Kaburi la Kanumba lapusuka na kutitia....

jozzb

Member
Jun 30, 2011
87
20
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kaburi la aliyekuwa nguli wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ limeanza kuweka nyufa na kutitia ikiwa ni siku 5 tu tangu alipozikwa, Ijumaa Wikienda limelishuhudia.




Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandishi waetu walifika katika nyumba hiyo ya milele ya marehemu Kanumba kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar na kushuhudia hali hiyo huku nyomi ya watu mbalimbali ikiendelea kumimika eneo hilo kuweka mashada ya maua.






Kama hiyo haitoshi, baadhi ya watu waliofika kutoka mikoani ambao hawaamini kama kweli marehemu Kanumba hatunaye, walipiga picha ili kupeleka ushahidi huko walikotoka.

CREDIT: << KABURI LA KANUMBA LAPASUKA>>

 
Kwenye link hiyo nimeona picha ya kanumba, sijaona picha ya kaburi lilopasuka na kutitia.
 
Kwa wajenzi thats a normal phenomenon hasa ukizingatia na izi mvua za DSM!
 
Kama kaburi limejengewa (yaani limemiminwa zege) mwili wa binadamu kama waliovyo wanyama wengine anapokufa hivimba tumbo na baadaye kupasuka hii hutengeneza gesi ambayo lazima itafute EXIT ndio hupelekea ufa. Hakuna muujiza wowote hapa
 
Ndugu,

HIKI NI KIPINDI CHA MVUA KABURI NI LAZIMA LITITIE. KANUMBA LALA PANAPOSTAHILI. KWA SASA TUONGELEE MAMBO MENGINE YA KILIJENGA TAIFA LETU na SIO MARA MALI ZAKE, MARA MTOTO WAKE, MARA WACHUMBA WAKE n.K
 
jamani mbona n kawaida sana has pale mtu anapozkwa wakati wa jua udngo huwa unakuwa na nafasi sasa mvua inaponyesha soil compaction hutokea na hapo udongo hutitia na ndio maana nyufa hutokea. sidhani kama ni ktu cha kuandikwa hiki manake ni cha kawaida kabisa.
 
kama kamati ilichakachua mkwanja wa kujengea kaburi na kuleta fundi mchwara wa kumlipa kiduchu mnategemea nn?
 
Huenda ratio ya zege haikuchanganywa ipasavyo hivyo kulikuwa na kaburi feki.
 
jamani mbona n kawaida sana has pale mtu anapozkwa wakati wa jua udngo huwa unakuwa na nafasi sasa mvua inaponyesha soil compaction hutokea na hapo udongo hutitia na ndio maana nyufa hutokea. sidhani kama ni ktu cha kuandikwa hiki manake ni cha kawaida kabisa.

Huo udondo unaotitia ni upi?!, nikukumbushe; kaburi limejengewa kwa matofari na kuwekwa vigae(tiles) kisha likafunikwa na mfuniko wa zege- sasa kinachotitia ni nino?, BTW, mleta mada hajaweka picha ya hilo kaburi ili tuone mpasuko na kutitia, hizi hypotheses zinazotolewa hazina maelezo ya kisayansi: tuseme tu kuwa mzimu wa ndugu yake(babu yake) umechukizwa na kitendo cha kutoenda kuhifadhiwa kwenye shamba lake huko mwanza, nadhani babu anaona kama amedharauriwa, na mataona mengi mwaka huu.
 
Kwa ule umati wasingeweza kwenda sambamba na ujenzi ulio mzuri ila wanatakiwa kulijenga vzr kama hali ndo hii.
 
hiyo ni kawaida hasa na hizi mvua lazima lititie na hiyo inasababisha nyufa.
RIP Kanumba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom