Kachinjwa Mchana Kweupe ~ Moshi Bar

Kachinjwa Mchana Kweupe ~ Moshi Bar

Nyie hamjui jinsi wanavyoporwa piki piki na kuuwawa kikatili na hao wezi inauma sana wkt mwingine mm siwezi kuwalaum kwa hatua waliochukua kwa ukatili wanaofanyiwa na hao waporaji
 
Aisee watu hawana huruma, kuna jamaa anayedaiwa mwizi wa bodaboda kachinjwa Mchana huu pale Moshi Bar karibu Mazizini Dsm, ni kwamba jamaa alikamatwa maeneo ya Kigogo na madereva bodaboda, akapakizwa pikipiki watu 3 ye kawekwa katikati kaambiwa aelezee pikipiki alizoiba kaziweka wapi, bodaboda wakawa wanaitana kila wanapowaona wenzao, Wakaenda Kinondoni hawakuona pikipiki, jamaa akawaambia zipo maeneo ya gongolamboto Moshi bar, Wakaenda walipoona jamaa anawasumbua Wakaamua Kumchinja, mchana Kweupe.... Police wa Stakishari wamekuja kuuchukua mwili wake wameenda Muhimbili...

Tuache Wizi Jamani.... Tuache Makundi.
Muda wote huo Polisi hawakuona kiashiria chochote cha hatari? How do we know huyo jamaa ni mwizi kweli ama la? Hopeless, peaceful Tanzania!!
 
Serikali ya ccm imetujazia vibaka mitaani...
 
kwa nilichoona wezi wakimfanyia mtu leo.. HIYO ADHABU NI STAHIKI YAKE KABISA ..KAMA WAMEJIHAKIKISHIA NI MWIZI KWELI
 
Mmmh duh !!!!! yani mtu unachukua kisu kabisaa unamchinja mwenzako Mmmh! !!!!! Binadamu kweli tunapoelekea pataeleweka tu

Kama inafikia hatua ya sisi kwa sisi, wenyewe kwa wenyewe kukatishana uhai wakati muhusika wa hilo yupo duh!!!!!

Yatupasa kusali na kuomba

Duh!!!!
 
boda boda wana hasira maana wao wenyewe wanavyo ibiwaga ni ukatili mtupu..kwaio wakimdaka mmoja wanamtakbiirr kabisa
 
Duh, police wafanye uchunguzi kuwabaini wahusika. Maana ni hatari sana
 
Wizi mbaya mwisho wake ni mauti...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom