Kabla hatujamhukumu Halima Mdee na wenzake, kuna yeyote kati yenu atagoma ikiwa atateuliwa na Rais kwenye nafasi zake?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,515
27,006
Rejea tena kichwa cha mada hapo juu.

Muda unakimbia kwa kasi na mengi yanatokea na kupita, kumbukumbu huwa zinabaki.

Huenda sina kumbukumbu za kutosha, lakini kwa kadri ya 'hansadi' zangu sikumbuki mtu aliyewahi kuteuliwa kwenye ulaji na akagoma ili kulinda kile kinachoitwa msimamo wa chama.

Kama yupo/wapo basi tukumbushane, na pia tuhusianishe sababu zao kugomea uteuzi na mazingira halisi ya nyakati zao.

Ninaowakumbuka mimi ni wale waliokuwa mstari wa mbele, lakini ghafla wamekuwa watiifu na wachapakazi kweli kweli.

Mifano ipo mingi, sina haja kuitaja hapa labda ikihitajika.

Sasa basi, mara paap Rais JPM akaamua kuwajumuisha kwenye serikali yake hawa watu ambao leo wanaonekana mwiba na mahiri kuwashambulia wabunge walioapishwa.

Ni nani atagoma?

Hakuna asiyeijua njaa ilivyo kali huku nchi kavu, nguvu ya mamba ni maji. Sio Halima pekee mwenye njaa au hicho kinachoitwa tamaa, pengine tunawaonea wivu kwamba ni ganda la ndizi.

Yule mtu angeweza kususia uteuzi na awe wa kwanza kuwanyooshea kidole hawa wabunge.

Ncha kali.
 
Halima Mdee kateuliwa na Rais?
 
CCM hawana akili hata kidogo walitumia nguvu kubwa kwenye unyang'anyi wa kura wakasahu kuna hela za mebeberu ambazo zinaifanya ccm ipumue wanawaponda mebeberu huku hela zao wanazitaka bila kambi ya upinzani hela za mebeberu hazipo pumzi ya ccm ipo kwa mabeberu mnataka nchi ya kijani wakati mfukoni yaani uchumi upo hoi mtafoji kila kitu safari hii na hii laana itaendelea kutafuna chama cha kijani.

Wenyewe ccm mmerudi tena chadema
 
Katiba na sheria za vyama vya siasa vimekanyagwa waziwazi na NEC kwa kushirikiana na Bunge!
Wamepata wapi mamlaka ya kupitisha majina ambayo hayana baraka za chama kwa maana ya kamati kuu?Huu ni uhuni na upuuzi wa kiwango cha juu!
Kama hili likipita,huenda miaka ijayo NEC ikaamua iteua wagombea ubunge wa upinzani kwenye majimbo ambao hawajapitishwa na vyama vyao!
Nchi hii inaongozwa na washamba
 
Back
Top Bottom