Kaburi la singeli 2018

Kaburi la singeli 2018

amos eglan

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
310
Reaction score
464
Huu muziki umekuja kwa kasi sana na kujizolea umaarufu Mkubwa kwenye media na baadhi ya wadau haswa vijana lakini huu mziki naliona kaburi lake 2018 kwa sababu zifuatazo
1. Wadau wakubwa wa muziki huu e FM ambao ndo waliubebea bango wameanza kuupa kisogo air time imepungua kabisaaa
2. Wasanii wengi wa singeli walioupaisha wamekosa management za uhakika na kuwafanya wakitaabika tu mitaani mfano. Man fongo , sholo mwamba
3. Wasanii wa muziki huu hawakai zizi moja hawapendani hawana maarifa na hawajui hata jinsi ya kuuinua muziki huu wakienda kwenye media wana kazi ya kupondana tu hakuna lingine
4. Muziki wa singeli umeanza kupoteza washabiki ambao walikuwa wamevutiwa na baadhi ya vibao vyao
 
Singeli wacha ife tu...maana haieleweki...bora zamani kulikuwa na mnanda...ninaamini mnanda ndo uliozaa singeli, Ila mnanda haukuwa na makelele kama singeli, Plus mnanda ulikuwa unachezwa kiume na sio kama hawa vijana wanaobinua migongo na kumwagiana maji wakati wakicheza singeli.
 
Nawakubali wanangu was Sarajevo,mwsnangu Ferguson, wekaaa wahuniiiiiiii!! oiiii babaaaaaa

mjinga haeezi kuelewaaaa!!

Bila bangi huwezi kuimba huu humziki
 
Huu muziki umekuja kwa kasi sana na kujizolea umaarufu Mkubwa kwenye media na baadhi ya wadau haswa vijana lakini huu mziki naliona kaburi lake 2018 kwa sababu zifuatazo
1. Wadau wakubwa wa muziki huu e FM ambao ndo waliubebea bango wameanza kuupa kisogo air time imepungua kabisaaa
2. Wasanii wengi wa singeli walioupaisha wamekosa management za uhakika na kuwafanya wakitaabika tu mitaani mfano. Man fongo , sholo mwamba
3. Wasanii wa muziki huu hawakai zizi moja hawapendani hawana maarifa na hawajui hata jinsi ya kuuinua muziki huu wakienda kwenye media wana kazi ya kupondana tu hakuna lingine
4. Muziki wa singeli umeanza kupoteza washabiki ambao walikuwa wamevutiwa na baadhi ya vibao vyao
Sipandi masingeli mimi.
Miziki ya watu wahuni hii hainaga ustaarabu yaani ni makelele bila mpangilio.
Nadhani asili ya muziki guy ni wavuta bhangi.
 
Singeli na wasanii wake watapita pia ila MSAGA SUMU ndio msanii pekee Wa aina hiyo ya muziki atakaesalia
 
Nawakubali wanangu was Sarajevo,mwsnangu Ferguson, wekaaa wahuniiiiiiii!! oiiii babaaaaaa

mjinga haeezi kuelewaaaa!!

Bila bangi huwezi kuimba huu humziki
Muziki wa mabaria ulikuwa mnanda...kama ni bangi basi kule ndo ilikuwa bila iyo kitu huimbi...plus jamaa walikuwa wanaimba kwa hisia mno kama reggae vile, Ndo maana hata namna ya uchezwaji wa mnanda ilikuwa ni kimawazo mawazo mno. Jaribu kutafuta nyimbo za mnanda utaliona hilo. Sio kama hawa watoto wa kiume wanaocheza singeli kutwa kukata mauno ya kike na kubinua migongo....Kiukweli wanaboa sana
 
Hahahah..

Watoto wa Libya.. Watoto wa Libya.. Watoto wa Sarajevo watoto wa mbwa roho mkononi.. Msalimie sadari kassim.

Singeli ni moja kati ya mziki mzuri sana.

1.watoto wa moto kombati
2.makabila dulla
3.shollo mwamba
4.man fongo
5.MSAGA SUMU (mwenye singeli yake)

sema huu mziki mtu mwenye staha inabd usikilize kwenye Simu kupitia headphones, ila sasa ukipita mtaani ukakuta wahuni wanakiamsha utatamani uingie kati, ila sasa kumbe umevaa suti unapita zako tu kisela, ukiangalia vile viuno vinaachiwa.

Ukitoa rege, na hip hop.. Singeli inafundisha maisha.

Chomaaaaaaaaaa bahariaaaaaa...
 
Back
Top Bottom