BJEVI
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 1,359
- 251
Aliyekuwa makamu mkuu wa chuo cha saut padri Kitima,hii leo anaagwa rasmi kwa misa takatifu,na kumkaribisha mrithi wake padri Mgeni,ambae atazika kabisa mambo ya siasa na itikadi katika chuo hicho.
Wakati wa utumishi wake Kitima amekuwa akiikosoa serikali katika udhaifu wake hasa katika kutatua matatizo ya Watanzania wengi.
Kitima pia atakumbukwa kwa mahubiri yake ambayo kila mara yaliikosoa serikali,na jambo hili liliwafanya vijana wengi chuoni hapa hasa wale mashabiki wa CHADEMA kumshangilia kila mara alipoikosoa serikali.
Je!kuondoka kwake ndio mwisho wa CDM chuoni hapo?na je mrithi wake nae atakuwa ktk mlengo huohuo wa kichadema?hatujui,ila muda utasema.
kweli si wote wanaosoma wanaondokana na ujinga...Kwani kukosoa SERIKALI ni vibaya ..
Jifunze hili .Serikali siyo mbaya ila watendaji wake baba ee.!!!!