Kafulila: Serikali ya CCM inataka kuniua

Kafulila: Serikali ya CCM inataka kuniua

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Kigoma. Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema endapo itatokea kwa namna yoyote akafa, mhusika mkuu wa kifo chake itakuwa "Serikali ya CCM" na ameagiza kuwa kamwe wasifike kwenye msiba wake wala kutoa rambirambi.

Wakati Kafulila akitoa tuhuma hizo nzito mkoani Kigoma, Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata kampuni ya kimataifa kwa ajili ya kukagua akaunti ya escrow iliyofunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha kusubiri kumalizika kwa mgogoro ulio mahakamani baina ya Shirika la Umeme (Tanesco) na kampuni binafsi ya kufua nishati hiyo ya IPTL.

Kauli ya Kafulila inatokana na mbunge huyo wa tiketi ya NCCR-Mageuzi kudai kutishiwa maisha na Mwanasheria Mkuu Jaji Federick Werema. Jaji Werema anadaiwa kutoa vitisho hivyo baada ya Kafulila kumtaja ndani ya Bunge kama mmoja wa wahusika katika kashfa ya wizi wa Sh200 bilioni kutoka katika akaunti hiyo ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwa nyakati tofauti katika Uwanja wa Mwanga Center na Cine Atlas mjini Kigoma, Kafulila alisema amejitolea maisha yake kupigania rasilimali za taifa ambazo zinachotwa na genge la watu wachache kwa masilahi yao binafsi na kuwaacha Watanzania wengi wakiishi katika lindi la umaskini na huduma mbovu za kijamii.

"Mbunge wenu (Kafulila) nilisema ndani ya Bunge kwamba Sh200 bilioni zimeibwa katika akaunti ya escrow na waliozichota wapo na wanajulikana, lakini Serikali haitaki kuwachukulia hatua. Mbaya zaidi hata Spika wa Bunge (Anne Makinda) amekataa kuunda Kamati teule ya Bunge ili ichunguze kashfa hiyo," alisema Kafulila.

"Matokeo yake nimeanza kutishiwa maisha yangu na Serikali imekaa kimya licha ya kuliwasilisha jambo hilo kwenye vyombo vya dola. Naomba nichukue nafasi hii kutoa tamko kwamba wakati wowote nikifa, mhusika mkuu wa kifo changu ni Serikali ya CCM na kamwe sitaki wafike kwenye mazishi na hata msiba wangu."

Pia, alimlaumu Mkuu wa Polisi (IGP), Ernest Mangu kwa kukalia kimya jambo hilo, akisema amepoteza imani na jeshi hilo kwa vile linaonekana kumuogopa Jaji Werema kwa kushindwa hata kumuhoji.

"Nilipeleka malalamiko yangu kwa IGP, lakini hadi hivi leo (jana) ninapoongea hapa hajawahi hata kuitwa polisi atoe maelezo. Hili ni janga kwa utawala wa kisheria nchini. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa tulitarajia mtu mwenye hadhi ya jaji awe mtii na mtekelezaji wa sheria za nchi, lakini inapofikia jaji kutishia kuniua, hapo ujue mfumo wa sheria ni legelege na hauna nguvu kwa baadhi ya watu."

Wakati wa Bunge la Bajeti, Kafulila alisema fedha hizo zilipitishiwa kwenye benki moja na kuchukuliwa zikiwa taslimu, tofauti na sheria za benki na kuwatuhumu vigogo wa Serikali kuhusika na akiomba Bunge liunde kamati huru kuchunguza tuhuma hizo.

Wakati Bunge hilo likiendelea, Jaji Werema alitumia neno "tumbili" kumhusisha na Kafulila na ndipo mbunge huyo wa Kigoma alipomwita mwizi na kusababisha tafrani ambayo iliepushwa na wabunge wengine waliomzuia Jaji Werema asimkaribie Kafulila.

Inataarifiwa kuwa akaunti hiyo ilikuwa na takriban Dola 250 milioni za Marekani, lakini baada ya kikao cha pamoja kati ya Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), Tanesco na Wizara ya Nishati ilikubaliwa kuwa Dola 122 milioni kati ya hizo zitolewe kutoka akaunti hiyo na kulipwa PAP ambayo ni mmiliki mpya wa IPTL.

Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa tenda kwa kampuni za ukaguzi wa hesabu za kimataifa ili kufanya uchunguzi. "Serikali iache bla bla, itoe tamko kwa fedha hizo zaidi ya Sh400 bilioni. Wanasema siyo fedha za serikali, wakati nyaraka zote hizi nilizonazo zinaonyesha kuwa ni za serikali.

Huu ni ufisadi tu kama ulivyokuwa wa EPA," alisema akirejea kashfa kashfa nyingine ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni iliyokuwa Benki Kuu.

Katika kashfa hiyo, kampuni 22 zilichota fedha kinyume na utaratibu.

"Rais Kikwete aitishe tenda kwa kampuni za ukaguzi wa hesabu za kimataifa ili tujue ukweli. Hizo fedha ni zetu, ni kodi ya wananchi."

Alionyesha kushangazwa na kitendo cha Kampuni ya IPTL kumshtaki Kafulila wakati suala lenyewe bado lilikuwa mikononi mwa Bunge, ambalo limeiagiza Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilichunguze.


Source: Mwananchi
 
Lazima atauawa kwani anataka kuzuia fedha za ESCROW zilizochukuliwa na CCM ili kununulia wapinzani na wapiga kura mwakani. Kama atahurumiwa lazima ang'olewe kucha na meno kama fundisho.
 
Maccm kazi kupanga kuuwa tu.

Ule wenu Kafulila afe.

Mnaleta ya Dr. Ulimboka eh!?
 
Tusifike huku jamani hata tukakataa kuzikana......tujenge hoja kwa nguvu bila kuathiri na kuharibu utamaduni wetu watanzania wa kushirikiana kwenye shida na raha.
 
Gamba walipofikia pabaya. Suluhisho wameona ni kuua tu. Damu ya mwanadamu haiendi bure.
 
Pole sana Kafulila najua unajisikia vibaya Werema aliteleza tu msamehe tu.
 
lazima atauawa kwani anataka kuzuia fedha za escrow zilizochukuliwa na ccm ili kununulia wapinzani na wapiga kura mwakani. Kama atahurumiwa lazima ang'olewe kucha na meno kama fundisho.

teh teh teh werema ni mwanasheria wa serikali na hawezi kuhangaika na dagaa ila ni msemo maarufu wakati wa session za murder kesi kwa mwanasheria wa serikali kuomba shingo ya mtu aliyepatikana na hatia ya mauaji
 
teh teh teh werema ni mwanasheria wa serikali na hawezi kuhangaika na dagaa ila ni msemo maarufu wakati wa session za murder kesi kwa mwanasheria wa serikali kuomba shingo ya mtu aliyepatikana na hatia ya mauaji

Unamaanisha nini unaposema hawezi kuangaika na dagaa? Haya mambo yenu mnaendeleza endekeza hayafai
 
Mbunge Kafulila ameituhumu serkali ya CCM kuwa inataka kumuua na akifa wasihudhurie mazishi na msiba wake.
Source : Mwananchi gazeti la leo

Kwanza akajibu case yake..Serekali toka lini ikataka kuuwa unknown person..Huyu elimu ya darasa 7 anataka umarufu
 
Mbunge Kafulila ameituhumu serkali ya CCM kuwa inataka kumuua na akifa wasihudhurie mazishi na msiba wake.
Source : Mwananchi gazeti la leo

Huyu anachekesha, Hawakuhudguria wa Balali utakuwa wake? amelikoroga wacha alinywe!!
 
Siasa bana sasa kafulila wakuuwe kwa nini..we si wanakupiga mtama tu unaanguka
 
Kwanza akajibu case yake..Serekali toka lini ikataka kuuwa unknown person..Huyu elimu ya darasa 7 anataka umarufu

Kesi ya CCM kuchota mabilioni ya pesa ya Iptl kupitia escrow account kwa ajili ya kununua wapiga kura na kuiba kura au kesi gani?
 
siasa bana sasa kafulila wakuuwe kwa nini..we si wanakupiga mtama tu unaanguka

hahhhhaaaaaaaaa naona ile makala ya meena katika mwananchi kuhusu gate of heaven inazidi kumuwewesesha anaogopa kufunguliwa mageti ya mbinguni umesema kweli mitama tu inamtosha
 
teh teh teh werema ni mwanasheria wa serikali na hawezi kuhangaika na dagaa ila ni msemo maarufu wakati wa session za murder kesi kwa mwanasheria wa serikali kuomba shingo ya mtu aliyepatikana na hatia ya mauaji
Sijakuelewa mkuu unaposema Kafulila ni mtu mdogo wakati amechaguliwa na maelefu ya wananchi na kumbwaga mgombea wa chama tawala pia ukilinganisha na Werema aliechaguliwa na mtu mmoja tu !!!Kuwa na cheo si ukubwa , ukubwa ni namna mtu alivyoingia madarakani, wakati wowote Rais anaweza kutengua uteuzi wa Werema kitu ambacho hakiwezekani kwa Kafulila.
 
Back
Top Bottom