britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 15,636
- 30,004
Mnamo mwaka 1985,Mwalimu wa kemia wa shule ya sekondari Sengerema JOHN POMBE MAGUFULI aligombea ubunge wa Jimbo la biharamulo akichuana na mkulima PHARES KABUYE (wote CCM). PHARES KABUYE alishinda na kutangazwa kuwa mbunge JOHN POMBE MAGUFULI akarudi Sengerema kuendelea na majukumu yake ya kila siku ya ualimu (alirudi kufundisha
Mnamo mwaka 1990 Mwalimu JOHN POMBE MAGUFULI alichuana Tena na mkulima PHARES KABUYE kwa mara ya pili. PHARES KABUYE alimshinda tena JOHN POMBE MAGUFULI akafanikiwa kukitetea kiti chake
Mnamo mwaka 1995,wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Jimbo la biharamuro liligawanywa kwa kupatikana majimbo mawili (Biharamulo mashariki na Biharamulo magharibi. PHARE KABUYE aligombea ubunge wa Jimbo la biharamulo magharibi akashinda. JOHN POMBE MAGUFULI nae aligombea ubunge wa Jimbo la biharamulo mashariki na akashinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda kugombea ktk Jimbo la biharamulo magharibi.
PHARES KABUYE alikwenda kuhamia T.L.P aligombea na kushinda kuwa mbunge pekee wa chama hicho kabla ya kufariki kwenye ajali ya Basi mwaka 2009,mkoani MOROGORO.
Baadae Jimbo la biharamulo mashariki lilibadilishwa jina na kuitwa JIMBO LA CHATO chini mheshimiwa Mwalimu JOHN POMBE MAGUFULI mbunge wa Jimbo Hilo.
Britanicca