Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
Kabla sijaenda mbali katika uandishi wa bandiko hili,naomba niweke wazi kuwa mimi sio daktari wala nesi bali nina fani tofauti kabisa ila nimesukumwa na ukweli ulio wazi juu ya ugumu na hatari iliopo katika kutumikia kada hizi mbili hasa ya udaktari.
Tukirudi kwenye mada,hali ya ugonjwa huu wa corona huko Marekani na Ulaya kwa sasa na hatari inayowakabili watumishi wa sekta ya afya katika mataifa hayo na mengine duniani ni ushahidi tosha kuwa kada hizi mbili ni kada muhimu na nyeti sana katika huu ulimwengu kuliko kada zingine zote.
Japo ni kweli karibu kila kada/kazi ina risk zake,lakini sidhani kama kuna kada ina high risk kama hizi kada mbili na hasa yanapotokea majanga ya maradhi ya mlipuko kama ilivyo corona kwa sasa.
Kwa mfano, wakati hivi sasa watu tunaogopa hata kusogeleana huku tukiwa hatuna hata uhakika kuwa mwenzangu huyu ana virusi,madaktari na manesi na wafanyakazi wengine katika kada hii wao hawana option zaidi ya kulazimika kuwahudumia wagonjwa licha ya hatari kubwa waliyonayo.
Yaani kwa kifupi, it is matter of death or life.
Mbali na pandemic kama hii ya corona,hata wanapohudumia wagonjwa wa magonjwa mengine,kama vile kuwafanyia upasuajj wagonjwa au kina mama wajawazito wenye magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile HIV, n.k. bado wanakuwa kwenye risk kubwa tu ya wao kuambukizwa magonjwa haya hivyo hizi kada ni kada zinazofanya kazi katika mazingira ya hatari karibu kila siku katika utumishi wao.
Naelewa katika mafunzo yao wanafundishwa namna zote za kujikinga na maradhi au hatari inayoweza kuwakabili katika utendaji wao wa kazi,ila bado hawa ni binadamu wanaoweza kufanya makosa kama wafanyavyo watu wengine waliko katika fani na kada tofauti ila tofauti hapa ni kuwa wao makosa yao ynaweza kugharimu maisha yao mbali na ya mgonjwa,
Kwa mfano, hivi sasa teyari kuna madaktari kadhaa wameripotiwa kufa kutokana na kuwahudumia wagonjwa wa corona huku ulaya na bila shaka bado wataendelea kufa kama ilivyokuwa kwenye ebola na magonjwa mengine.
Kuna watu wanaweza kusema kada ya ualimu ndio muhimu na inayostahili kulipwa vizuri kuliko hata kada ya udaktari kwasababu bila mwalimu huwezi kupata daktari, lakini wanasahau uhai wa mtu ukipotea, hakuna namna unaweza kuurejesha na hakuna asiegopa kifo hata kwa wanajeshi waliko vitani.
Naelewa kazi ya jeshi ni ngumu na ya hatari lakini ni heri mwanajeshi anaepambana na adui anaeonekana kwa macho kuliko nesi au daktari anaepambana au ku-deal na adui asionekane kwa macho kama huyu COVID-19 na wengine wengi.
.
Hivyo,natoa wito kwa serikali kutazama upya maslahi ya kada hizi kama walivyofanya kwa watumishi wa TRA enzi za utawala wa Mkapa lakini nawataka na hawa madaktari na manesi nao wawe na utu na pia wajali na kuthamini wagonjwa.
Hata kama wanalipwa risk allowance, mishahara ya tofauti ni muhimu sana kwa hizi kada na msisahau shule ya udaktari ni pasua kichwa.
Pichani ni dakatri wa kichina aliejulikana kwa jina la Doctor Lie Wenliang alietoa tahadhari kwa mara ya kwanza juu ya uwepo wa ugonjwa wa korona na ambae alifariki kwa ugonjwa huo nchini China: