Kafulila atishia: Nikishindwa kesi nitahamia chama kingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila atishia: Nikishindwa kesi nitahamia chama kingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, May 11, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, amesema yuko tayari kukihama chama chake na kujiunga na chama kingine ikiwa atashindwa kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama aliyoifungua mahakamani.

  Kafulila aliyasema hayo wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya na kuwa ana uhakika wa kushinda kiti cha ubunge kwenye jimbo lake hata kama atagombea kupitia chama kingine, hivyo uamuzi wa kutimuliwa NCCR Mageuzi hamuumizi kichwa.

  Alisema kuwa endapo mahakama itaamua kubariki uamuzi wa yeye kufukuzwa NCCR Mageuzi, hana mpango wa kukata rufaa katika Mahakama ya juu, badala yake atahamia chama kingine na kurudi jimboni kuomba ridhaa ya wananchi aendelee kuwa mbunge wao.

  Hata hivyo Kafulila hakuwa tayari kutaja chama anachokusudia kuhamia, akisema kuwa hilo atalisema baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kesi aliyoifungua mahakamani.

  “Nimesema nitahamia chama chochote, tusubiri uamuzi wa mahakama kama utaniondoa NCCR Mageuzi ndipo nitakuwa tayari kutamka chama gani najiunga nacho,” alisema Kafulila. Kafulila alijiunga na NCCR Mageuzi mwaka 2010 akitokea Chadema.

  Hata hivyo mwaka jana alihitlafiana na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia hali iliyosababishwa avuliwe uanachama kabla ya kukimbilia mahakamani.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ccm hatumtaki hata kidogo
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  na laana ya CHADEMA itamwandama mpaka pale atakapoamua kuacha siasa
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kuwepo NCCR ni sawa na upo CCM
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  jamaa hawezi kuhamia ccm maana kule mbatia tayari yupo so hana ujanja bali kuingia cdm.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  Chadema watampokea mwana wao mpotevu
   
 7. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  atashnda akiwa na chama chochote!!? Ahamie ccm aone....
   
 8. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ili chama kisipoteze ruzuku ndio maana Mh. Mbatia kateuliwa, sasa ajiandae kutafuta chama tu, nadhani mahakama zetu kama kawa zitakuwa na maelekezo o juuuuuuuuuu
   
 9. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Akishindwa kesi automatically atakuwa siyo mwanachama wa NCCR, sasa anatishia nini.
  Labda angesema hata akishinda kesi atahamia chama kingine hapo inge make sense.
   
 10. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aombe msamaha na arudi kundini
   
 11. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Anatishia sababu ana gerantii ya jimbo lake, hata akihamia ADC atachaguliwa
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Utofauti wa NCCR na CCM kwamba CCM ni Mafisadi, lakini ni chama kimoja viongozi tofauti
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Wewe una wadhifa gani kukisemea chama? Au ndiyo vile kuwa CCM imekosa mwelekeo kila mtu anaropoka kivyake?
   
 14. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  atahamia ADC akiwa kama katibu mwenezi kwa rafiki yake Hamad Rashid
   
 15. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 308
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  We swahiba wa Zito, Hakuna binadamu asiye na kasoro. Nakushauri muombe msamaha rais we2 mtarajiwa Dr. Slaa, kisha rudi kundini CDM. Hilo jimbo lako utalipata, vinginevyo sahau ndoto ya ubunge.
   
 16. E

  Eddie JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa alimwita "Sisimizi" umesahau?
   
 17. L

  LEYANA LESINDAMU Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka nilishaleta uzi hapa jamvini nikamshauri aombe msamaha arudi kundin hata kama ni kupoteza ubunge lkn nyota yake ya kisiasa izidi kung'ara. Akikataa ni ubishi wake,atakua kama Shitambala wa mbeya!
   
 18. s

  sawabho JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Alitakiwa kusema akishindwa kesi, atajiunga na chama kingine na sio kwamba atahamia chama kingine. Maana kama akishindwa kesi, hatakuwa mwanachama wa chama chochote mpaka hapo atakapoomba uanachama na kuruhisiwa kuingia chama husika ikiwa ni pamaoja na NCCR-Mageuzi !!!!
   
 19. k

  kumdyanko Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kigoma wana mashine 2 mbili zitto kabwe na kafulila kichwa hicho hakiwezi kutoweka walamawese hawabahatishi.huoni NCCR imejikita zaidi kigoma? ni baada ya mafisadi kuteua wagombea ambao ni mafisadi then wananchi wakaamua kuweka wanafunzi. Wala mawese na Migebuka ni balaa hawadanganyiki.ila tunasikia kuna mbunge mwenzake wa kigoma hukohuko anamwandama sana na ndo wako karibu sana na mbatia siajabu na yeye ccm.
   
 20. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Akikataliwa CCM B ni dhahili CCM watamkataa
   
Loading...