Jile79
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 17,668
- 13,237
Kuhusu kutafuta hifadhi kwa viongozi wa upinzani katika mataifa yanayoheshimu uhuru na haki ya kuishi.
Na Mwl, John Pambalu
Mwaka 2015 baada ya uchaguzi uliompa ushindi Mhe. Magufuli. Aliyekuwa Mkt wa Chadema mkoa wa Geita na mgombea ubunge Jimbo la Busanda marehemu Alphonce Mawazo. Alipokea taarifa za vitisho juu ya uhai wake, hakuamua kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini, siku chache baadaye aliuawa kikatili mchana kweupe mita chache kutoka kituo cha polisi huku jimboni Busanda mkoani Geita.
Kiongozi mwingine wa Chadema na mkosoaji wa serikali ya awamu ya tano Ben Saanane alipokea taarifa za kutishia uhai wake. Hakuona sababu za kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini. Siku chache baadaye alipotea na mpaka leo hakuna anayejua yuko wapi Ben Saanane.
Mwaka 2017 Mhe. Tundu Lissu alipokea vitisho juu ya uhai wake. Yeye alijaliwa kujua mpaka namba za gari za waliokuwa wakimfatilia. Lissu hakuona umuhimu wa kutafuta hifadhi. Siku chache baadaye alishambuliwa kwa risasi za moto kwenye nyumba za serikali zenye ulinzi full-time. Mpaka leo hata hao wanaodai nchi iko swali hawajawahi kusema ni wakina nani walimshambulia Lissu.
Nataka kusema nini?.
Wapinzani wanaotishiwa uhai wao kuamua kuondoka nchini kutafuta hifadhi ni hekima ya kimungu. Yusuph alimkimbiza Bethlehem mtoto Yesu kukwepa tishio la kupoteza uhai wa mtoto Yesu baada ya mfalme Herode kutangaza watoto wote wa kiume wauawe.
Mhe. Lissu na Lema ambao wameondoka nchini kutafuta hifadhi nje ya nchini wanastahili pongezi hata Yesu alipelekwa uhamishoni ili abaki salama.
Wasalaam
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa