JWTZ yakabidhiwa majengo Chuo Kikuu cha Ulinzi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limekabidhiwa msaada wa majengo ya Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Taifa na Serikali ya China.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Dar es Salaam jana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi alisema chuo hicho kitakuwa cha kwanza nchini na kitatoa mafunzo na kozi zilizoegemea zaidi katika ulinzi na usalama.

“Chuo hiki cha kihistoria kitakuwa cha pili Afrika Mashariki kwa kuwa Nairobi kulikuwa na chuo pekee cha ulinzi na hapa Tanzania ilitulazimu kuwapeleka nje maofisa wetu kupata
mafunzo jambo ambalo sasa limepatiwa ufumbuzi,” alisema Mwinyi.

Alisema ujenzi wa chuo hicho ulikamilika Desemba 30, mwaka jana na ulifadhiliwa na Serikali ya China kupitia Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo kwa gharama ya dola za Marekani milioni tatu na Serikali ilichangia dola milioni moja.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange alisema mafunzo katika
chuo hicho yanataanza Septemba mwaka huu kwa wanafunzi 20 wa ngazi za ukanali na kuendelea lakini pia watakuwamo watumishi wa umma hasa wakurugenzi.

Alisema lengo la kuanzishwa kwa chuo hicho ni kuwakutanisha pamoja maofisa wa majeshi mbalimbali yakiwamo ya nje ya nchi, ili wabadilishane ujuzi na uzoefu katika masuala ya ulinzi na usalama.

Jenerali Mwamunyange alisema lengo lingine ni kuwapatia maofisa hao na wale wa umma uelewa kuhusu ulinzi na usalama hasa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na namna ambavyo
jeshi linawajibika na mipaka yake.

Naye Balozi wa China nchini, Liu Xinsheng alisema msaada huo ni sehemu ya misaada mingi
inayotolewa na nchi yake nchini kutokana na urafiki na ukaribu baina ya nchi hizo wa siku nyingi.

“Natumaini tutazidi kushirikiana na sisi tunatoa na tutaendelea kutoa misaada kwa Watanzania.”

HabariLeo | JWTZ yakabidhiwa majengo Chuo Kikuu cha Ulinzi
 
Nimeona hicho kinachitwa chuo cha ulinzi kwenye tv na kugundua ni majengo macheche sana. Nimebaki kujiuiza hivi kweli serikali haikuweza kujenga yenyewe hicho chuo hadi ikaomba msaada toka china? Au viongozi wetu wamekuwa tegemezi hadi wanaomba vitu vidogo namna hii. Kama tusipoangalia kuna siku tutaomba hata kiberiti china!
 
Back
Top Bottom