Kada zote ni sawa, tusiwakuze Madaktari hiyo ndiyo kazi yao

Andie

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
713
1,641
Kutokana na janga hili ni wazi madaktari na wauguzi wamekua wakijitoa kweli kweli, pongezi kwao.

Lakini napenda kukumbusha kua wanachofanya ni wajibu wao, hawajatupendelea kututibu. Kumekua na wimbi la watu kuwatukuza madaktari huku wengine hata wakidiriki kupendekeza eti mishahara ya kada zingine ipunguzwe waongezewe madaktari.

Hivi vita ikitokea mbona wanajeshi sio kujitolea tu kufanya kazi kama madaktari wao hujitolea uhai wao kabisa kwaajili ya watu wengine na hua wanapongezwa ila "hawaabudiwi" kama kinachotokea kwa madaktari.

Wakulima ndio WANATULISHA bila wao ni kufa kwa njaa ila hua tunawathamini kwa mchango wao ila "hatuwaabudu" kama kinachofanywa kwa madaktari.

Iwe wazi madaktari wanafanya kazi nzuri wanahitaji pongezi kama kada nyingine ila sio kusujudiwa. Wanachofanya ni wajibu wao. KILA MTU ANA UMUHIMU SAWA.
 
Kinachonichekesha haswa ni baadhi ya wale wanaojiita "Wajasiriamali" na "waliojiajiri" wanawatukanaga mno madktari na watu walioenda chuo kuwa wanapoteza Muda bora waiingie kwenye "ujasiriamali".

Sasa hivi wote wamejificha ndani kwao wanategemea Madaktari Waje na tiba. Dunia ni kutegemeana.
 
Kama kuna vitu zaidi ya kimoja ulinganifu haupo, tukubali tu daktari na Engineers wanagusa maish ya watu directly.
Moja ameweka ubunifu duniani na kuwa rahisi ktk maisha yetu na mwingine anakarabati miili yetu.
Hizo ndo kozi muhimu hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
Engineers wa bongo??
Wakati hata mashine za Sanitizers zenye sensor wameshindwa kubuni.
Mpaka kijana kutoka SIDO ndio amevumbua.
Hatuna Ma Engineer ila tuna ma Formen ( wasimamizi wa Vibarua!!!)
 
Huyo mkulima anatumia zana gani, chuma inatengeneza na mkulima au madawa, kila kilicho tengenezwa hapa duniani kimetengenezwa na Engineer
Duuuh kizazi cha 2000 mnasikitisha sana, yani mkuu engineer ni muhimu kuliko mkulima ? Kumbe kua na nyumba ni muhimu kuliko kula ?! Nawaona wanasai makiishi kwa kuhama bila kua na nyumba, niambie mtu anaeishi bila kula ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kufananisha madaktari na fani yoyote ile duniani ndio maana duniani kote ndio wanaongoza kwa kulipwa hela ndefu.

Huyu ana deal na afya ya mwili wako,ana deal na delicate organs za mwili wako,bado anafanya kazi katika mazingira ya hatari kila siku kwani kila siku ana chezea damu ambayo imebeba maambukizi ya magonjwa kibao (mf HIV,Homa ya ini) na kwenye magonjwa ya mlipuko ndio kabisa anachungulia kifo mfano ebola ,Chorela ,Covid-19 yeye kila siku anakuwa exposed kwenye mazingira hayo.Yaani sometimes nahisi hata wanacholipwa bado hakitoshi.

The highest-paying jobs in the world

25 Highest Paid Occupations in the U.S. for 2019

The 20 Highest-Paying Jobs in the World

Top 50 Highest Paying Jobs or Careers in the World - WiseStep
 
Kutokana na janga hili ni wazi madaktari na wauguzi wamekua wakijitoa kweli kweli, pongezi kwao.

Lakini napenda kukumbusha kua wanachofanya ni wajibu wao, hawajatupendelea kututibu. Kumekua na wimbi la watu kuwatukuza madaktari huku wengine hata wakidiriki kupendekeza eti mishahara ya kada zingine ipunguzwe waongezewe madaktari.

Hivi vita ikitokea mbona wanajeshi sio kujitolea tu kufanya kazi kama madaktari wao hujitolea uhai wao kabisa kwaajili ya watu wengine na hua wanapongezwa ila "hawaabudiwi" kama kinachotokea kwa madaktari.

Wakulima ndio WANATULISHA bila wao ni kufa kwa njaa ila hua tunawathamini kwa mchango wao ila "hatuwaabudu" kama kinachofanywa kwa madaktari.

Iwe wazi madaktari wanafanya kazi nzuri wanahitaji pongezi kama kada nyingine ila sio kusujudiwa. Wanachofanya ni wajibu wao. KILA MTU ANA UMUHIMU SAWA.

Mkuu wakati unaandika huu Uzi ulikua unatumia TAKO kufikilia nini??
 
Vp kuhusu walimu waliowafundisha hao maengineers na madokta uchwara?
Madaktari ni muhimu sana ila sio Tanzania wala Africa,
Africa ni sehemu pekee Duniani, utakuta Daktari hana uwezo wa kugundua au kufanya tafiti juu ya dawa zitakazomtibu mwafrika,pia utamkuta engineer ambaye hawezi hata kutengeneza banda la kuku.

Africa hakuna kada muhimu kuliko ingine, wote tunasubiri muziki upigwe ulaya sisi tucheze.
Tuna kada mama ya elimu ambayo nayo imebebeshwa zigo zito la mitaala ya kizungu.
Kama kuna vitu zaidi ya kimoja ulinganifu haupo, tukubali tu daktari na Engineers wanagusa maish ya watu directly.
Moja ameweka ubunifu duniani na kuwa rahisi ktk maisha yetu na mwingine anakarabati miili yetu.
Hizo ndo kozi muhimu hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna vitu zaidi ya kimoja ulinganifu haupo, tukubali tu daktari na Engineers wanagusa maish ya watu directly.
Moja ameweka ubunifu duniani na kuwa rahisi ktk maisha yetu na mwingine anakarabati miili yetu.
Hizo ndo kozi muhimu hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi kuhusu anayempatia marifa huyo daktari na enginer?
 
CONCLUSION : Kila kada ni muhimu kutegemea na mazingira husika, Na kila kada inategemea kada nyingine Katika kuongeza ufanisi wake
" No single size fits all"
 
Elimu na ualimu kwa ujumla wake ndio chanzo cha maarifa yote duniani. Akili ya binadamu inatabia ya kuzalisha maarifa hasa tunapokabiliana makuzi yetu. Na hakuna daktari mwenye grantee ya mgonjwa kupona hata mafua ,daktari hutibu tu kupona ni kazi yake Mungu.
 
Back
Top Bottom