CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 853
Justin Kalikawe, ni moja ya waasisi wa muziki wa reggae ya Kiswahili. Na moja ya wasanii wa muziki wa Kiswahili waliosumbua sana mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Justin Kalikawe, alitamba zaidi na nyimbo kama vile 'Roho ya Korosho' 'Ningekuwa na Mabawa' 'Wamachinga' 'Panapofuka Moshi' 'Mv-Bukoba' 'Utaratibu Wetu' na 'Nafurahi na Wenzangu'
Nyumba ya milele ya Justin Kalikawe, kwao Bukoba.
Justin Kalikawe kwa pamoja na Sugu, wakilishambulia jukwaa.
Pumzika kwa amani Justin Kalikawe
======
Alizaliwa tarehe 28.08 1967 Kitendaguro nje kidogo ya mji wa Bukoba akiwa mtoto wa 7 kuzaliwa kati ya 8 wa familia yao na alipata elimu yake ya msingi darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kibeta mwaka 1974-1977 na kuendelea darasa la tano hadi la saba katika shule ya msingi Muhimbili jijini Dar-es-salaam alikohitimu mwaka 1980. Mwaka 1981 alichaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari Tambaza ambako alihitimu kidato cha nne mwaka 1984 na kubahatika kuwa mmoja kati ya vijana 4 waliochaguliwa kujiunga kufanya kazi katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha TIPER cha jijini DSM, kazi aliyoianza mwaka 1985 kabla ya kuiacha kwa hiari yake mwaka 1986 na kujitosa rasmi katika fani ya muziki.
Mwanamuziki huyo ambaye alikwishatoa albamu 8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae, amekuwa kielelezo kizuri cha muziki na utamaduni wa mkoa wa Kagera kwani baadhi ya albamu zake aliziimba katika lugha ya kihaya hali iliyomfanya ajikusanyie mashabiki wengi katika ukanda unaozunguka Ziwa Viktoria, na wakati mauti yakimkuta alikuwa katika maandalizi ya kuzindua albamu yake mpya aliyoirekodi hivi karibuni.
Justine alifariki ghafla mwezi wa nane mwaka 2003 katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba miezi michache baada ya kurejea kutoka ziara ya kimuziki nchini Denmark. Mpaka mauti yanamkuta alikuwa ndiye msanii mwenye albamu nyingi zaidi za Reggae nchini Tanzania (8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae).
Justine aliyelelewa na mama yake Ephrazia Kashebo (71) baada ya baba yake mzazi kufariki akiwa na umri wa miaka (1971) ameacha mke Georgia na watoto wawili wa kike Abayo (7) na niwe(4) na alizikwa nyumbani kwake Kitengule Alhamisi saa 10 jioni kwa taratibu za madhehebu ya Orthodox.
Kifo chake ni pigo jingine katika sanaa ya muziki hapa nchini na ndani ya familia yao baada ya kaka yake aliyekuwa mpiga disko mashuhuri hapa nchini Dj Kalikali aliyefariki mwaka 1991.
Atakumbukwa kama mtetezi wa wanyonge na mpigania haki, amani na utulivu katika jamii, na msanii aliyekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya UKIMWI na zaidi atakumbukwa kwa vibao vyake kama Roho ya Korosho, Wamachinga, Watu, Maisha na vingine vingi vilivyotamba.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU JUSTINE KALIKAWE MAHALA PEMA
Moja ya kazi za Justine Kalikawe nilizokuwa nazipenda (na bado nazipenda) ni ile aliyoiimba kwa lugha na midundo ya nyumbani Bukoba.
Wimbo unaitwa NOIJUKA ambao unazungumzia maisha ya utoto (ama niseme ya zamani) na namna ambavyo kama waHaya tuliishi kabla ya kuingia kwa "u-sasa" ulioondoa utamaduni wetu
Ni MAISHA YETU YA KIJIJINIIIIIIIIII
"Ego ninyijuka amakir'Ago"