JWTZ kutumwa tena DRC, Rais wa DRC asema kikosi cha Afrika mashariki kinashirikiana na M23 kuimaliza DRC

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Rais wa congo yuko mjini Gaborone kwa ziara ya kikazi na leo amesema kikosi cha Afrika mashariki kilichopelekwa nchini mwake hakijafanya lolote la maana na kimeanza kushirikiana na waasi wa M23 na ameziomba nchi za SADC zisaidie.

Mh Rais Samia Suluhu Hassan yupo mjini Windhoek na ameombwa Tanzania kuwa kiongozi wa kikosi kitakacho tumwa DRC hivi karibuni kupambana na waasi wa M23.

Itakumbukwa kuwa kikosi cha SADC kikiongozwa na Tanzania kiliwahi kuwafurahisha waasi wa M23 miaka ya 2010-2014 likishirikiana na wale wa Malawi na South Africa.

My take: kumbe wale wakora wa KDF wako kushirikiana na waasi hii ni hatari sana kwa walinda amani kushirikiana na wauwaji

chanzo RFI

USSR

=======
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amelishtumu jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutofanya vya kutosha kudhibiti utovu wa usalama Mashariki mwa nchi yake.

Tshisekedi ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Botswana na kudai kuwa kikosi hicho kinashirikiana na waasi wa M 23 na huenda kikaondoka nchini mwake kufikia mwisho wa mwezi Juni.
“Kazi ambayo kikosi hiki kilipewa haijatekelezwa kabisa, leo tumeona katika baadhi ya maeneo ushirikiano kati ya kikosi cha jumuiya na waasi wa M23 kinyume na ilivyopangwa kwenye makubaliano.“ alisema rais Felix Tshisekedi

EM Sound - Rais wa DRC Felix Tshisekedi amekosoa utendakazi wa kikosi cha EAC mashariki mwa nchi yake
Kauli yake inakuja siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya SADC nchini Namibia, ambako jumuiya hiyo imesema itatuma vikosi vyake Mashariki mwa DRC.

Matamshi yake pia yanakuja baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kamanda wa kikosi hicho nchini DRC Jenerali Jeff Nyagah katika kile kilichodaiwa ni kutokuwepo kwa maelewano na uongozi wa nchi hiyo ambao pia ulikosoa utendakazi wake.

Meja generali Jeff Nyagah, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya EACRF nchini DRC © EACRF Aidha mkuu huyo wa DRC alisema kuwa muda wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki utakapofika tamati mwishoni mwa mwezi Juni watafanya tathmini kuona iwapo kikosi hicho kitakuwa kimefanya kazi yake na baadae watafanya maamuzi kuona namna watakavyolinda nchi yao ya Kongo.

Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC AP - Ben Curtis
Kando na rais Tshisekedi kukosoa jukumu na uwezo wa kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, raia nchini humo pia nao wamekuwa na kauli sawa na kiongozi wakituhumu wanajeshi hao kwa kukosa kutekeleza walivyotarajiwa kufanya.

Licha ya uwepo wa vikosi hivyo katika baadhi ya maeneo yanayodhibitiwa na makundi yenye silaha ikiwemo M23, mashambulio dhidi ya raia yamekuwa yakiendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo ya mashariki ya DRC.

Waasi wa M23 wanatuhumiwa kwa kuhangaisha usalama wa raia mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa

Japokuwa wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kukosa kuwakabili waasi, baadhi ya raia wameeleza kuwa wamerejea katika makazi yao ya zamani baada ya M23 kuondoka na kupeana sehemu kwa jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nchi za SADC zinajumuisha Afrika Kusini, Angola, Tanzania, Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na DRC.

Screenshot_20230510-092714.jpg
 
Wakenya waliopelekwa sio wanajeshi wa maana walienda tu. Kula dola za safari za nje

Jeshi gani ambalo Generali wake anakimbia vita?

Generali kiongozi wa vikosi kutoka Kenya kakimbia vita eti anaogopa kuuawa.Kichekesho vita alifikiri na ngoma ya mdundiko

Kenya hakuna jeshi walipeleka tu watoto wa vigogo na ndugu zao

Tanzania ikienda vitani haina utani ikiingia mahali lazima matokeo yaonekane
 
Tanzania iliwahi kuwa kiongozi wa kikosi cha SADC kilicho tumwa DRC mwaka 2010-214 kupambana na waasi wa M23.
Jeshi letu lilijua kumfurahisha na kumtokomeza kabisa M23, hali hii ilipelekea PK kuchukizwa na ghafla akaanza maneno ya chokochoko kwa JK
 
binafsi naungana na rais felix, EACRF/KDF warudi tu kwao
 
Wakenya waliopelekwa sio wanajeshi wa maana walienda tu. Kula dola za safari za nje

Jeshi gani ambalo Generali wake anakimbia vita?

Generali kiongozi wa vikosi kutoka Kenya kakimbia vita eti anaogopa kuuawa.Kichekesho vita alifikiri na ngoma ya mdundiko

Kenya hakuna jeshi walipeleka tu watoto wa vigogo na ndugu zao

Tanzania ikienda vitani haina utani ikiingia mahali lazima matokeo yaonekane
Majenerali wa Kenya ni kama Majenerali ya Urusi tu.
 
Kabisa katika eneo lisilotaka upendeleo kuanzia ajira au kupanda vyeo ni jeshini

Kule hakutaki mchezo

Vita ikiwaka kama mtu hayuko fit lazima atunguliwe na risasi vitani awe general au yeyote

General hilo la Kenya ndio wale wa kupanda mivyeo kienyeji vita hii linakimbia linaachia Askari wasio na vyeo na wa chini wapambane lenyewe linatoroka vita

Sipati picha kama angekuwa General ali wa JWTZ aseme sitaki kuendelea kuendesha vita najiuzuru nawindwa kuuawa

Kitu ambacho kingemkuta hata Askari wadoho wangemtwanga risasi kuwa kwa hiyo unatuachia sisi Askari wadogo? Wangemuua angerudi kwenye jeneza kuwa kauawa na adui vitani na angezikwa kishujaa siri inabaki jeshini

Askari wa Kenya wajinga sana Generali anakimbiaje kuongoza vita?

Hicho kitu JWTZ hakiwezekani

Huyo Generali wa Kenya angekuwa wa JWTZ asingethubutu hilo angerudi nchini maiti
 
Kabisa katika eneo lisilotaka upendeleo kuanzia ajira au kupanda vyeo ni jeshini

Kule hakutaki mchezo

Vita ikiwaka kama mtu hayuko fit lazima atunguliwe na risasi vitani awe general au yeyote

General hilo la Kenya ndio wale wa kupanda mivyeo kienyeji vita hii linakimbia linaachia Askari wasio ba vyeo na wa chini wapambane lenyewe linatoroka vita

Sipati picha kama angekuwa General ali wa JWTZ aseme sitaki kuendelea kuendesha vita najiuzuru nawindwa kuuawa

Kitu ambacho kingemkuta hata Askari wadoho wangemtwanga risasi kuwa kwa hiyo unatuachia sisi Askari wadogo? Wangemuua angerudi kwenye jeneza kuwa kauawa na adui vitani na angezikwa kishujaa siri inabaki jeshini

Askari wa Kenya wajinga sana Generali anakimbiaje kuongoza vita?

Hicho kitu JWTZ hakiwezekani
Huyo jenerali ndiye aliyekuwa anashirikiana na m23, kaona maji yamemfika shingoni kajiuzuru.
 
Back
Top Bottom