mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,502
- 256
Nukuu by Mwananchi.co.tz , Jumanne,Julai 30, 2013
Chama cha mapinduzi katika jiji la Mbeya kimepata pigo baada ya kada wao maarufu , David Mwankina (70) kukibwaga chama hicho na kujiunga na CHADEMA. Mzee huyo ambaye ni hakimu mstaafu alikabidhi rasmi kadi ya CCM kwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi (Sugu) Mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Baada ya kukabidhiwa kadi ya CHADEMA Mzee huyo alizungumza na kusema '' uamuzi wa kuachana na siasa za CCM umetokana na kusoma alama za nyakati na kudai kwamba tayari CCM hakina mpango mzuri kwa Watanzania. Alisema baada ya kuona CCM imepoteza msingi alioacha baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere, ni bora akahamia upande wa pili wa CHADEMA ambacho kina Uzalendo.