Kachinjwa Mchana Kweupe ~ Moshi Bar

Kachinjwa Mchana Kweupe ~ Moshi Bar

Sizinga

Platinum Member
Joined
Oct 30, 2007
Posts
9,519
Reaction score
7,289
Aisee watu hawana huruma, kuna jamaa anayedaiwa mwizi wa bodaboda kachinjwa Mchana huu pale Moshi Bar karibu Mazizini Dsm.

Ni kwamba jamaa alikamatwa maeneo ya Kigogo na madereva bodaboda, akapakizwa pikipiki watu 3 ye kawekwa katikati kaambiwa aelezee pikipiki alizoiba kaziweka wapi, bodaboda wakawa wanaitana kila wanapowaona wenzao, Wakaenda Kinondoni hawakuona pikipiki, jamaa akawaambia zipo maeneo ya gongolamboto Moshi bar.

Wakaenda walipoona jamaa anawasumbua Wakaamua Kumchinja, mchana Kweupe...

Police wa Stakishari wamekuja kuuchukua mwili wake wameenda Muhimbili...

Tuache Wizi Jamani.... Tuache Makundi.
 
Duh! Labda ajira,labda tabia,labda makundi! Mmmh ila hii ya kuchinjana hapana asee!!
 
bodaboda inabidi wadhibitiwe kama kila mtu anajichukulia sheria mkononi hiiitakuwa sio nchi bahati mbaya wanasiasa wanawatumia kama mtaji wao kisiasa
 
Yawezekana wenzake huyo mwizi walikua wana hamahama na pikipiki hizo zilizoibiwa,hii ni hatari sana tusipoangalia hawa bodaboda watazidi kujichukulia sheria mikononi,so sad.R.I.P marehemu.
 
Boda Boda washenzi sana. Yamkini hata hakuwa mwizi wa piki piki, akaamua kukubali yaishe.

Damu ya huyu mtu itakuwa juu yao washenzi hawa wanajifanya wao ndio polisi, wao ndio wanasheria, wao ndio mahakimu na wao ndio watekelezaji wa hukumu.

Aliomuuua watakufa vifo vya maumivu na fedheha kali sana. Mungu amewalaani.
 
Nalaani walichokifanya bodaboda,ila hao bodaboda wanajifunza.........Polisi wetu wamekua wauaji wa raia mara kadhaa,na hatua zinazochukuliwa dhidi yao ni kama "0" tu.....Nao bodaboda wanapita mulemule.Lakini pia mchakato ungeenda mahakamani ungekua mrefu sana,jamani mahakama zetu si mnazijua?Mwisho wa siku hata kauli za viongozi zinachangia.Mnakumbuka kauli hizi.
1."Anayeua albino nae auawe"
2."Polisi waue tu majambazi"
3."Wapigwe tu,tushachoka"
Tusizichukulie powa hizi kauli,,,zinahamasisha sheria mkononi
 
wanafuata mkumbo sana.wenyewe waita eti ushirikiano. Mmmh!

Bodaboda waliitana wakawa wengi... Walikuwa na hasira sana, police walipata taarifa kabla ya tukio wakawa wamejitahidi kwenda kuwaokoa ila nasikia gari yao ilipata pancha kabla ya kufika Moshi bar, tukio likawa limeshafanyika.
 
Hawa jamaa wa bodaboda wasipoangaliwa watatupeleka kubaya

Hawakupigwa picha? Hao waliofanya hivyo ni wahalifu pia, wanastahili adhabu ya kunyongwa, pengine jamaa hata sio mwizi alikuwa anawazungusha tu ku buy time ili aokolewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom