Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,714
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, amedai kuwapo kwa mkakati wa kuzuia ripoti ya uchunguzi wa fedha za Escrow zaidi ya Sh. bilioni 400, isijadiliwe katika mkutano ujao wa Bunge mjini Dodoma.
Kafulila ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa kuulinda ufisadi wa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambao alidai unafanywa na kampuni za ufuaji umeme na baadhi ya vigogo wa serikali.
Soma pia: Uzi maalum wenye matukio yote yaliyojiri kwenye sakata la ufisadi wa ESCROW
Kwa mujibu wa Kafulila, kumekuwapo na kampeni ya kupotosha ukweli kuhusu madai ya ufisadi huo wa fedha ambao anadai unaratibiwa na baadhi ya watu waliojitoa kufahamu kutetea wizi.
"Napenda kusisitiza kwamba, fedha za Escrow Dola milioni 270 (zaidi ya Shilingi bilioni 400), zimetolewa kifisadi na ndiyo sababu kwa muda sasa kumekuwapo mkakati wa kuzuia ripotri za uchunguzi zisijadiliwe bunge lijalo," alisema Kafulila na kuongeza:
"Wito wangu kwa serikali ni kuwa endapo ripoti hii haitaletwa,Bunge lijalo halitakalika. Nitapeleka hoja ya kutokuwa na imani na serikali."
Alisema kutokana na hali hiyo, hadi sasa nchi wahisani hazijachangia bajeti kwani zinasubiri utekelezaji wa ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kwa mujibu wa Kafulila, anao ushahidi wa nyaraka takribani 600 zinazothibirisha fedha hizo kutolewa kifisadi huku akihoji sababu za Takukuru na CAG kutotoa taarifa za uchunguzi kuhusu madai hayo.
Alisema, ripoti hiyo isipojadiliwa kwenye Bunge hilo, ataomba mahakama itoe amri kwamba mbunge asiwe mjumbe wa bodi ya mashirika ya umma na kutoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na Rais.
Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, alisema, hakuna mtu anayeweza kukwamisha kazi yao na kuwa muda wowote ripoti ikiwa tayari wanaiwasilisha.
CHANZO: NIPASHE