Kadinali Giovanni Angelo Becciu atumbuliwa kwa ufisadi na kufutiwa haki zote zinazotokana na nafasi hiyo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Kadinali wa ngazi ya juu Vatican, Giovanni Angelo Becciu amejiuzuru ghafla bila kutarajiwa lakini imebainika kuwa aliambiwa na Papa Francis kufanya hivyo.

Kadinali huyo alishukiwa kutoa fedha ya kanisa na kuwapa ndugu zake ingawa amekanusha kufanya kosa hilo. Cardinal Becciu alikuwa mshauri wa karibu wa papa na awali katibu wa Vatican.

Alihusika na mkataba ambao una utata wa kuwekeza katika kujenga jengo la kifahari mjini London kwa kutumia fedha za Kanisa.

Uwekezaji huo ulikuepo tangu waanze kumfanyia uchunguzi wa matumizi ya fedha.

Mtu kujiuzuru katika ngazi ya Ukadinali ni jambo la nadra sana kutokea, taarifa kutoka ofisi ya baba mtakatifu zinasema.

"Baba Ntakatifu amekubali maombi ya kujiuzulu yaliyowasilishwa na mwadhama kadinali Giovanni Angelo Becciu."

Lakini Kadinali huyo mwenye umri wa miaka 72, aliuambia mtandao wa Domani nchini Italia kuwa alilazimishwa kujiuzulu kwa sababu alishukiwa kutoa fedha za Kanisa kwa kaka zake.

"Sijaiba hata Euro moja. Sijafanyiwa uchunguzi lakini wakinipeleka Mahakamani , nitajitetea mwenyewe kuwa sijaiba," Kadinali huyo alinukuliwa akisema hivyo.

Alizungumza baadae na vyombo vingine vya habari , Kadinali huyo alisema kuondolewa kwake kumekuja kwa kushtukiza. Alisema, Papa alikuwa na wakati mgumu sana kutoa taarifa hizo.

Kadinali Becciu ni nani?

Giovanni Angelo Becciu, ni raia wa Italia ambaye amekuwa akitumikia ofisi ya huduma ya diplomasia ya Vatican.

Kuanzia mwaka 2011 mpaka 2018, kadinali Becciu alikuwa katibu mkuu wa Vatcan, wakati alipopewa jukumu la kumsaidia papa na shughuli zake za kila siku.

Giovanni Angelo Becciu alipata ukadinali Juni, 2018

Ni papa Francis ndiye aliyempa ukadinali huo mwaka 2018, wakati alipochukua jukumu jipya la kusimamia idara inayoangazia maisha ya utakatifu.

"Ni mshtuko mkubwa kwangu na familia yangu na watu wa nchi yangu. Ninakubali kutii kutokana na upendo wangu wa kanisa na Papa," vyombo vya habari vya Italia vimemnukuu Ijumaa.


images (10).jpg
images (9).jpg
images (6).jpg
images (8).jpg
images (4).jpg
 
Wangekuja huku kwetu waone maaskofu na mapadre wanavyotumia ipasavyo hela za kanisa kwa mambo yao binafsi Tena yenye ukakasi mno ikiwemo kuwajengea wanawake wanaotembea noa nyumba za kifahari.
 
Back
Top Bottom