Karot
JF-Expert Member
- Mar 6, 2017
- 1,159
- 1,316
Habari za mihangaiko wanajamii wenzangu.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Wakuu ni hivi; kuna jamaa ambae tulifahamiana kwa ukaribu kidogo, ila sijawahi kuona familia yake (Baba na mama) isipokua mke wake tu.
Sasa katika urafiki ule kuna biashara aliigusia, ambayo ananiambia alishawahi kuifanya na inalipa kiasi ni kununua spear za simu kutoka Dar to Zanzibar. Ambapo alinambia ambapo angekua na mtaji japo kidogo angefanya ila amekwama hana cha kuanzia.
Akaniomba mimi nimpe mtaji huo ili tufanye hiyo biashara. Mtaji wenyewe amenambia nimpe japo m2 amenihakikishia ndani ya miezi 6 amerudisha mtaji huo.
Mimi kusema ukweli napenda kufanya biashara ila sina uwezo wa kusimamia kutokana na shughuli zangu za hapa na pale. Kwakweli amenishawishi sana, ila naona kama roho inasita kufanya hivyo, maana kuna mdada mmoja alinambia mambo kama hayo ila alichonifanyia alinisababishia niondoe uaminifu kwa watu wote kwenye pesa.
Nimeona kabla sijafanya maamuzi yoyote nije hapa niwashirikishe wenye akili na maarifa kunizidi mimi. Labda kuna chochote kile ambacho unaweza kunishauri na kikawa kizuri zaidi kuliko hiki nnachofikiria mimi.
Mawazo yangu mimi ni kwamba kabla hatujafanya chochote tuende tukaandikishane aidha polisi au mahakamani ili kukwepa usumbufu ambao utakuja kujitokeza kama atakuwa kigeu geu.
Pili ni kwamba kwa mnavyofahamu mimi mtaji mara nyingi unakua mdogo kama unaanza, sasa nilijipanga nije nimpe m1 kwanza.
Je nyinyi mnanishauri vipi kuhusiana na hili?