Kagame ni Shujaa

Pato la wastani Rwanda(per capita income)kubwa kuliko la Tanzania. Hivo kwa ujumla warundi wanaishi maisha mazuri kuliko Mtanzania.
Sasa kinachowafanya wakimbilie TZ ni nini? Ndio matatizo ya kusoma report bila kuwa na kanuni za uchumi kichwani. Kama per capita income ingekuwa inareflect unachoongea basi waafrika wengi wasingekimbilia South Africa bali wangejazana Equatorial Guinea, wasingekimbilia USA, Ulaya na hata china wangeelekea Brunei. Halafu Tanzania isingekuwa na Tatizo la Wahamiaji haramu.
 
Wakuu, Nimefatilia Mkutano wa viongozi wa Afrika na Obama huko Marekani.

Kagame kampa za uso Obama na kumwambia aachane na hotuba za miaka nenda miaka rudi.

Kwakweli huyu Raisi ameonyesha kwamba yeye siyo legelege kama naniihii.
Kweli waafrika hatuna vipaumbele! Kagame kapayuka tu mtu anasema shujaa? Kwani Obama anashida na mtu anayemkosoa? Yaani mtu katoka kigali amepania kupinga speech ya obama tu? Kama amepinga hotuba ya obama yeye amekuja na solution gani ya kutatua matatizo? Au ni ile ile solution yake ya kuu kila anayempinga.
 
Kama ni kusema mbona hata Dr. Slaa alisema? Kuna haja gani ya kuiuza nchi kwa kagame wakati kuna watz wanauwezo na uchungu na nchi?

Dr. slaa yeye alisema angehalalisha gongo...da bongo raha sana pamoja na umaskini wetu..yani kama ze comedy..
 
Watu nawashangaa wanaisifia Rwanda kwa kusoma magazetini....hawashangai hakuna sehemu ingine inayosifiwa zaidi ya Kigali....

Ni sawa usifie O'bay wakati pande nyingine za Dsm ni kituko...

Mshikaji wangu ametoka huko juzi kati...nimemuuliza umeenda wapi zaidi ya Kigali...ananambia sehemu nyingine haziko accessible kirahisi...milima na barabara mbovu...sasa hapo kumbuka ukubwa wa nchi ni kama mkoa lakini si full lami...na watu wanapiga kelele humu...



 
Simplemind; kwanini unazungumzia pato LA Rwanda harafu unamzungumzia maisha ya warundi?. OK, OK, OK, nimekuelewa, hata Tanzania in muungano wa Tanganyika na Zimbabwe. No problem

Meant Rwandese
. Samahani.
 

Sawa. Rwanda data is relatively symmetrical therefore your argument does not hold water. Sema jengine. Ndugu zako CCM have screwed the economy proper.
 
nikishapata hotuba nzima ya alichokuwa anazungumzia na muktadha ulikuwa ni nini nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusema chochote ngoja nitafute





Nakubaliana na wewe kwa 100%.
Waafrika wengi hawafikirii sawasawa.
Hilo ndilo tatzo mtu anakurupuka tu na kuanza kuponda bila kuangalia kuwa kwenye soko huria ukubwa wa nchi na wingi wa watu ni mtaji mkubwa sana wa kuibua fursa za kiuchumi
 
Pato la wastani Rwanda(per capita income)kubwa kuliko la Tanzania. Hivo kwa ujumla warundi wanaishi maisha mazuri kuliko Mtanzania.

Mkuu am sorry to say this is absurd. Inakuwaje pato la wastani la Rwanda liwe kubwa kuliko la mtanzania, halafu mtu wa burundi ndio awe na maisha mazuri kuliko mtanzania? Hakuna nadharia yoyote ya uchumi inayoweza kusema kwakuwa Per capita income ya mtu wa Rwanda iko juu kuliko ya mtu wa Tanzania, kwa hiyo mtu wa burudi ana maisha mazuri kuliko mtanzania.

Hata kama utakuwa umekosea, unajua per capital income si kigezo kizuri cha kuonesha maisha mazuri ya watu katika nchi fulani? Unajua inawezekana kuwa per capita ya Mzanzibar ni kubwa kuliuko ya mbara, lakini inawezekana si kweli mzanzibar ana maisha mazuri kuliko mbara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…