Uchaguzi 2020 Kwa wapiga kura sasa ni wakati wa kutafakari zaidi

Oct 6, 2020
27
50
Na Thadei Ole Mushi

1.Ni kawaida ya wanasiasa, Maadui wao wanataka wawe maadui wetu sote. Hili ndio kosa kubwa la wanasiasa, Kote Duniani.

2.Kosa lingine kubwa ninaloliona hapa ni selection ya nani akusemee nini au Nani akuombee Kura. Shekhe Ponda yeye Binafsi ana tatizo na Waumini wenzake kwa maana ya kwamba movement zake hazikubaliki na Waumini wenzake.

3. Wote wawili Wana tatizo Moja, hawaamini Kama suluhu ya mgogoro wowote unaweza kumalizwa Mezani bila mtu kuumia. Wanaamini Sana katika jino kwa jino, siamini Kama wataruhusu Familia zao kuwa front line kwenye mapambano au wanategemea mtoto wa pale Mburahati anayepambana na maisha yake awe ndiye kafara ya kutafuta maisha Bora ya familia zao.

4. Agenda yao kubwa kabla ya kuwaletea maendeleo wananchi Ni kulipa Kisasi. Yaani kabla ya kuanza kuleta maendeleo watawashikisha adabu kwanza wabaya wao.

5. Najaribu kuwaza kuhusu Serikali itakayoundwa na position za watu ndani ya Serikali mpya. Hakuna mahali ambapo Lisu ataunda Serikali aache kuwatunuku wafuatao uwaziri (Askofu Mwamakula, Shekhe Ponda, jongwe, Lema, Mbowe na wengineo) Hawa tutawakabidhi majeshi yetu, vifaru vyetu fedha zetu, bunduki zetu, na kila kitu. Itakuwa Serikali ya aina yake Duniani kwa kuwatendea watu wake mema na itakuwa inaongoza kwa uadilifu mkubwa Duniani. Kwenye uadilifu na wema usitoe neno na Kuongeza neno Kama asemavyo Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza. Maana yangu ibakie hivyo hivyo.

6. Ukiniuliza Leo kitu cha kwanza kinachomtesa Rais Magufuli Ni Nini nitakuambia ni Rasilimali za Taifa hili. Usimshangae Ponda kutaka Magufuli aondoke Madarakani, mshangae Zaidi Robert Amsterdam kwa kuwapenda watanzania kuliko JPM. Achana na madini anayoyalinda sasa JPM aliwahi kulinda pia Samaki wetu wasivuliwe hovyo na akakamata meli wanafunzi wakaoga Samaki. Pamoja na figisu zote leo hii hakuna mtu mwenye uthubutu wa kuvua eneo la bahari ya Tanzania hivyo hakuanza leo kuzilinda rasilimali hizi.

7. Tofauti kubwa ya Lisu na JPM na ambayo haionekani na watu wote Ni katika Imani yao juu ya Taifa hili. JPM anaamini kwa rasilimali zetu tukijibana tutatoboa na tutayafikia mataifa makubwa kiuchumi. Lisu yeye anaamini kuwa bila mkono wa Beberu kutoka kwa urahisi Ni ndoto. Zote hizi ni Imani na ndipo wanapotofautiana tu.

8. JPM na Lisu sio malaika, Hawa wamezaliwa na binadamu kama Mimi na wewe hivyo katika ubinadamu wao hawakosi mapungufu yao. Mchezaji aliyepo Benchi anaweza kuona makosa zaidi ya mchezaji mwenzake aliyepo kwenye mchezo, Ni Kama wadau wenzangu wa draft ukilicheza ukiwa nje unashinda Mara Moja tofauti na ukiwa ndani. Mtu anayejaribu kufanya Mambo mengi ni rahisi kukosea mengi kuliko yule ambaye hafanyi au hakuwahi kufanya hii sio Falsafa na siamini Kama utashindwa kuelewa.

9. Kuna maisha baada ya Uchaguzi, uchaguzi usikuachie Kilema, uchaguzi usikuachie matatizo makubwa, baada ya uchaguzi huu bado wagombea wote watakuwa na maisha Bora kuliko sisi. Tuwekeze zaidi kwenye mipango ya kutoboa kimaisha kuliko kwenye Siasa. Baada ya Tarehe 28 Kuna watakaokuwa Wana Sonya na wengine wakikenua meno. Tatizo zaidi ni kwa yule atakayepata matatizo makubwa kisa Siasa.

10. Vita ikitokea niwaambie watoto wa wagombea wote watakuwa wa mwisho kufa. Sisi wenye viherehere tutakuwa wa kwanza.... Ben Ali alitoroka na familia pale Tunisia, Nani alimuona mtoto wa Mugabe Barabarani kipindi Cha maandamano, watoto wa Mubaraki wao walishtakiwa kishua huko nje, Wa Gadafi ilikuwaje? Kule Syria Kuna mtoto yeyote wa kiongozi ambaye ulisikia kafa? Hizi Ni hesabu rahisi Kama za kukopa maduhulu alizozifanya Polepole. Tusitoe Mifano mingiiiii mpaka Sasa tumeshapoteza ndugu zetu kadhaa kisa uchaguzi, umesikia ni mtoto wa kiongozi gani? Watoto wa Viongozi wapo kwenye viyoyozi na Wala hawajui nn kinaendelea.

Ngoja niwaache!! Tuendelee kuomba kura na kusubiri Comment za Graduate upime na aina ya Elimu waliyonayo. Logic imekuwa ni Tatizo Lao number moja. Utamjua tu hatoweza kujadili atatukana. Tusubiri sote.Daktari anapomdadisi mgonjwa kwa kumshika hugundua palipo na Tatizo haraka kwa mgonjwa kutoa mlio anaposhika eneo husika.

Nasubiria milio hapa kugundua mwenye tatizo na lipo wapi tatizo husika.

Ole Mushi
0712702602
 
Back
Top Bottom