Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
tuite koleo,koleo, nimekuwa kwenye kundi sogozi la watsapp ghafla zikaanza kurushwa picha nyingi za baadhi ya wanasiasa wa nchi za ng'ambo hususani Africa na kwingineko. Wengi walionekana kukerwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kung'ang'ania madaraka hata pale wanapokuwa hospitalini wakiuguzwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Kwa sababu jambo hilo lilitokea katikati ya mkutano wa SADC mwingine akarukia ''angalia hata huyu Mswati hana msaada wowote kwa taifa lake lakini anatawala milele'' hawa waliotawala mjadala huu wanajiita ''wanamabadiliko'' wanataka kuona Afrika na Tanzania inatawaliwa na vyama tofauti na vile vya ukombozi.
Ndugu mmoja alinitumia ujumbe binafsi akitaka asikie maoni yangu nikamwambia kijana wangu jiulize haya maswali kwanza;

- Je Tundu Lisu si mgonjwa zaidi ya mwaka? mbona yeye hatajwi? je si Tundu Lissu ndiye alisema bado hajapata ruhusa toka kwa daktari wake akimjibu spika ndugai?
- Hivi unajua malkia Elizabeth katawala uingereza toka mwaka 1952?
- Unakumbuka kuwa katiba ya pendekezwa ya Jaji Warioba ilipendekeza kuwa mbunge akiugua miezi sita mfululizo aachishwe na Tundu Lissu anaiunga mkono? unakumbuka JK alipojaribu kushauri kuwa ''hii itasababisha wabunge waende majimboni na dripu'' Tundu Lissu walimtukana huku wakimbeza kwa maradhi Mh.JK aliyokuwa akiugua (tezi dume)?
- Unakumbuka Tundu Lissu ndiye alikuwa kinara kupinga wajumbe wa Tume ya Warioba wasilipiwe bima ya afya?