Kafulila kuendelea kuwa mbunge: kuna mchezo mchafu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila kuendelea kuwa mbunge: kuna mchezo mchafu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maskini Mkulima, Dec 29, 2011.

 1. M

  Maskini Mkulima Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepata shida kidogo kuhusiana na suala la Kafulila lilivyoendeshwa na lilipofikia. Napata wasiwasi kwamba kuna mchezo mchafu na pengine Zitto anahusika na mchezo huo ndo maana akawa wa kwanza kutueleza humu kwamba Kafulila anaendelea kuwa mbunge. Wanasheria wajitokeze watuweke sawa kwa sababu hata maelezo ya Dr. Mvungi sijayaelewa pengine kwa sababu sikuhudhuria press conference yake nimekuwa nikipata vipiece vipiece tu vya alichokisema. Nijuavyo mimi uamuzi wa NEC ya NCCR unaheshimiwa mpaka hapo mahakama itakapoutengua kwenye kesi ya msingi iliyofunguliwa na Kafulila na kwa kuwa uamuzi huo unaamanisha kwamba hana chama tena anachokiwakilisha kwa sasa (kwa mujibu wa katiba mbovu tunayoitumia kwa sasa), then na ubunge anasimama. Isipokuwa court injuction sasa inazuia taratibu nyingine kuendelea kuanzia hapo ilipotoka, kwa maana kwamba Tume ya Uchaguzi haitatangaza uchaguzi mdogo mpaka kesi ya msingi iamriwe. Na ndicho kilichotokea kwa akina Erasto Tumbo na Danny Makanga walipofungua kesi mwaka 2001 kupinga kufukuzwa uanachama wa UDP. Na ndicho pia kilichotokea kwa madiwani wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho. Hapakufanyika uchaguzi wala waziri hakuitaarifu tume ya uchaguzi kwamba nafasi zao ziko wazi ila waliendelea kuwa pembeni ya udiwani na ndo maana waziri alipotaka kuchakachua ili waendelee kuwa madiwani umma ulimwakia sana. Sasa hii ya Kafulila inakuwaje aendelee kuwa mbunge? Zitto na wenzako jitokezeni mtuambie kama mlimhonga Jaji ama ni nini mmefanya.

  S
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mimi ndo nilivoelewa. ngoja tusubiri tuone.
   
 3. a

  abam Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  serikali haina hera za uchaguzi nani atagharamia
   
 4. G

  Godfrey GODI Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ktk sakata hili huwezi kuwatoa Rais kikwete na zitto. Zitto anatumiwa na kikwete kutaka kuigawa chadema. Kama jaribio la kumpindua mbatia lingefanikiwa, zitto na genge lake wangehamia nccr na zitto kuwa mwenyekiti. Chadema na nccr vingekuwa vyama hasimu na kukiacha ccm kuendelea kutawala. Rejeeni kauli ya mh. Machali kuhusu zitto. Baada ya zoez hilo kukwama na kafulila kupoteza uanachama na hivyo ubunge, waliomtuma lazima wamsaidie. Jaji kapewa maelekezo na rais. Kesi danadana hadi 2015. Zitto si mtu wa kuaminika ktk siasa.
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  jamaa eti wamembatiza wanamwita "Mbunge wa mahakama"
   
 6. H

  Hume JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Ndo kusema kutokuaminika kwa Zitto kutokane na hisia zako hizi?
   
 7. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mnaleta porojo kwenye masuala mazito na ya msingi.Mtoa hoja ana hoja bado haijajibiwa hata mie naunga naye maana Dr.Mvungi jana ametumia nguvu na misuli kuwasema wana habari na kuwasuta badala ya kuwaelewesha na kuwaelimisha watanzania na wananchi hasa wa jimbo la kigoma kusini.
   
 8. G

  Godfrey GODI Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu sitaki ukubaliane haraka na nilichoandika lakini nakushauri fanya utafiti. Kabla kulikuwa na mazungumzo ya kafulila na machali, akimwelezea malengo yao na zitto. Kwa kutokubaliana machali akavujisha mazungumzo hayo bila kuuma maneno. Posts nyingi zilieleza hii njama humu jf. Anyway kwa kuwa hujui maendeleo ya IT, sikushangai. Sisi wengine ni hackers wa mawasiliano.
   
 9. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Ulikuwepo hapo Rais alipompa maelekezo Jaji? Au tena kwa vile umejipa ujiko wa kuwa ni hacker maarufu wa mawasiliano ndiyo unataka tukuamini?
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mkuu tuache hisia,Kafulila naye ana haki zake kwa namna moja au nyingine hakutendewa haki.Mbatia si mpinzani hata kidogo.Mbunge Moses Machali amejidhalilisha sana katika hili.
   
 11. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Vijana munakazi,ZItto alishapinga tuhuma za machalli,pia km zitto kamsaidia kafulila arudi kwenye ubunge wake ni safi sana,kwan amemuokoa kijana mwenzake.Tuache majungu
   
 12. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii inshu sioni Zitto anahusishwa vipi, au ndio tunakurupuka tu tukusikia rumors kwa watu basi tunazibeba?
   
 13. C

  Concrete JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  @Ni suala lililo wazi kuwa Zitto anahusika kwa sana katika mgogoro wa NCCR, kama unafuatilia mchezo mzima Ulipoanzia mpaka sasa ulipofikia hakika hili utaliona tu,na kama ukishindwa kuliona sasa,jipe muda maana litaendelea kuwa wazi zaidi. @Kwa issue ya hukumu ya mahakama wengi wetu inatupa utata tu,Nategemea kuna mdau wa JF atatuwekea nakala ya hukumu hapa ili tuweze kuisoma wenyewe,Lakini pia wanasheria(Neutral) tunasubiri ushambuzi wao,nafikiri kila kitu kitakuwa wazi tu muda si mrefu ujao.
   
 14. G

  Godfrey GODI Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SITAKI UNIAMINI, ila fuatilia ninachokiandia. Unganisha matukio ya jambo hili. Hii ni njia rahisi kwako maana umeonyesha njia zingine za ufuatiliaji huziwez. Kama hutaweza kwa njia basi utakuwa umejitia upofu ktk ufuatiliaji. Kwa mtu mwenye kufikiri suala hili la zitto kutumika na kisha kumtumia kafulila liko wazi sana. Nawa uso utaliona vizuri.
   
 15. G

  Godfrey GODI Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unategemea zitto angezikubali tuhuma hizo? Kwa hili ilikuwa ni lazima apinge. Ni kazi kwako kujua kama ni kweli au anasingiziwa. Kama mfuatiliaji wa mchezo, utajua nani mkweli. Ishu za epa na nyingine zote zilianza kama walivyoita wakati huo MAJUNGU. kama na wewe unalitumia neno hili bila kuchunguza basi utakuwa unachora graph kwa kutumia point moja.
   
Loading...