Kabla ya DOT COM

Kabla ya DOT COM

Kulikuwa na Chama kimoja, chama kushika hatamu
Kulikuwa na SHIHATA Shirika la Habari Tz
Kulikuwa hamna magazezi ya UDAKU.
Chakubanga alikuwa bonge ya staa
Nipashe ndio ilikuwa sehemu pekee ya kuchekesha kwenye gazeti la MFANYAKAZI
Redio Tanzania ndio ulikuwa mpango mzima, hakukuwa na FM
Motomoto lilikuwa ndio gazeti la kwanza la binafsi
Tulitii bendera, hata ya CCM ikishushwa au kupandishwa lazima usimame
Redio ilikuwa mwisho saa sita
Hakukuwa na Tv stesheni
Mama na mwana ilikuwa na wasikilaji kibao, hata wazee
Kulikuwa na somo la Siasa na KIlimo pia Sayansi Kimu
Juma na Roza walifahamika nchi nzima
Shule maarufu ilikuwa Mtakuja Primary School
Ukiwa na kitabu cha Willie Gamba wee ni noma
Lyrics tuliandika kwenye madaftari
Hakukuwa na CD, kanda ndio ulikuwa mpango mzima


Hebu ongezeeni tuwape shule watoto wetu wa dot com

Yaani hapo pa Juma na Roza...mtu ulikuwa unakremisha "huyu ni Juma....Juma anasema...kimbia ng'ombe kimbia upesi...baba ana njaa" cause ulisoma/kutamka bila kuangalia kitabu, mwalimu akisema "onyesha kimbia iko wapi" unatoa macho...chezeiya kukremisha weye???
 
Dj J.DILINGA,..njoo changia mada na wazee wenzio!
 
Yaani hapo pa Juma na Roza...mtu ulikuwa unakremisha "huyu ni Juma....Juma anasema...kimbia ng'ombe kimbia upesi...baba ana njaa" cause ulisoma/kutamka bila kuangalia kitabu, mwalimu akisema "onyesha kimbia iko wapi" unatoa macho...chezeiya kukremisha weye???
Sista alimeza kitabu kizima kuanzia mwanzo hadi mwisho, hapo alikuwa anasoma vidudu, dingi akawa anajisifia kwa wenzake kuwa mtoto wake yuko vidudu lakini anajua kusoma.
Siku moja wageni walitutembelea, kwa masifa akaenda kuchukua kitabu ili awasomee.
Mgeni mmoja akamfungulia ukurasa wa katikati, sista akaanza kutiririka kuanzia ukurasa wa kwanza wakati kafunua ukurasa wa 14
 
Tanzania beats you cause it offers the best safari packages and nothing of Al Shaabab a reason why a tourist is willing to spend more in TZ than in KE! And just to inform you Southern circuit i.e. selous+Katavi+Ruaha+Mafia is completely unexplored and with the opening of Songwe International Airport count more loses since Tanzania will keep on beating you guys three combined! Not to forget Western Circuit lake Tanganyika + lake Victoria with numerous islands and Saanane+Mahale+Gombe NPwhen expansion and modernization of Mwanza Airport is complete...:A S 103:

Ww muongo wapi na wapi RTD na mchezaji wa Ubelgiji
 
mi nimemfaidi ezekiel malongo enzi anatangaza mpira...

enzi za utangazaji wake,
kulikuwa na mchezaji mmoja wa kongo alikuwa anaitwa mbo mpenza!

basi jamaa alikuwa akitangaza akifikia kwenye mbo mpenza, hataji full name qulaleki.. ananishia kusema mpenza! mpenza!

aisee i loved ezekiel malongo soo much during my child hood!

Ww muongo RTD na mchezaji wa Ubelgiji wapi na wapi
 
Ww muongo RTD na mchezaji wa Ubelgiji wapi na wapi

aisee sipendi watu wanaopanik unajua... wapi nimeandika ubelgiji mkuu?

btw, mbo mpenza kazaliwa kongo, then kahamia belgium... next time uwe unasoma kwanza kabla hujatuhumu watu...
 
Mr Daudi, Mrs Daudi,Musa,Neema na Baraka hivi yule baraka hajakua tu sasa atakuwa mtu mzima na Mr and Mrs Daud watakuwa wazee sasa hahaha
 
Kabla ya Dot.com kwenye somo la kiingereza tulikuwa tunaimba
when I was a farmer, a tailor, yani tulikuwa tunataja fani ambazo sikuiz zinadharaulika kutokana na mfumo mbovu wa serikali
 
nimemiss zamani..
images
 
Sista alimeza kitabu kizima kuanzia mwanzo hadi mwisho, hapo alikuwa anasoma vidudu, dingi akawa anajisifia kwa wenzake kuwa mtoto wake yuko vidudu lakini anajua kusoma.
Siku moja wageni walitutembelea, kwa masifa akaenda kuchukua kitabu ili awasomee.
Mgeni mmoja akamfungulia ukurasa wa katikati, sista akaanza kutiririka kuanzia ukurasa wa kwanza wakati kafunua ukurasa wa 14
.. Ha! Ha! Ha! Ladies and Gentlemen...And the Winner is ---- Sista wake Bujibuji. Lol!:wink2:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom