Kafulila: Upo mkakati kuzuia ripoti fedha za Escrow

Kafulila: Upo mkakati kuzuia ripoti fedha za Escrow

Ni haki yako kujadili ndoa ya kafulila kama yako ipo imara ila suala langu ni kwamba wewe utavumilia na sisi tukianza kujadili ndoa ya Kikwete na Makahaba anaotembea nao na watoto aliozaa nao na watu waliofungwa kwasababu ya ufuka huo???

Mbona umepanic mkuu na we mmoja wapo nini

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Kafulila anazungumziaje tuhuma za yeye kupokea
milioni tisini kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa
walioathirika na kitendo cha waziri mpya wa nishati na
madini sospeter muhongo kufunga mirija ya kifisadi
waliyokuwa wanatumia kujinufaisha na kuifilisi nchi
(rostam,mengi,mkono) ili awachafue na kuwakomoa muhongo
na katibu wake maswi?
sasa hizi ndizo hoja za kiume,achana na story za fulani kapolwa mke.
ungeuliza hivi mwanzo hapo ni lazima akujibu na bado ni jukwaa la siasa mambo ya ndoa peleka MMU.
 
Mi nashangaa, kwa nini tunarazimisha kuwa na imani na serikali hii baada ya matukio makubwa ya kifisadi namna hii? Ni bahati mbaya tu kuwa hakuna vyombo thabiti vya kukimbilia kuwabana rais na waziri wake mkuu kuwajibika.

Nchi nyepesi kuongoza ni Tanzania chini ya ccm na polisi wao. Rais anaweza amua kufanya chochote atakacho au kutokufanya anayopaswa kufanya na asidhurike chochote.
 
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, amedai kuwapo kwa mkakati wa kuzuia ripoti ya uchunguzi wa fedha za Escrow zaidi ya Sh. bilioni 400, isijadiliwe katika mkutano ujao wa Bunge mjini Dodoma.

Kafulila ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa kuulinda ufisadi wa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambao alidai unafanywa na kampuni za ufuaji umeme na baadhi ya vigogo wa serikali.

Kwa mujibu wa Kafulila, kumekuwapo na kampeni ya kupotosha ukweli kuhusu madai ya ufisadi huo wa fedha ambao anadai unaratibiwa na baadhi ya watu waliojitoa kufahamu kutetea wizi.

"Napenda kusisitiza kwamba, fedha za Escrow Dola milioni 270 (zaidi ya Shilingi bilioni 400), zimetolewa kifisadi na ndiyo sababu kwa muda sasa kumekuwapo mkakati wa kuzuia ripotri za uchunguzi zisijadiliwe bunge lijalo," alisema Kafulila na kuongeza:

"Wito wangu kwa serikali ni kuwa endapo ripoti hii haitaletwa,Bunge lijalo halitakalika. Nitapeleka hoja ya kutokuwa na imani na serikali."

Alisema kutokana na hali hiyo, hadi sasa nchi wahisani hazijachangia bajeti kwani zinasubiri utekelezaji wa ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kwa mujibu wa Kafulila, anao ushahidi wa nyaraka takribani 600 zinazothibirisha fedha hizo kutolewa kifisadi huku akihoji sababu za Takukuru na CAG kutotoa taarifa za uchunguzi kuhusu madai hayo.

Alisema, ripoti hiyo isipojadiliwa kwenye Bunge hilo, ataomba mahakama itoe amri kwamba mbunge asiwe mjumbe wa bodi ya mashirika ya umma na kutoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na Rais.

Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, alisema, hakuna mtu anayeweza kukwamisha kazi yao na kuwa muda wowote ripoti ikiwa tayari wanaiwasilisha.

CHANZO: NIPASHE

Kwahyo KAFULILA unataka tuungane nawewe katika kuupotosha umma??? Wananchi tumestukia mchezo mchafu wa KAFULILA tunajua kuwa unatumika na pande nne kwenye upuuzi huu ambao sasa wananchi wamekosa imani nawewe. Tunajua umevuta mrungula kutoka kwa MKONO, MENGI na ROSTAM na hivi majuzi umepata ufadhiri mpya kutoka kwa STANDARD CHARTERED BANK- HONG KONG.
Unazidi kuudanganya umma kwakudai kuwa unanyaraka zaidi ya 600, kwa hulka yako wewe KAFULILA kama ungekuwa na nyaraka unazozisema lazima tu ungemake head lines wewe ili kujipa kick na mabosi wako wakupongeze. Tunakumbuka wote bungeni ulivyokuwa unapeperusha karatasi zako za kufungia vitumbua kwa kudai kuwa ni nyaraka za siri juu ya escrow account. Wewe KAFULILA huna nyaraka yeyote inayoweza kuthibitisha kuwa utoaji fedha kwenye escrow account ulikuwa wa kibabaishaji. Wanajamvi wote tunakumbuka hii thread;

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ndal-confidential-files-you-need-to-read.html

Kwa ambao hawafahamu hii thread imetolewa humu;

Ten Files You Should Read About Tegeta Escrow Account Scandal | Tegeta Escrow Scandal


Hii ni word press ya kina Kafulila
Na KAFULILA ameandika ukidhama kwenye hyo link utaona;
These are ten important documents that one must read if he really wants to get himself educated on the scandal.
Wote tulipata nafasi ya kuziona hizo files humu na hata ukirudi kwenye mjadara ulivyokuwa humu JF utapata conlusion moja, hizo file hazina mashiko ya kumfanya mtu aseme kuna ushahidi wakutosha kuiita moja ya ushahidi kuwa kuna ufisadi uliofanywa na IPTL/PAP.Huu ni mchezo mchafu ambao KAFULILA anacheza kama kweli slogan yetu kwasasa ni NGUVU YA UMMA kwanini kafulila aaniki hizo files ili hata sisi mbao hatukubaliani nae pamoja na umma tuweze kuwa mbele ya KAFULILA katika kudai serikali iwawajibishe mafisadi ambao watakuwa wamebainika. TUNAMWOMBA KAFULILA ATOE USHAHIDI ALIONAO MBELE YA UMMA KAMA HANA BADALA YA KUENDELEA KUBWABWAJA BASI AUFYATE.
KAFULILA huna ushahidi ungekuwa nao ungeshauanika kwenye ki Blog chenu mlichokianzisha kwa ajili ya sakata la escrow kama mlivyoweka hizo ten file mkaziita confidential files.
Wewe KAFULILA ndio upo kwenye kampeni ya kupotosha umma iliyofadhiliwa na mafisadi wakina MKONO,MENGI, ROSTAM na SCB-HK.
 
Kuna juhudi kubwa sana zinazofanywa na mafisadi kumchafua Kafulila ili kuzima habari zinazohusiana na wizi huu na hata kuwaweka watu hapa ambao wengi wao wamejiunga siku za karibuni kupost mabandiko mbali mbali ya kumchafua Kafulila. Inaelekea hawa ni wahusika waliolipwa mapesa chungu nzima na mwizi rugemarila au wamewekwa hapa na hao mafisadi mbali mbali waliopokea mabilioni ya pesa za wizi akiwemo fisadi Tibaijuka.
 
Hatuwezi wote kuwa na mawazo sawa kama ya KAFULILA, mimi binafsi haja nishawishi kabisa. Siku zote mtu anae cheza na minds za watu huja na hoja nyepesi kama za KAFULILA, una nyaraka zaidi ya 600, ziko wapi?? kwa manufaa ya nani?? kama una nyaraka zaidi ya 600 kwanini usije nazo kwetu wananchi?? Vita dhidi ya ufisadi siyo ajenda ya mtu mmoja mmoja, lakini kwenye hii vita Kafulila anapigana peke yake na msaada mdogo kutoka kwa Zitto, kwanini??? jibu ni kwamba Kafulila bado hajawa na hoja zenye mashiko mbele ya umma, mimi nipo tayari kuwa mbele ya Kafulila kama yupo tayari kuachia hizo nyaraka mbele ya umma.
 
Kuna juhudi nzito sana za kumziba mdomo Kafulila, kwa maoni yangu nchi hii ilivyoingiliwa na mafisadi ambao hawaogopi lolote lile basi si ajabu wanaweza hata kumuwinda huyu ili wachukue uhai wake.

MWENZETU ULIINGIZIWA NGAPI? mwenzio mama Tiba aliwekewa bil 1.663 tshs.
 
Hii ni baadhi ya hoja nilizo hoji wakati zile nyaraka za Kafulila zinajadiriwa humu JF; Kama Kafulila anazo nyaraka nyingine zenye mashiko zaidi ya hizi namwomba Kafulila azitoe ili watanzania mara moja tumsaidie kubeba mzigo uliomtesa muda mrefu na mimi binafsi ntamuomba radhi humu JF kwaku mbeza kwenye hili sakata.


Minamshukuru sana aliyeleta hizi files sababu amesaidia sana kuonesha nikwanamna gani IPTL wanastahili kulipwa Fedha za ESCROW account. Hizi files zinatuonesha waziwazi kwamba KAFULILA alikuwa anatumika kwa kubadilisha maneno kiujanja ujanja na kupotosha ukweli kwamba pesa hizi hazistahili kulipwa kwa IPTL

View attachment 189476

kwakutumia Pdf no. 9 yenye kichwa cha habari:

View attachment 189490

Tunagundua kwamba kulikuwepo na makubaliano ya IPTL kulipwa fedha zilizopo kwenye account ya escrow. Lakini vikao vilifanywa kudiscuss masuala muhimu kama kodi, capacity charges na mengineyo:

View attachment 189497

Lakini tunaona tena upotoshaji uliokuwa ukifanywa na KAFULILA na timu yake hapa chini:

View attachment 189498

Huu ni upotoshaji, mfano kama argument inasema huyu provisional liquidator anaiachia majukumu yote PAP/IPTL ukijumlisha na mitambo, navilevile PAP anajicommite kubeba deni lote la IPTL je kwanini asichukue fedha ya ESCROW??? KWAHIYO TUNAMRUHUSU PAP ABEBE MADENI YA IPTL NA SIYO HAKI NYINGINE ZA IPTL KAMA FEDHA ZA ESCROW????
View attachment 189499
Naikumbukwe kwamba wakati fedha ya ESCROW inalipwa tiyari kulikuwa na muafaka wa kupunguza capacity charge:

View attachment 189501

Jaribu nawewe sasa kutafakari alafu tuulizane!


View attachment 189502
Kwahiyo tusimpe sasa PAP hela ya IPTL iliyopo kwenye ESCROW account?? KAFULILA anajitoa ufahamu nakujifanya hajui kuhusu ESCROW AGREEMENT!!!
Tukumbuke pia hukumu ya Jaji UTAMWA ilibase kwenye Dispute baina ya wabia wa IPTL, Na hukumu ya ICSD ilishatolewa kwa kuzitaka pande zote mbili kukaa na kukokotoa upya mahesabu na pande zote zilikaa na kufanya hivyo, soma kidokezo hapo juu.

IPTL: NYUMA YA PAZIA | TAIFA IMARA
 
Hatuwezi wote kuwa na mawazo sawa kama ya KAFULILA, mimi binafsi haja nishawishi kabisa. Siku zote mtu anae cheza na minds za watu huja na hoja nyepesi kama za KAFULILA, una nyaraka zaidi ya 600, ziko wapi?? kwa manufaa ya nani?? kama una nyaraka zaidi ya 600 kwanini usije nazo kwetu wananchi?? Vita dhidi ya ufisadi siyo ajenda ya mtu mmoja mmoja, lakini kwenye hii vita Kafulila anapigana peke yake na msaada mdogo kutoka kwa Zitto, kwanini??? jibu ni kwamba Kafulila bado hajawa na hoja zenye mashiko mbele ya umma, mimi nipo tayari kuwa mbele ya Kafulila kama yupo tayari kuachia hizo nyaraka mbele ya umma.
.....uwe mbele ya Kafulila ili akufanye nini? nilikuwa nauliza tu!
 
.....uwe mbele ya Kafulila ili akufanye nini? nilikuwa nauliza tu!

Lengo nikuubeba ujumbe wa Kafulila ambao muda mrefu sasa amekuwa akihangaika peke yake kuueneza bila kupata msaada na kama nilivyosema tatizo ni kuwa hoja yake bado haina mashiko; Nnaposema nipo tayari kuwa mbele ya Kafulila maana yangu ni kwamba nitakuwa tayari sasa baada ya kuziona hizo nyaraka 600 za Kafulila kuubeba ujumbe wa ufisadi ambao kwasasa Kafulila anajaribu kuuneza bila mafanikio na bila kuungwa mkono na wananchi wala kundi kubwa la wanasiasa wenzake.
 
Huu ulikuwa mchango wangu kwenye vile vinyaraka kumi alivyovitoa Kafulila;

http://escrowscandaltz.wordpress.com/2014/08/24/important-files-you-should-about-tegeta-escrow-account-scandal/

""Sijui Mbunge Zitto Kabwe alicomment nini wakati anapost hizi files kwenye facebook account yake, lakini kama dhamira yake ilikuwa kutaka kutuendelezea ule mchezo mchafu basi kwenye hili mimi binafsi na mpuuza nakumwona kama kibaraka wa mabeberu, sababu ya kusema hivi ni moja kwakumbukumbu inaonyesha pia ushiriki wa ZITTO kwenye kuwapotosha wananchi huku akitumia karata yake ya imani ambayo wananchi wanayo juu yake.
Hili sakata la IPTL kabla kina ZITTO na KAFULILA kulidakia,ilikuwa nikampeni ya mabeberu kuilazimisha serikali kuwapa dili ya kuuza umeme kupitia kampuni yao ya SONGAS. Hawakulidhishwa na serikali kutoa dili kwa nchi ya malaysia, mwendelezo wa hili sakata ulipamba moto baada ya watu wenye interest tofauti kudakia na kuanza kuishambulia serikali kuwa kuna ufisadi kwenye mradi wa IPTL,lakini ikumbukwe kuwa hivi nilini mabeberu walifanya kitu kwamaslahi ya nchi maskini na ndio maana Tanzania kwa mara ya kwanza tulipotaka kampuni binafsi ya kwaajiri ya kuzalisha umeme suruhisho letu kama nchi lilikuwa Malaysia kupitia South-south Commision.
Mabeberu kupitia BRIAN COOKSEY walianza kutuandama kwa lugha chafu sababu tu IPTL imeiside line SONGAS:

View attachment 189515

Malalamiko yanayotengenezwa na BRIAN COOKSEY yanabase kwenye kutaka kuimbua serikali kuwahaikufanya uamuzi mzuri ilipokubari kuipadili IPTL. Lakini je dili ya SONGAS ingekuwa na tofauti kweli naingelinda maslahi ya wazalendo kweli?? nimataifa mangapi ya kibeperi yamewekeza kwenye sekta kubwakubwa lakini bado wazalendo tunalia na mikataba yao??

View attachment 189516

Lakini tunaona sasa kwamba pamoja na ubungo gas turbines kufanya kazi bado tunawahitaji IPTL,na BRIAN COOKSEY yupo kimya kabisa toka atoe chapisho lake, hii yote nisababu anajua mabeberu wamepata walichokuwa wanahitaji SONGAS kuwa operational.
Lakini IPTL waliliona hizi hila za BRIAN COOKSEY:

In a long letter to the African (1 June 1998) titled ‘Brian's phobia against South-South Commission', I am dubbed a racist with a ‘pathological hatred of South-South cooperation', with ‘derogatory tendencies towards African governments, leaders and its people.' In a letter to Minister of Planning, Nassoro Malocho, IPTL copied an article that appeared in East African Alternatives, and accuse me of having vested interests in Songas. I am referred to as a ‘dangerous underground advisor,' ‘an academic and business crook,' with ‘prejudices against African and Asian leaders'.

Kilichofuata wote tunajua, waandishi waudaku wakina MIHANGWA wakatafsiri maandishi ya udaku ya BRIAN nakuyasambaza. Nasasa tunamuona ZITTO na KAFULILA wakiyabeba maneno yaleyale na kuyasambaza kwa umma, mfano ZITTO anarudiarudia sana kusema "Wapinzani, vyombo vya habari na civil society vimelikalia kimya sakata hili" nikitu kilekile alichokindika BRIAN kwenye udaku wake:

""View attachment 189517

Watanzania wenzangu hapa tunachokiona ni mchuano mkali wa kibiashara ambao ndani yake mafisadi wakubwa wa taifa hili wamenunua kesi aliyoiacha BRIAN kibaraka wa mabeberu, na sasa ndugu zetu wenyewe wakina MKONO, MENGI na ROSTAM wanatugawanya kwa maslahi yao wakimtumia mbunge wa KIGOMA KUSINI, DAVID KAFULILA.
Upotoshaji unaofanywa na KAFULILA niwawazi kabisa, niwamakusudi kwa maslahi yake binafsi na ndio maana Katibu Mkuu wa NISHATI ndugu MASWI alisema tena hadharani kuwa KAFULILA na ZITTO wanatumika na wamepewa fedha na MKONO. Sababu nyingine za kutengeneza skendo ya IPTL;
(i) Nikukweli uliowazi hawa wabunge huu nimchezo wao wa siku nyingi kuanda zengwe ambalo mwisho wasiku wanafaidika nalo kwa kupozwa nawahusika, hii nimichezo inachezwa nakamati nyingi za bunge.
(ii) Masakata makubwa kama haya husaidia kuwapa kick wanasiasa tunakumbuka sakata la EPA na RICHMOND. ZITTO na mabilioni ya uswis

Watanzania tusikubali kuwa madaraja yawatu binafsi kujipatia umaarufu wakisiasa na kujiongezea ukwasi walionao.

View attachment 189518""

NASUBIRI HIZO 600 ZILIZOBAKI, KAFULILA NAOMBA UNISHAWISHI NAHIZO NYARAKA 600 KAMA UNAZO KWELI!!! ACHA KUCHEZA NA FIKRA ZA UMMA, HUNACHOCHOTE WEWE ZAIDI YA AJENDA YA SCB-HK.
 
HAKUNA MKAKATI WOWOTE, ACHA KUTAFUTA HURUMA YA WANANCHI WEWE UMEKUWA MPIGARAMLI SIKUHIZI KUZUNGUMZIA MASUALA YA MBELENI???
Kafulila kafilisika hoja, anakuja mbele ya umma kuzungumzia mambo ambayo hakuna wakuyathibitisha kwasasa, unaposema kuna mkakati wa kuzuia ripoti isijadiliwe nini maana yake sasa?? kwanini asisubiri hiyo Novemba ili wote tuone kama ripoti haito jadiriwa?? Unaposema kuwa una nyaraka 600 maana yako nini sasa kama siyo uzushi?? Wenzako walisoma list of shame na wananchi wote tukasimama nao na tukapigana kuueleza umma juu ya EPA na RICHMOND ilikuwa movement kubwa sana. Nawewe lete nyaraka 600 sasa uone kitakacho fuata, acha maneno mengi tugee nyaraka hizo alafu wewe pumzika maana utakuwa umetuuzia sisi wananchi hiyo kesi. Kama huna nyaraka "ufyate" acha kujadiri makapuni ya watu binafsi.

""" utoaji fedha kwenye account ya ESCROW ulifuata utaratibu uliopitia vikao halali katika ngazi mbalimbali. Nakwamba hakuna taratibu zilizopindishwa humo. Halafu nakuuliza swali mkuu " KAMA PAP/IPTL WALIPEWA MITAMBO YA IPTL PAMOJA NAKUBEBA MZIGO WA DENI LA IPTL KUTOKA KWA LIQUIDATOR JE KWANINI IPTL/PAP WASIWE NAHAKI YA KUCHUKUA FEDHA ZA ESCROW ACCOUNT???? lakuzingatia kesi ya ICSD imekwisha na TANESCO na IPTL wamekubaliana juu ya viwango vipya vya capacity charge. JE MLITAKA FEDHA HIZO ZICHUKULIWE NANANI??? lakuzingatia umeme wa IPTL tumetumia bila malipo husika."""""""
 
Kuna juhudi nzito sana za kumziba mdomo Kafulila, kwa maoni yangu nchi hii ilivyoingiliwa na mafisadi ambao hawaogopi lolote lile basi si ajabu wanaweza hata kumuwinda huyu ili wachukue uhai wake.


Kafulila atawindwa na ukweli kwenye mind yake, siku zote as long as anaendelea kusambaza uongo wake basi hawezi kuwa sawa hata kidogo ndio maana leo hata ukikutana na Kafulila waweza jua tu huyu mtu hayupo sawa, kuna mwandishi mmoja niliwahi kukutana nae wakati anatoka kwenye mahojiano na Kafulila serously yule mwandishi alisema Kafulila anatakiwa apate counselling maana hayupo katika stable conscious.
 
Acha upumbavu wewe!!! Angekuwa anasambaza uongo hii Serikali ingechukua hatua ya kufunga bank account ya Rugemarila yenye $65 million kule Netherlands!? Mnaweweseka sana na huu ufisadi mlioufanya.

Dar es Salaam. The government has frozen an account in a bank in The Netherlands that is linked with the $65 million (approximately Sh129 million) that was controversially taken from an escrow account at the Bank of Tanzania and paid to a private entity last year.
The Citizen on Saturday has reliably learnt that a substantial amount of money was transferred from an account at the Catholic Church-owned Mkombozi Bank to the bank in the Netherlands. The Mkombozi account belongs to VIP Engineering and Marketing--the company that owned 30 per cent shares in Independent Power Tanzania Limited (IPTL) until it allegedly sold its shares to Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP) for $65 million.
VIP Engineering and Marketing is owned by James Rugemalila.

Kafulila atawindwa na ukweli kwenye mind yake, siku zote as long as anaendelea kusambaza uongo wake basi hawezi kuwa sawa hata kidogo ndio maana leo hata ukikutana na Kafulila waweza jua tu huyu mtu hayupo sawa, kuna mwandishi mmoja niliwahi kukutana nae wakati anatoka kwenye mahojiano na Kafulila serously yule mwandishi alisema Kafulila anatakiwa apate counselling maana hayupo katika stable conscious.
 
Acha upumbavu wewe!!! Angekuwa anasambaza uongo hii Serikali ingechukua hatua ya kufunga bank account ya Rugemarila yenye $65 million kule Netherlands!? Mnaweweseka sana na huu ufisadi mlioufanya.

Dar es Salaam. The government has frozen an account in a bank in The Netherlands that is linked with the $65 million (approximately Sh129 million) that was controversially taken from an escrow account at the Bank of Tanzania and paid to a private entity last year.
The Citizen on Saturday has reliably learnt that a substantial amount of money was transferred from an account at the Catholic Church-owned Mkombozi Bank to the bank in the Netherlands. The Mkombozi account belongs to VIP Engineering and Marketing--the company that owned 30 per cent shares in Independent Power Tanzania Limited (IPTL) until it allegedly sold its shares to Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP) for $65 million.
VIP Engineering and Marketing is owned by James Rugemalila.


[h=2]Jumatano, 1 Oktoba 2014[/h][h=3]HATIMAYE UKWELI UMEBAINIKA FEDHA ZA ESCROW SIO ZA UMMA[/h]

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu hatimaye imebainika kuwa fedha za escrow si fedha za umma bali malipo halali yaliyokubaliwa kwa mujibu ya sheria kati ya Tanesco,IPTL na BOT(kama wakala wa Escrow)
kama malipo halali yaliyotokana na mauzo ya umeme uliozalishwa na IPTL kwa TANESCO na kuhifadhiwa na BENKI KUU(kama wakala wa Escrow) kutokana na mgogoro baina ya wanahisa wa IPTL yaani Mechmar na VIP,ambapo ilikubaliwa kuwa baada ya kumaliza mgogoro wao malipo hayo yataidhinishwa walipwe,hivyo baada ya PAP kuinunua Mechmar iliyokuwa na hisa 70% na kisha kuinunua VIP iliyokuwa inamiliki 30% ya hisa za IPTL,hivyo PAP kuwa mmiliki wa asilimia mia wa IPTL ambapo alikubali kununua hadi madeni ya IPTL,aliomba kuidhinishiwa malipo yake yaliyokuwa ya mehifadhiwa katika akaunti ya ESCROW maana kisheria alipaswa kulipwa kama mmiliki na kama mkataba wa escrow unavyosema,hapa chini ni baadhi ya screenshot za mikataba ya escrow.
















​

source: Mwandishi Wetu

Posted by HABARI HURU at 6:15 AM Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Shiriki kwenye TwitterShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest




[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: reactions-label-cell, width: 1%"]Reactions: [/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]



[h=4]Maoni 3 :[/h]
  1. b36-rounded.png

    Sandra Hamad1 Oktoba 2014 8:02 AM
    Kwasisi waelevu tulishagundua hii filimbi inayopulizwa na KAFULILA ni ya udongo wa kinyesi. KAFULILA anatumika kwa maslahi ya mafisadi wakubwa wakina MKONO, MENGI na ROSTAM kwa maslahi yao siyo kwa maslahi ya WATANZANIA kama anavyojipambanua. NASISI WANAKIGOMA KUSINI TUNAMSUBIRI HUKU JIMBONI MANNA YEYE SIKATULEKEZA KAAMUA KUWAHUDUMIA WAKINA MKONO, MENGI NA ROSTAMJibu​

    ​
  2. b36-rounded.png

    Kingu Kibudu1 Oktoba 2014 8:12 AM
    KAFULILA UMBWA KABISA HII, INAKAA INATUMIKA KWAKUTUDANGANYA WATANZANIA KWA MASLAHI YA MABEPARI WACHACHE. KWAHIYO YEYE ALITAKA PESA YA ESCROW ALIPWE NANI???Jibu​

    ​
  3. photo.jpg

    Mfalme Selemani1 Oktoba 2014 9:12 AM
    Kafulila katuaibisha sana,nimesoma jinsi alivyokula rushwa mil 90 za kina mengi na rostam ili kuwakomoa wakina muhongo,hafai kuwa kiongozi huyu mtu unless amejisafisha na kurudisha hizo pesaJibu​

    ​

 
Back
Top Bottom