Kada CHADEMA azidi kuteswa

Kada CHADEMA azidi kuteswa

So sad and touching loh. Ee Mungu sikia kilio cha walio ktk shida. Ndugu na jamaa wa huyu kijana wanamaumivu makali. Anyway Mungu anaona.
 
Leo yeye kesho nani?
Mtanzania tafakari na chukua hatua kabla hayajakukuta, acha kushabikia huo siyo uzalendo, labda unafiki na uzandiki dhidi ya wanyonge na wazalendo wa nchi hii.
 
Mtuhumiwa wa ugaidi huwezi kutegemea akawa treated kama mtuhumiwa wa wizi wa bodaboda na ndiyo maana kwa kuliona hilo Marekani na washirika wake waliamua kuwaanzishia watuhumiwa wa ugaidi gereza lao maalum. Mtu hadi awe gaidi anakuwa na roho ngumu sana na nina uhakika hayo anayoyapitia hayafikii hata robo ya wanayokumbana nayo watuhumiwa wenzake walio chini ya serikali ya Marekani.

Naona unachangia kishabiki bila kuushirikisha ubongo wako na mfumo wa fahamu, ebu nifafanulie haya yafuatayo angala kwa ufupi

1. Kuna ushahidi wowote juu ya huyo jamaa kuhusika na tuhuma za Ugaidi na je kwa hali halisi ya neno Ugaidi linashabihiana na hayo anayotuhumiwa?

2. Said Kubenea alimwagiwa Tindikali je Serikali imeishawatia nguvuni waliofanya uhalifu huo? na kama bado WHY?
3. Yule aliyemuua mwangosi kule Iringa katika hati ya mashitaka anashitakiwa kwa kosa gani? je alichokifanya pamoja na Kamuhanda kwa nini na wao wasichukuliwe hatua kama Magaidi kwa matendo yao na maelezo ya kina yaliyoelezwa sioni tofauti na Ugaidi kama mnavyouzungumza.

4. Vipi kuhusu sakata la Mwakyembe kugeuzwa zeruzeru kwa ile sumu nalo limeishia wapi?

5. Vipi uteswaji wa Ulimboka ile kauli ya Pinda ya LIWALO NA LIWE ilimaanisha nini na je Mh. Pinda hausiki na UGAIDI? na Vipi yule Mkenya wa KOVA mbona kimya?

6. Vipi sakata la Kibanda aliteswa na akina nani na je wameisha kamatwa?

Naomba ufafanuzi usipofanya hivyo nitakuona ni mtu unayeshabikia vitu bila kujua nini unamaanisha.
 
Eti mtuhumiwa
haruhusiwa kuonekana lakini Tanzania Daima limejua kuwa anateswa. Yaani
utafikiri zile hadithi za watoto wanaobaleghe wanaoambiana kuwa "kila
siku silali usiku kucha na kila siku nakuota wewe!!!"

kaonana na mawakili wake!
 
Naomba wanachadema tutengeneze uzi unaotaja na kuwatambua wanachadema wahanga wote wa mateso ya polisi Tanzania. Kuna siku tutaandika kitabu cha mashujaa...
 
JESHI la Polisi Makao Makuu limeendelea kumshikilia kwa siku 11 bilakumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) mjini Bukoba, Evodius Justinian (30) huku ndugu zake wakizuiliwa kumpa chakula isipokuwa maji tu.

Justinian alishikiliwa mjini Bukoba Aprili 2, mwaka huu kisha kusafirishwa hadi jijini Mwanza na kuhojiwa, kisha Dar es Salaam huku akipewa mateso makali ya kulazimishwa akubali kuhusika kutengeneza video inayomhusisha na uchochezi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare.

Awali ndugu zake na viongozi wa CHADEMA mjini Bukoba walielezwa na polisi kuwa Justinian anasafirisha kwenda wilayani Igunga, Tabora ambako alidaiwa kuwaalitenda makosa ya jinai, lakini alifichwa jijini Mwanza.

Wakizungumza na gazeti hili, mawakili wa mtuhumiwa huyo Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatala walisema kuwa juzi jioni ndugu zake walimpelekea chakula,lakini walipofika waliambiwa kuwa haruhusiwi chakula isipokuwa maji tu.

“Asubuhi alipelekewa chai, lakini polisi walidai kuwa ndugu walichelewa na hivyo kuwazuia. Na walipopeleka chakula cha mchana waliambiwa hayupo kwani alikuwa amepelekwa hospitali bila kuitaja kwa jina,” alisema Kicheere.

Kicheere aliongeza kuwa baada ya ndugu kuwapa taarifa hiyo, yeye na wakili mwenzake Kibatala walilazimika kuondoka mahakamani Kisutu walipokuwawakimsubiri mteja wao afikishwe.

Mawakili hao walisema wanakusudua wakati wowote kupeleka maombi Mahakama Kuu kudai polisi wapeleke mwili wa mtuhumiwa mahakamani (habeas corpus).

Lakini pia mawakili hao walisema kuwa leo wataendelea kushinda mahakamani muda wote wa kazi kumsubiri mteja wao.

Waliwataka Watanzania wakiwemo wanasheria na watetezi wa haki za binadamu kuendelea kupiga kelele dhidi ya Jeshi la Polisi linavyokiuka haki za binadamu.

Akizungumzia hatua ya mtuhumiwa huyo kutofikishwa mahakamani kama ilivyokuwa imeahidiwa, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema wakiwa tayari watasema na kuomba watu wasiingilie kazi yao.
“Tutasema siku ya kumfikisha, hapa suala la msingi ni polisi tunafanya nini, ni kama wewe unavyoandika habari, hakuna wa kukuuliza,” alisema Senso.

Alipoelezwa juu sheria inavyotaka mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa, Senso alisema pasipo kufafanua kuwa sheria hiyo hiyo inaweza kutumika vinginevyo.

Jumatatu wiki hii, mbele ya wakili wake Kicheere, mtuhumiwa huyo alieleza unyama aliofanyiwa na jeshi hilo wakati wote wa mahojiano mkoani Mwanza na jijini hapa.

Katika maelezo yake yaliyoshuhudiwa na Ofisa wa Polisi Makao Makuu, Advocate Nyombi, Justinian alisema kuwa baada ya kutolewa mjini Bukoba kwa siri bila ndugu zake kujua, alipelekwa jijini Mwanza na kuhojiwa bila kuruhusiwa kuonana na wakili wake.

Alieleza kuwa wakati wote wa mahojiano hayo alikuwa akilazimishwa kukirikurekodi video ya Lwakatare inayoonesha mikakati ya ugaidi.

Alisema alisafirishwa kwa siri kwa ndege hadi Dar es Salaam, akapelekwa chooni na kupigwa, kutishiwa na kuteswa kwa nyaya za umeme na kunyimwa fursa ya kupewa chakula.

“Nimepigwa na polisi nikiwa Mwanza, nikiwa chooni Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati naletwa huku, polisi wakaniambia mimi ni mtu hatari sana, niseme nilifanya nini Igunga.

“Nikiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam niliomba kwenda chooni, waliingia pamoja na mimi wakanipiga sana, nimeshaandika maelezo kwa kulazimishwa, niliomba kuwa na wakili wakanikatalia,” alisema.

Aliongeza kuwa akiwa Dar es Salaam alihojiwa aseme ukweli kuhusu video ya Lwakatare. Akawajibu kuwa ilifanyiwa uhariri na Ludovick, lakini akapigwa makofi na askari wakaagiza nyaya za umeme za kutesea.

“Waliposema kuleta nyaya za umeme, kwa kuhofia mateso ya umeme nikasema hii video ni yangu,” alisema.

Source; Tanzania Daima
Haya magazeti ya Tanzania Daima na Uhuru yamekaa kipropaganda kila kukicha na kufabricate stories!
 
Mawakili walichelewa kupeleka maombi ya 'habeas corpus' Mahakama Kuu kwani maombi hayo yalitakiwa yafanywe punde baada ya mtuhumiwa 'kupotea'. Kikubwa nachokiona hapa bado ni 'impunity' katika vyombo vya dola.Nao wanakiri kuwa ni nani wa kuwauliza? Sheria wanaweza kuipinda wapendavyo kwani nayo inapindika pia.
Sheria ya ugaidi ilipitishwa haraka haraka kwa 'copy and paste' kiasi kuwa vitu vinavyofanana kama 'rendition' vilivyokuwa vinatumiwa na Wamarekani vinatumika kwa sasa hapa Tanzania.Katika sheria ya ugaidi dhamana kubwa ya uangalizi wa maamuzi kuhusu uhai wa mtu na nguvu ya kutumia wamepewa maafisa wa Polisi lakini ndiyo wa kwanza wanai 'abuse'. Yote haya ni mapungufu ya katiba na sheria zetu.
Ni wakati wa kulipeleka Jeshi la Polisi katika Tume ya Haki za Binadamu na kuanza kuwashitaki watumishi wa Jeshi hili mahakamani kama watu binafsi.. Pia uongozi wa Wizara inayosimamia Jeshi hili haitaepuka kuwajibika.

Nakuunga mkono kaka. Hivi nani anajua zilipo ofisi za Tume ya haki za binadamu. Kuna wanasheria wa kujitolea kuokoa maisha ya huyu kijana? Mwenye kujua aweke wazi hapa plz!!!!
 
Nakuunga mkono kaka. Hivi nani anajua zilipo ofisi za Tume ya haki za binadamu. Kuna wanasheria wa kujitolea kuokoa maisha ya huyu kijana? Mwenye kujua aweke wazi hapa plz!!!!
Executive Secretary
Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG)
Street : Plot No.8, Luthuli Street (Haki House)
Address: P.O.Box 2643
City: Dar es Salaam
Country : Tanzania
E-mail: chragg@chragg.go.tz,mary.massay@chragg.go.tz
Telephone:+255 22 2135747/8
Fax : +255 22 2111533,2111281

www.chragg.go.tz
 
Back
Top Bottom