Kaburi la Bibi Titi Mohamed

History zote ziko very very unfair..
Wanaokupenda wanaweza ongeza chumvi kidogo..
Wasiokupenda wanaweza ifuta au hata kupotosha historia ya kweli...
 
Laki...

Hujapata kuona mtu karim kama Salum Shamte.

Mlango wa nyumba yake ulikuwa wazi kwa kila muhitaji.

Kwa kipindi karibia miaka 10 tuko sote Tanga kila mwezi bila kukosa wala kumkumbusha akinipa fedha nimlipe mwalimu wa madrasa Muheza.

Siwezi kuhadithia yote.

Akipenda mambo ya kheri na mfuko wake ulikuwa wazi muda wote. Slim kawasomesha watoto wa nduguze katika imani udaktari chuo kikuu na leo watoto hawa wanatibu watu katika hospitali kubwa na wanawafaa wazee wao na watu wengine.

Hakuna watu watakaoelemewa na msiba huu kama ndugu zetu wa Tanga.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa. Hata majizi na mafisadi nayo yanaweza kuwa makarimu kinafiki kama Rugemalira ili mradi yapate misifa kutoka jamii wanayoishi lkn kwao hizo pesa wanazogawa ni small change tu ukilinganisha na pesa wanazodhulumu. Huyo marehemu alifariki akiwa na kesi ya kujibu dhidi ya Jamhuri.
 
KABURI LA BI. TITI MOHAMED, KISUTU

Siku tatu hizi zimekuwa ngumu sana kwangu na naamini na kwa wenzangu wengi tuliokulia Dar es Salaam kwa kuondokewa na wapenzi wetu.

Juzi nikiwa nimesimama pembeni mwa kaburi tukimzika mmoja wa wapendwa wetu jicho langu lilivutiwa na kaburi lililokuwa pembeni kwa jinsi majani ya kijani yalivyokuwa yameota kama vile kuna mtu ananyeshea majani yale maji kila siku na kupalilia.

Kaburi hili ni kaburi la Bi. Titi Mohamed mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika.

Bi. Titi alipata kuniambia nyumbani kwake nilipokwenda kutaka kufanya mahojianonae ya historia ya maisha yake wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.

Alinambia, ''Bwana Mohamed una lipi wewe la kuandika kuhusu mimi ambalo bado halijaandikwa?''

Hakika sikuwa na jipya ambalo halikuwa limeandikwa kuhusu Bi. Titi lakini pia nilikuwa na mengine ambayo yeye hakuyasema kuhusu maisha yake na wengi hawayajui lakini wale waliokuwapo wakati wa kupigania uhuru walinieleza.

Abbas Sykes na Tewa Said Tewa walipata kunieleza mengi kuhusu Bi. Titi na uwezo wake katika kuhamasisha umma wakati wa kupambana na Waingereza.

Nitalieleza moja.

Abbas Sykes anasema, ''Tuko chini ya jukwaa tunasubiri kuanza mkutano Mnazi Mmoja.

Nyerere anataka kupanda jukwaani lakini anatuambia kuwa nachoka na hana jipya la kusema.

Nyerere hakika amechoka basi atamwendea Bi. Titi, ''Titi hebu anza wewe kuzungumza,'' Mwalimu atamwambia Bi. Titi.''

Bi. Titi atapanda jukwaani akisindikizwa na nyimbo mashuhuri ya TANU iliyokuwa ikiimbwa na Bi. Hawa Maftah na kundi lake la akina mama:''Muheshimiwa nakupenda sana wallah sina mwinginewe, In Shaa Allah Mungu yuko Tanganyika tutajitawala.''

Bi. Titi atakapoanza kuzungumza uwanja utalipuka kwa vimondo ambavyo Bi. Titi anavirusha.

Bi. Titi anawauliza Waingereza, '' Hivi nyie hamna kwenu? Kwa nini mnatung'ng'ania hivi ondokeni nendeni kwenu. Nyie watu gani msiojua kukataliwa?''

Vifijo vinazizima uwanja mzima.

Mwalimu Abbas Sykes akanambia kuwa kutokana na hotuba ile ya Bi. Titi Nyerere atakuwa kapata ''cue'' na atakapopanda jukwaani Nyerere atapita mle mle alimopita Bi. Titi lakini kwa namna nyingine ya kuhutubia.

Allah mrehemu mama yetu na lifanye kaburi lake kuwa moja ya mabustani ya peponi.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ujinga mtupu. Hadithi hizi kawasimulie wajukuu au vitukuu vyako wakienda kulala. Huyo Abbas Sykes kama yeye kweli alikuwa kidume na shujaa wa kupigania uhuru kama unavyomtukuza, kwanini hakupanda yeye jukwaani kuhutubia huo umati hadi amwombe mwanamke? Muislamu gani huyo? Wee zee zima huna haya na story za kutunga? Pumbaaf!
 
Hata sisi watu wa kigoma tulitoa mchango Sana Ila leo tunaonekana wakimbizi
Watu wa pwani hasa Dar es salaam wana mchango mkubwa sana katika kuzaliwa kwa taifa hili (Tanzania), na inasemekana Nyerere alipewa msaada mkubwa Sana na wenyeji wake wa Dar kipindi Cha harakati za ukombozi. Ila Cha ajabu hv Sasa watu wa pwani wamekuwa wakibezwa sana Kama si lolote.

Hivi ukiachia ile barabara iliyopewa jina lake, huyu Malkia ana kumbukumbu gani nyingine hapa nchini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom