Kaburi la pamoja lagunduliwa Tripoli lenye miili 1,270 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi la pamoja lagunduliwa Tripoli lenye miili 1,270

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Sep 26, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,228
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  26 Septemba 2011 02:26

  ?


  Kaburi la pamoja la mamia ya watu lagunduliwa mjini Tripoli, Libya.

  Kaburi la pamoja linaloaminika kuwa na miili 1,270 limegunduliwa katika mji mkuu wa Libya, Tripoli baraza la mpito la nchi hiyo limesema.

  Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouwawa na maafisa wa usalama mwaka wa 1996 katika gereza la Abu Salim.

  Uasi dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi ulianza kama maandamano kutaka wakili aliyewakilisha familia za wafungwa wa Abu Salim aachiliwe huru.

  Uchimbuaji wa kaburi hilo la pamoja unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

  Baraza la mpito la kitaifa (NTC) liligundua kaburi hilo la pamoja- jangwa lililotawanyika sehemu za mifupa katika uwanja wa gereza la Abu Salim- baada ya kuwahoji walinzi wa gereza hilo waliofanya kazi wakati wafungwa hao waliuwawa baada ya kuadamana dhidi ya hali yao ya maisha.

  Baadhi ya sehemu za mifupa na nguo zilizochanika tayari zimepatikana.

  'makombora na risasi'

  Baadhi ya familia walizuru eneo hilo, miongoni mwao akiwa Sami Assadi, ambaye alipoteza kaka wawili katika tukio hilo.

  Alielezwa kaka zake walikufa kutokana na sababu za kawaida miaka mitano iliyopita. Alieleza BBC alivyojihisi alipofika mahali ambapo kaka zake huenda walizikwa.

  ''Nina hisia tofauti kwa hakika. Sote tulikuwa na furaha kwa sababu mageuzi haya yamefanikiwa lakini, wakati ninaposimama hapa nawakumbuka kaka zangu na marafiki wangu wengi sana ambao wameuwawa, na sababu hasa, ni kwamba hawakumpenda Muammar Gaddafi.''

  Mwandishi wa BBC Jonathan Head ambaye alifika katika eneo hilo anasema, hadi hivi majuzi ni habari chache sana ndizo zilijulikana kuhusu mauaji ya wafungwa hao.

  Watu wachache walioshuhudia tukio hilo wamelezea kuwa wafungwa hao waliuwawa katika seli zao kwa makombora na kupigwa risasi baada ya kuandamana.

  Maafisa katika serikali mpya wanasema watahitaji kufanya uchunguzi wa kisasa kusaidia kujua kilichofanyika katika eneo hilo.
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Gadafu anataka kuundiwa kosa la mauaji ya halaiki endapo atapatikana. Bora ajifiee huko huko alikojificha vinginevyo atadhalilika vibaya maana kila kosa litatafitiwa ushahidi ili aonokane hakuwa kiongozi bali dikteta.
   
Loading...