Huyu Mwenyekiti wa UVCCM mbona kama vijana wamepigwa?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Huyu Mwenyekiti wa UVCCM NI kweli alijenga hoja akachaguliwa na wapiga Kura au alipitoshwa? Nimemsikiliza anazungumza jukwaani Dodoma, nikamsikiliza anaanza kusema anataka amfundishe Dr. Slaa kujenga hoja, najiuliza MTU anayetembea ameandika vitu vyakusema kwenye hotuba yake anaweza mfundisha Dr. Kujenga hoja?

Kuhusu bodaboda, anasema bodaboda oyee! Hajui kwamba nchi haina tena bodaboda ina maafisa usafirishaji? Kama wenye kazi Tu wameikataa yeye anawezaje kuwalazimishawaitwe boda boda?

Tunapochagua viongozi ndani ya CCM tuchague watu wenye sifa itasaidia Sana kuimarisha mapambano ya hoja. Tukiendelea kuchagua kutoka kwenye system na familia za wanasiasa tutaishia kila siku kudandia hoja.

Lema amewatoa wote kwenye reli na Arusha aliwambia amekuja kuwavuruga. Msikibali kuvurugwa jiandaeni au tafteni watu wenye akili wawasaidie, fanyeni utafiti.

Haiwezekani mseme lema Hana hoja wakati huo huo mwaruhusu bodaboda wa chama cha mapinduzi wabadili jina nakuitwa maafisa wasafirishaji. Natumai waliosoma NIT wote sasa Watakuwa waendesha pikipiki au vinginevyo wabadili tittle zao.
 
Back
Top Bottom