini bila ruhusa weee mbona alikoma!!! Ingawa nilikuwa na kesi ya kumzaba vibao mwanajeshi mwenzao; kumbe makosa yake yalikuwa makubwa kuliko yangu jamaa kazi yake ilikuwa kubananisha watu wenye platenumber za nje ya Rwanda na kuwala pesa kwa visingizio, Sisi tukaruhusiwa kwenda nyumbani, kwani niliact ku defend mgeni wa Rwanda na kumtoa mikononi mwa maharamia waliokuwa wakitaka kumdhulu, weee Mgeni wetu mbona alitaka kuzimia, eti kuanzia leo najipa ubalozi wa Rwanda popote nta'po enda, nakusema eti pamoja na uzee wake ni mara yake ya kwanza kushuhudia haki kati ya raia na mwanajeshi ikitendeka.
Rwanda ya leo siyo ile utakayo ipata kwenye inyenyeri au Jambo news jMali, ni Rwanda ya wenye malengo na wajasili, tulioamua kufanya miujiza iliyo ishinda dunia, najuwa itakuwa vigumu kwako kuelewa ila hakuna utakacho badilisha, mwendo mdundo mpaka mwisho.
Naona Jumapili uliamuwa kuharibu kabisa! Eti ulikuwa ujuwi kwamba yatima anaweza kuwa na mzazi? Kivipi? Hivi hujuwi kwamba unaweza kuwa na wazazi lakini usiwe na walezi? Sumu zako zinasema tumuiteje mtu wa hivyo? Ukabila wako unakuambia eti uhutu wako ni kabila? Unajidanganya sana, huo uhutu wako ni ukoo tu kwa sababu hamna lugha zaidi ya kinyarwanda! Hebu tazama kabila la wahaya, lugha yao ni kihaya is ndio? lakini humo humo wenyewe wanasema eti wana wahutu na watutsi, kama huamini we waulize wahaya wanaoitwa WARANGIRA au ... ndio utajuwa nnachokuambia.
Wacha kupotosha watu, mi binafsi nakuomba urudi nyumbani kwani hamna utacho badilisha ukiwa nje hata shemeji yako profeseri tushamuambia yale maneno yake, asimung'unye wala asiteme ila ameze tu! Ndio maana unaona yameanza kumtokea kwa chini, fanya mchezo na wauwaji! Mkee mkikenuliana huko huko, kwetu madhala yake tunayajuwa, na hatuhitaji mwalimu.