Kagame ever a hero of the our time | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagame ever a hero of the our time

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by king kan, Jul 1, 2012.

 1. king kan

  king kan JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,267
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  KAGAME A HERO
  Its a precious thing that in my life I have lived to witness a nation growing from a disconsolate and direful situation to a nation that is approaching zenith. Katika kipindi hiki ambacho sisi vijana historia imekuwa mwalimu wetu katika kutuelezea jinsi ambavyo yaliinukia mataifa zamani na kuandika historia duniani chini ya viongozi shupavu kama Urusi enzi za V.I. Lennin na Marekani enzi za T. Roosevelt najisikia furaha angalau kuwa mmoja wa watu ambao nimefanikiwa kuyaona mafanikio ya Rwanda katika kipindi cha miaka yake 50 ya uhuru.
  Lakini ntakuwa sijatenda haki kama kiongozi mahiri na shupavu huenda kuliko wote wa kizazi hiki kinachoshikilia madaraka sasa ambaye amekuwa nguzo imara katika maendeleo ya Rwanda tangu alipoteuliwa kuongoza taifa hilo katika kipindi ambacho ndio kwanza taifa hilo lilikuwa limetoka katika mauaji ya kikabila na kikoo ya mwaka 1994.
  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema, nanukuu ;
  "In Tanzania, it was more than one hundred tribal units which lost their freedom; it was one nation that regained it"
  Kauli ya Hayati Baba wa taifa inanifanya kutathmini kwa kina ambacho kwa hakika serikali ya Raisi Paul Kagame imeweza kukifanya kuwa kweli ambapo kwa sasa Rwanda ni nchi ambayo raia wake wanaishi maisha ya upendo na mshikamano. Ni hali ya kushangaza kabisa watu wa Rwanda nchini Rwanda watu wameweza kuwasamehe hata waliowaua wazazi wao na sasa wanaishi pamoja mitaani. Serikali ya Raisi Kagame imejitahidi kuliunganisha Taifa hilo kitu kinachonipa wakati ngumu ni kwanini wakati kiongozi kama Kagame amewaunganisha Wanyarwanda wote na wameondoa itikadi zote zinazoweza kuwatenga. Ni kwanini viongozi wa muungano wameshindwa kuondoa kero ya udini ambayo hata hivyo mara zote wameshindwa kukiri wazi kama upo?
  Katika kipindi hiki ambapo kiongozi shupavu Kagame anaweza kuongoza serikali na nchi yake kusherekea miaka 50 ya uhuru tunayomambo muhimu ya kujifunza.

  1. Hali ya uchumi nchini mwake. Leo hii Rwanda imepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kuliko nchi nyingine ndani ya kanda yetu hii. Naikumbuka kauli ambayo Rais Kagame amekuwa akiitoa mara nyingi
  "Kama nchi za Asia Mashariki zimekuwa zinakua kwa kasi katika sekta za maendeleo kwa nini sisi tushindwe"
  Ni kauli hizi huweza kutamkwa na viongozi thabiti.Ni dhahiri ukienda Rwanda huhitaji kuoneshwa ili kuona mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali.Ukichunguza kwa makini utagundua kwamba huduma za jamii kama elimu, afya, makazi bora, ulinzi na usalama, maji na umeme zimewafikia karibu wananchi wote wa taifa hilo. Tena zinatolewa kwa ubora na usawa unaokidhi viwango.

  2. Uwajibikaji wa watumishi wa umma. Hali ni tofauti sana katika nchi ya Rwanda kuliko mataifa mengine ya East Africa. Huduma nchini Rwanda zimekuwa zikitolewa kwa wananchi bila rushwa, upendeleo wala kwa kufuata itikadi flani, huduma hizi kwa umma zimekuwa zikitolewa ndani ya muda mfupi tofauti na kwa ubora bila bugdha.

  3. Mgawanyiko wa Rasilimali. Ardhi ni rasilimali ya muhimu nchini Rwanda kwa kuwa nchi hiyo haina deposits nyingi za madini au wanyama kama sisi tulivyojaaliwa. Sera za ardhi nchini Rwanda imetoa furrsa kwa kila mzawa kumiliki ardhi kiasi cha kutosha kwa ajili ya mahitaji yake na kwa kuzingatia mahitaji ya jamii nzima kwa ujumla. Inashangaza kuona hata kucopy na kupaste ili tuweze kuwa na sera ambayo itaweza kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji au wananchi na wawekezaji.
  Makala haya yaweza kuwa marefu kwani wenzetu wamefanya makubwa sana katika kipindi kifupi chini ya Gen. Paul Kagame kwa mfano angalia sekta za miundo mbinu, ubora wa huduma za usafiri, makazi, usalama wa raia na mali zao, usafi na mpangilio wa miji n.k

  TAREHE 1 JULY 2012 WAKATI WANASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU WAO NI VIZURI WOTE KWA PAMOJA TUKAUNGANA NAO KAMA ISHARA YA KUKUBALI MAFANIKIO YAO NA UJIRANI MWEMA.

  RWANDA WAMETHUBUTU, WAMEFANIKIWA NA WANAZIDI KULETWA PAMOJA NA KUUNGANISHWA JEMEDARI PAUL KAGAME KUELEKEA KWENYE KILELE CHA MAFANIKIO.
   
 2. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kuna haja ya kuandamana tushinikize tuwe chini ya Kagame badala ya AHDIUF na WOLAIL LANIWE!
   
 3. n

  nyabhera JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  kuna kujenga taasisi ya kiadilifu na inayoendeleza taifa na kiongozi mmoja kusimamia uadilifu ana kuleta maendeleo kwa incha ya upanga na risasi. aliwahi kuwapo Gamal wa misiri alileta maendeleo Misir alipokufa kila alichoanzisha kikafanaye
   
 4. T

  Tendulkar222 Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Big up Afande KAGAME. He's the man of this generation. Hakuna wa kumfikia aisee, kiongozi shupavu sana, MZALENDO na mwenye VISSION.

  ANGEKUWA tanzania, tungekuwa mbali sana jamani!
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka kauli ya Major Kagame, pale aliposema Nikipewa kuiongoza Tanzania, kwa mbuga za wanyama peke yake nitaifanya kuwa Japan!
   
Loading...