Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli


mkuu... kwenye red hapo ni kuuingilia uhuru wa mahakama kati ya mihimili hii miwili.... sahihi ni kwamba serikali inaweza ikaweka pingamizi ili hukumu isisajiliwe
 
Collective Responsibility italisumbua sana Baraza la Mawaziri!
 


Ama kweli Tanzania mambo yameiva. Jamani wenzetu mnaopiga kura kwa ccm hali mmefunga macho hebu yafumbueni macho yenu. Ikiwa hata mawaziri wanashindwa kuvumilia na kulazimika kupingamana na dhamira ya wazi ya mkubwa wao inakuambia nini? Ina maana moja tu. Uonzo wa ccm umefikia mahali ambapo umeanza kuinukia yenyewe. Ukiona mtu anaonea kinyaa sura yake mwenyewe ujue ama ni mwendawazimu au uchafu wake umevuka mpaka.
 

Soma vizuri hukumu, mkataba ni baina ya Dowans na Tanesco. ICC huwezi kukiuka hukumu yao na nchi ikikataa kulipa kitachofatia ni kutolewa kwenye uanachama wa ICC, sasa sijui hapo biashara zako utafanya na nani kwani nchi nyingi na bidhaa za biashara kubwa lazima ziidhinishwe na Chemba za biashara. Hapo ndio panakuwa patamu. Hili ni pigo kubwa kwa waTanzania.

Nilisema na ninasema tena, aliyesababisha hili ni yule aliyekurupuka na kuvunja mkataba halali na si yule aliyeweka mkataba.
 
come rain ..come sun, go east.. go west.... Zomba wewe sio Mtanganyika

LAT, Zomba ni Mtanzania tatizo lake he is realist wakati wengi humu ni ma populist wanafuata public opinion. Mimi ni kama Zomba, kwa hukumu ya ICC, tumeshikwa pabaya na hatuna pa kutokea and that is a fact!.

Pasco you missed my point.... i stand to my point Zomba sio Mtanganyika i dont care Zomba preaches what... what i know zomba is a hate preacher
 
Pasco you missed my point.... i stand to my point Zomba sio Mtanganyika i dont care Zomba preaches what... what i know zomba is a hate preacher

Nimezaliwa Tanganyika, jee wewe umezaliwa Tanganyika au Tanzania? Hisabu miaka yako halafu nijibu. Kwa sasa si Mtanganyika, ni mTanzania hakuna nchi duniani kwa sasa inayoitwa Tanganyika, ilikuwepo na ndipo nilipotokea mimi, Jee, wewe! Patamu hapo.
 
Ni zaidi ya mwezi mzima tunaendelea kulumbana kuhusu hukumu ya shauri la Dowans ... ninachoshangaa na kujiuliza, je, ni kwanini hao wenye Kampuni hawaendi kusajiri hukumu hiyo Mahakama Kuu kama jinsi inavyotakiwa?

Je, wanapima upepo kwanza?

Dowans inachimba kaburi la CCM ... soon tutalamba pilau ya mazishi.
 
Nimezaliwa Tanganyika, jee wewe umezaliwa Tanganyika au Tanzania? Hisabu miaka yako halafu nijibu. Kwa sasa si Mtanganyika, ni mTanzania hakuna nchi duniani kwa sasa inayoitwa Tanganyika, ilikuwepo na ndipo nilipotokea mimi, Jee, wewe! Patamu hapo.

Hapa kwenye red umeshanipa jibu wewe ni nani..... nimemaliza
 

Maswali matamu sana haya!
 
unatafutwa na madokta wa mirembe, ati ulitoroka kabla hujamaliza tiba @#%x*??!#$
 
Kwa ufupi ni kuwa endapo Dowans watalipwa kama ilivyoamuriwa na serikali ya JK; na wakalipwa na ikajulikana wamelipwa fedha hizo basi Sitta na Mwakyembe watapaswa kujiuzulu nafasi zao katika Baraza la Mawaziri mara moja. It is as simple as that.
 
wewe zombe

mbona umekubali kununuliwa kwa bei ndogo kiasi hicho kutetea kila ovu la serikali huoni aibu?

Hakuna alininunuwa ila kama hatuna ukweli kwenye nyoyo zetu hatutoweza kuendelea kwa kujidanganya, lazima tuwe realists na kutazama ukweli uko wapi.

Kwa hili la Dowans ukweli ni kwamba, Dowans wamefanya kazi waliyokubaliana na Tanesco na piga uwa utawalipa tu, kama huwalipi, hutatuwi tatizo itazidisha. Hakuna kampuni duniani itaingia tena mkataba na wewe, kwani inajuwa itakuwa hailipwi. Na hiyo itashinikizwa na ICC, utakuwa kwenye cold list.

Ukiyajuwa hayo, utaona, bora ulipe kuliko kujitenegezea matatizo yatakayo kugharimu kuliko haya.

Sasa wanaopiga debe Dowans isilipwe ndio hao waliopiga debe mkataba uvunjwe. Matokeo ndio haya. Na kila mtapodhani kutolipa ni ushindi, mjuwe mnajidanganyan mnajiongezea matatizo.

And we dare say we are "great thinkers", mashudu.
 

Pasco pamoja na uelewa wangu mdogo wa sheria lakini nnakumbuka vizuri kipengele kinachosema hamuwezi kukubaliana kuvunja sheria. Hii maana yake nini? Nni kwamba mfano kima cha chini cha mshahara ni Tshs 90,000.00 Lakini mimi kwa shida zangu tukakubaliana na kusainishana kulipwa Tshs 50,000.00 Halafu say baada ya miaka 5 nikaibuka kukushtaki kunipunja mshahara hakuna mahakama itakayoamuru eti sina kesi kwa sababu tulisainishana. Kifupi ni kwamba mkataba wetu ulikuwa illegal.

Tuje kwenye Dowans, ukiisoma vizuri hoja ya Mwakyembe, objectively na bila ushabiki utagundua kwamba mkataba kati ya Tanesco na Dowans ulikuwa illegal, simply kwa sababu Dowans ni kampuni ya kitapeli na hilo lilithibitishwa na kamati ya bunge yeye akiwa mwenyekiti. Sasa sijaelewa hapo upopulist uko wapi. Please nieleweshe.
 

Given that what you have writen is true, and I believe it's true, Serikali ikiwalipa mafisadi papa wahusika kupitia kampuni hii hewa, bila ridhaa ya bunge, wananchi tutaipindua nchi yetu na kufanya alichokifanya Jerry Rawlings kule Ghana (aliwaua mafisadi wote).

Watanzania tumechoka na tunasema sasa basi!
 
katika sheria za biashara mmliki wa biashara na biashara ni vitu viwili tofauti hivyo dowans inaweza kuishtaki serikali endapo ni kampuni halali ila kwa kuwa sio halali haipaswi kwenda kuomba fidia kwani mkataba ule ni void
 
Sasa wanaopiga debe Dowans isilipwe ndio hao waliopiga debe mkataba uvunjwe. Matokeo ndio haya. Na kila mtapodhani kutolipa ni ushindi, mjuwe mnajidanganyan mnajiongezea matatizo.

Mkuu huu ni upotoshaji makusudi kabisa nnachokumbuka kilichokuwa kikipingwa ni ununuzi wa mitambo ya Dowans na si masuala ya kuvunja mkataba. Yaani inakuwa kama haya mambo yalitokea mwaka 60, wakati ni juzi juzi tu. Enywayz unaweza kuja na nukuuya gazeti lolote likiwa na taarifa ya Sitta au Mwakyembe kusisitiza kuvunja mkataba kati ya Tanesco na Dowans?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…