Kabla ya kumpigia kura kuwa John Pombe Magufuli kuwa rais wa Tanzania soma hapa

Sheria ya Mipango Miji. Na. 8 ya mwaka 2007 imeweka masharti kuwa ujenzi wa nyumba mijini (KATIKA Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji, Miji midogo n.k) ni sharti mhusika aombe na kupata kibali cha ujenzi, yaani (building permit) kutoka kwenye mamlaka husika kabla ya kuanza ujenzi. Na yeyote atakaye jengo mijini bila kibali cha ujenzi, jengo husika linastahili kubomolewa na mhusika kushitakiwa.

Ikumbukwe kuwa vibali vya ujenzi hutolewa kwa viwanja vilivyopimwa tu, ilihali ni 10% tu ya ardhi yote ya Tanzania ndio imepimwa. Zaidi ya 90% ya watanzania wanaishi katika ardhi isiyopimwa vijijini na mjini. Kwa mijini hali ni mbaya zaidi ambapo hata viwanja vinavyopimwa na Serikali ya CCM huuzwa kwa bei ya kuanzia Milioni 6 na kuendelea, na kuwafanya wananchi wengi hususan wa vipato vya chini (ambao ndio wengi sana) kutoweza kumudu bei hivyo hulazimika kujenga kiholela katika ardhi zisizopimwa. Na kwa maana hiyo wamekuwa wamevunja Sheria za Mipango Miji, Na. 8 ya mwaka 2007 bila ya kujikua

Miaka ya 1970 Serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Nyerere ilitekeleza “Operesheni Vjiji” ambapo baadhi ya wananchi walihamishwa kwa nguvu toka makazi na mashamba yao na kuhamishiwa katika vijiji vya ujamaa vilivyoanzishwa. Baadhi ya vijiji hivyo vilianzishwa pembezoni mwa baadhi ya barabara zilizokuwepo au kuwa katika ramani zilizoandaliwa na wakoloni tokea mapema 1932. Kutihibitisha kuwa Serikali ndio iliwahamishia wananchi hao hapo ikawajengea majengo ya huduma mbali mbali ya huduma kama vile hospitali, zahanati, shule n.k.

Kutokea mwaka 1995 Mhe John Magufuli alipoteuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi alianza kuwatendea wananchi hawa unyama uliokithiri ambao haukuwahi kufikiriwa kuwa unaweza kutendwa na kiongozi wa nchi ya Tanzania hususan kutoka chama cha CCM ambacho wakati wote hujinasibu kuwa kinawajali wanyonge kwa kubomoa nyumba zao pasipo malipo yoyote fidia, kuziwekea nyumba hizo alama za X na unyama mwninge mwingi toka maafisa walioko chini yake. Amekuwa akifanya hivyo ili kuokoa fedha na aweze kutekeleza kmiuradi mingi zaidi ya barabara na kujipatia sifa binafsi pasipo kujali ni kinazitokea kaya anazozibomolea makazi na kutwaa kinguvu ardhi zao.

Matendo hayo ya kinyama yamewasababishia wananchi hawa madhara mbali mbali ya kijamii na kiuchumi. Baadhi ya wananchi hawa wameugua magonjwa mbali mbali yanayohusiana na mishtuko ikwemo BP, kupooza n.k na baadhi yao wamepoteza maisha na kuacha watoto wajane, yatima katika hali ya umaskini wa kutupa kutokana na unyama huo uliokithiri. Wakati haya yakitendeka Mhe John Magufuli aliendelea kukaa katika baraza la Mawaziri ambalo lilikuwa likiruhusu mabiliano ya fedha kufujwa huku akikataa kuwalipa wananchi fidia hata kidogo.

Hivyo basi kutokana na ahadi lukuki mgombea wa CCM Mhe John Magufuli anazotoa ni dhahiri kuwa Serikali yake itahitaji fedha nyingi kuzitekeleza, hivyo serikali yake haitakuwa tayari kuwalipa fidia yeyote wananchi watakaolazimika kupisha ujenzi wa miradi mikubwa na mingi anayoiahidi katika kampeni zake. Na kana alivyowafanyia wananchi waliotajwa hapo juu, kila mara ardhi ya kujenga viwanda, miradi anayoahidi atatumia Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya 2007 kuwanyima fidia na kudai kuwa wamejenga holela.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi cha maika 20 aliyotumikia Serikjalini ameonyesha dhahiri kuwa mtu asiye zingatia haki za binadamu, asiyekuwa na huruma na wananchi hususan wananchi maskini na wanyonge. Kwa hali hiyo sisi ambao tayari tumeguswa na kuthirika na unyama wa ajabu aliotundea Mhe Magufuli ndani ya miaka hii 20 iliyopita tunachukua fursa hii kuwaonya watanzania wenzetu wote waliojenga katika Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji, Miji midogo na popote mijini bila vibali vya ujenzi kuwa mko katika hatari kubwa ya kubomolewa nyumba zenu kutokana na kuvunja Sheria ya Mipango Miji. Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007. Matumizi mabaya ya madaraka kama inavyoelezwa hapo juu yaliwahi kufanyika nchi kama vile Zimbabwe n.k

Kama Mhe John Pombe Magufuli ndani ya Tanzania huru ameweza kutumia Sheria za mkoloni za mwaka 1932, 1940,1955 n.k kuwanyanyasa mamilioni ya wananchi waliohamishiwa na TANU na CCM katika Vijiji vya ujamaa vilivyoko pembezoni mwa barabara mbali mbali zilizokuwepo au kuwa katika michoro ya wakoloni, hatasita kutumia Sheria ya Mipango Miji. Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007 iliyotungwa na bunge letu huru kuwanyanyasa wananchi waliojenga bila vibali vya ujenzi ili kuokoa fedha za utekelezaji wa miradi aliyoaihidi katika kampeni zake.

Kila mara dunia inapotaka kuwaweka madarakani watu wenye silika za kutozingatia haki za binadamu tunapaswa kukumbuka kuwa hata Dikteta anayeongoza hap duniani Adolph Hitler wa Ujerumani aliingia madarakani kupitia sanduku la kura, na hatimaye watu milioni 50 duniani walipoteza maisha.

HIVYO KABLA YA KUFIKIRIA KUMSHABIKIA MAGUFULI KUWA RAIS WA TANZANIA HAKIKISHA UNACHO KIWANJA KILICHOPIMWA AMBAVYO SERIKALI YA CCM HUVIUZA ZAIDI YA MILIONI 6 KWA KIWANJA CHA MITA 20X20 NA UMEJENGA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI, LA SIVYO ITAKULA KWAKO.
Maelezo yako ni upuuzi wa karne.
Magufuli atastafu 2025, over!. Utake usitake!

Unachofanya ni Sawa na kuloa maji kwa kutumia tenga.
Aneweza zuia Magufuli asifike 2025 ni Mungu pekee, binadamu wachovu model yako hamna ubavu, sanasana ni ngonjera tu
 
Kwa mwendo huu lazima akili zifunguke tu ila tatizo sasa Chebukati wetu hatamsukumizia tena ?
 
2025 na yeye anamsukumia mwingine kwenye uongozi yani lazima nchi inyooke
 
Back
Top Bottom