Bwana Banzi
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 464
- 251
- Thread starter
-
- #21
Shukran kwa nyongeza nzuriWakutu wameshajichukulia kama kabila ila kiuhalisia wakutu ni Waluguru wa bondeni ambao ndio wametoa wazaramo. Wazaramo wengi wanalijua hilo kuwa asili yao ni ukutu, na wakutu nao wanalijua hilo kuwa asili yao ni Uluguru. Wakutukila kuhisi, ni kiluguru kikimaanisha wamedondokea bondeni. Na ndio uhalisia. Zamani jamii ziliishi katika makundi ya koo, hakukuwa na makabila. Ila koo hizo zilikuwa zikifanana katika mambo mengi na pia zilikuwa zikihamahama kwa sababu mbalimbali. Wakutu ni baadhi ya koo za Uluguruni zilizoelekea maeneo ya bondeni. Ukichunguza vizuri koo za wakutu na wazaramo, utagundua kuwa zaidi ya asilimia 90 ni koo za Kiluguru, na kuna koo chache sana ambazo haziko uluguruni, Na Waluguru wana koo nyingine ambazo haziko kwa wakutu na Wazaramo na Wakwere. Hitimisho. Ukitaka kujua nani ni muhasisi wa hizi jamii, jaribu pia kuchunguza tamaduni nyingine kama Ngoma na maeneo ya tambiko. Wakutu, Wazaramo na Wakwere wote wanatambua kuwa kwenye mzimu wao ni Kolelo ambako ni Uluguruni. Ili kupata uthibitisho wa hili, tafuta wale wazee haswa wanaojua historia za jamii zao.
Naunga mkono uamuzi wakokuanzia leo mimi ni mkutu na ntajitambulisha hivyo
natokea kijiji cha mvua
Mzimu wa kolelo ni maarufu sana,je twaweza pata historia yake?Wakutu wameshajichukulia kama kabila ila kiuhalisia wakutu ni Waluguru wa bondeni ambao ndio wametoa wazaramo. Wazaramo wengi wanalijua hilo kuwa asili yao ni ukutu, na wakutu nao wanalijua hilo kuwa asili yao ni Uluguru. Wakutukila kuhisi, ni kiluguru kikimaanisha wamedondokea bondeni. Na ndio uhalisia. Zamani jamii ziliishi katika makundi ya koo, hakukuwa na makabila. Ila koo hizo zilikuwa zikifanana katika mambo mengi na pia zilikuwa zikihamahama kwa sababu mbalimbali. Wakutu ni baadhi ya koo za Uluguruni zilizoelekea maeneo ya bondeni. Ukichunguza vizuri koo za wakutu na wazaramo, utagundua kuwa zaidi ya asilimia 90 ni koo za Kiluguru, na kuna koo chache sana ambazo haziko uluguruni, Na Waluguru wana koo nyingine ambazo haziko kwa wakutu na Wazaramo na Wakwere. Hitimisho. Ukitaka kujua nani ni muhasisi wa hizi jamii, jaribu pia kuchunguza tamaduni nyingine kama Ngoma na maeneo ya tambiko. Wakutu, Wazaramo na Wakwere wote wanatambua kuwa kwenye mzimu wao ni Kolelo ambako ni Uluguruni. Ili kupata uthibitisho wa hili, tafuta wale wazee haswa wanaojua historia za jamii zao.
Wamefikaje hapo mbona mbali sana na kwao?Pia hapo kidatu/ruaha kuna wakutu wa kutosha ila hujitambulisha wazaramo
Itakuwa migration tu za zamani ila wapo wengi sana hapoWamefikaje hapo mbona mbali sana na kwao?
Ni ukoo wa Mamba au Momba?Kuna Mkutu kutoka ukoo wa Mamba, anasema kabila lao wana roho mbaya sana.
Sifahamu mkuuNi ukoo wa Mamba au Momba?
Nadhani ni Momba.
Mamba Waluguru, Momba wakutu.Sifahamu mkuu
Bado mnaoata muda wa kuongelea makabila!!!! Du!!!!Wakutu ni Kabila linalopatikana mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Pwani. Kwa mkoa wa Morogoro wanapatilana katika wilaya ya morogoro ( Morogoro vijijini ) katika vijiji vya Dutumi, Mvua, kisaki, Ngerengere, Matuli, Kidunda, Kiwege, Lilongwe,Kongwa, Magogoni, Kilengwe, Kwaba n.k.
Katika mkoa wa Pwani wanapatikana katika wilaya ya kibaha( magindu, Dutumi ya kibaha, Chaduma, kisangire na baadhi ya maeneo ya wilaya ya kisarawe na chalinze. Ni Kabila kubwa ila nadra kukutana na watu wa Kabila hili la kikutu, Wakutu wengi wanakopatikana maeneo ya mkoa wa Pwani hujitambulisha kama Wazaramo au wakwere. Na wengine hujitambulisha kama waluguru, hivyo sio rahisi kukutana na mtu wa Kabila la kikutu, japo kuwa ni Kabila kubwa mojawapo kwa mkoa wa Morogoro na Pwani.
Maana ya Kabila la WAKUTU:
Neno Wakutu limetokana na neno la Kiluguru ( wakutuka ), maana yake waluguru waliodondoka au wanaoishi mabondeni. Neno wakutuka ndio limezaa Kabila la Wakutu. Wale wa mlimani ( waluguru ) waliendelea kujiita waluguru na wale wenzao ambao wanaoishi mabondeni waliendelea kuitwa Wakutu na ndugu zao wa mlimani, hiyo ndo chanzo cha Kabila la Wakutu, na mwisho wa siku wakajitenga na kuwa makabila mawili tofauti makubwa.
Zifuatazo ni baadhi ya koo katika Kabila la Wakutu:
1. Wanyange; mwanaume nyanga mwanamke mlanyanga ( kwa waluguru mara chache hutumia nyanga na mlanyanga, waluguru hutumia mkude,au kunga'aro na mwanamke huitwa mwenda )
2. Wanyange; mwanaume huitwa nyange, mwanamke mlanyange.
3. Wa mlali; mwanaume huitwa mlali na mwanamke huitwa mlamlali ( kwa waluguru; mwanaume bwakila , mwanamke mlali au mlamlali).
4. Wabena; mwaume mbena, mwanamke mlambena.
5. Wakiraru; mwanaume kiraru, mwanamke mlakiraru.
6. Wahafigwa; mwanaume mhafigwa, mwanamke mlahafigwa.
7. Mponda; mwanaume mponda, mwanamke mlamponda.
8. Zongo; mwanaume zongo, mwanamke mlazongo.
9. Wa mindu; mwanaume semindu, mwanamke mindu.
10. Wa mng'ango; mwanaume mng'ango, mwanamke mlamng'ango.
11. Wakali; mwanaume mlali, mwanamke mlamlali.
12. Wa chuma; mwanaume chuma, mwanamke mlachuma ( kwa waluguru; mwanaume mponda, mwanamke chuma).
13. Wa kwambe; mwanaume mkwambe, mwanamke mlamkwambe.
14. Wa tebe; mwanamke mlatebe, mwanaume tebe.
15. Wasagara; mwanaume sagara, mwanamke mlasagara.
16. Wahimbwa; mwanaume dihimbwa, mwanamke mladihimbwa.
17. Wa chogeza; mwanaume chogeza, mwanamke mlachogeza.
18. Wakiluwa; mwanaume kiluwa mwanamke mlakiluwa.
19. Wakongela; mwanaume kongela, mwanamke mlakongela.
20. Watonga; mwanaume mtonga, mwanamke mlamtonga.
21. Wa chili; mwanaume mchilo,mwanamke mlamchilo
22. Wa mbali; mwanaume m'bwali, mwanamke mlam'bwali.
Hizo ni baadhi ya koo za Kabila la Wakutu, utaona kwa asilimia zaidi ya tisini zinafanana na koo za waluguru au wazaramo au wakwere.
Lugha ya Wakutu;
Baadhi ya maneno ya kikutu, mfano; aulamke (umeamkaje)? Unajibu anoga ( vizuri), imanye gwegwe ( sijui wewe). Ausindile ( ushindaje)?, Ukae ( nyumbani), ukae kutali ( nyumbani mbali). Kwa ufupi lugha ya kikutu ni sawa na lugha ya kizaramo, kikwere au Kiluguru .
Ngoma za asili za Kabila la Wakutu ni Vanga, mdundiko, n.k. Hayo ni machache yanayohusu Kabila Wakutu, wenyeji wa mkoa wa Morogoro na manispaa ya Morogoro.
Kwa uchache.Mzimu wa kolelo ni maarufu sana,je twaweza pata historia yake?
Tunaongelea Makabila kwakuwa yametunza hazina ya historia ya mtu mweusi.Bado mnaoata muda wa kuongelea makabila!!!! Du!!!!
Ahsante Mkuu,naomba ukileta huu uzi unitagKwa uchache.
Mzimu wa Kolero ni Mungu wa Waluguru na jamii zake.
Mzimu huu ulikuwa unaishi kwenye pango lililo chini ya mlima Lubasazi kando ya mto Lubasazi, kijiji cha Lubasazi kwenye kata ya Kolero tarafa ya Mvuha Morogoro vijijini.
Kolero alikuwa kwenye himaya ya Chifu Hegga wa Kolero, ambaye alikuwa na makazi yake kijiji cha Lubasazi. ( Kijiji cha Lubasazi kilitokana na kugawanywa kwa kijiji cha Kolero)
Mzimu wa Kolero ulihudumia jamii yake kupitia kwa mtoa huduma ( Kuhani Mkuu) aliyeitwa Bibi.
Bibi alikuwa binadamu (mtumishi) aliyekuwa anahudumia jamii hiyo kwa maelekezo ya Kolero mwenyewe.
Waluguru na jamii zao, Wazaramo, Wakutu, Wakwere, Wakami nk, walifika mahali hapo kufanya ibada.
Walienda kuomba, maombi binafsi na pia maombi kwa jamii zao.
Bibi ambaye ndiye aliyekuwa msemaji wa Kolero aliteuliwa na Kolero mwenyewe kutoka kwenye maeneo yake ya kiutawala.
Bibi aliteuliwa vipi, aliishije, aliishi wapi?
Tukutane kwenye uzi maalum unaohusu Mzimu wa Kolero ambao nitauleta hapa Inshaallah tukijaaliwa.