Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Kwa mara nyingi sana tumeandika humu kuhusu Uongozi wa CCM unavyoivunja na kuidharau Katiba yetu ila kila siku mmekuwa kimya.
Wameweka bungeni wabunge wasio na vyama baada ya kufukuzwa uanachama wao Chadema kinyume kabisa na Katiba na wakawalipa mamilioni ya fedha ya kodi za Wananchi.
Wamekamata, kuwaua, kuwaweka magerezani, kuwateka na kuwafira watu waliotekeleza uhuru wao wa kikatiba kutoa maoni kuhusu mwenendo wa nchi.
Wameyafunga makanisa na kuwazuia watu kutekeleza na kufaidi haki yao ya Kikatiba ya uhuru wa kuabudu.
Wamewakamata na kuzuia wasisafiri watu waliokuwa wanasafiri na kuwazuia kufaidi uhuru wao wa kikatiba wa kuenda popote wanapotaka
Sio hivyo tu saivi wanatoa rushwa waziwazi. Wananunua pikipiki na baiskeli na kuzigawa waziwazi kweupe kabisa kwa Wananchi ili waungwe mkono kwenye chaguzi. Rushwa za wazi kinyume na Sheria za Nchi.
Pamoja na yote haya nyie wenye kiapo cha kwanza cha kuilinda Katiba mmekaa tu hamfanyi lolote.
Sasaivi wameanza hadi wana CCM kulalamika kuwa Katiba inavunjwa. Sasa tuelezeni, inakuwaje Katiba mnayoilinda inavunjwa waziwazi na nyie mkiwepo?
Kwa nini hamchukui hatua?