Justin Nyari ashikiliwa na polisi, ahojiwa

Msee Lekasio

Member
Mar 25, 2010
73
8
Nduku sanguni lidhe jambasi bado linatesa!!! Hii habari ni ya gaseti la mwananji

JESHI la PoIisi mkoani Arusha linamshikilia mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani hapa, Justin Nyari kwa tuhuma za wizi wa madini ya Tanzanite pamoja na mamilioni ya fedha za kigeni.

Taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha, Matei Basilio zinasema kuwa Nyari alikuwa akisakwa na polisi tangu juzi na kukamatwa jana na kwamba mpaka saa 8:00 mchana Nyari alikuwa akihojiwa.

Kamanda Matei alisema kuwa wanamshikilia mfanyabiashara huyo na kumuhoji kutokana na tukio lililofanyika mapema mwezi Aprili mwaka huu wakati madini yenye thamani ya Sh36 milioni yalipoibwa pamoja na dola 42,000 za Kimarekani (sawa na Sh54.6 milioni za Kitanzania).

Inadaiwa kuwa fedha na madini ziliporwa kutoka kampuni moja inayojishughulisha na ununuzi na uuzaji wa madini aina ya Tanzanite iliyo mjini hapa na wahusika hawakuweza kufahamika kwa wakati huo.

Jeshi hilo lilidaiwa kuwa tangu kutokea kwa wizi huo, upelelezi umekuwa ukifanyika na watu watano walikamatwa na kuhojiwa na kwamba baadaye ilibainika kuwepo umuhimu wa kumuhoji mfanyabiashara huyo.

Kamanda Matei alisema kuwa ni kweli jeshi hilo lilipata taarifa juu ya mfanyabiashara huyo kuhusishwa na tuhuma hizo hivyo walimtafuta na kumpata na baadaye kumuhoji ili kujua kama kuna kosa la kujibu.

"Ni kweli yupo hapa... muda huu anahojiwa na mkuu wa upelelezi na suala la kuendelea kumshikilia ama kumwachia litategemea na uzito wa tuhuma zinazomkabili," alisema Kamanda Matei.

Mfanyabiashara huyo amekumbwa na tukio hilo wakati akitajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotaka kuwania kiti cha udiwani wa Kata ya Mererani mkoani Manyara kwa tiketi ya CCM.
 
Huyu ni jambazi na anajulikana kikwete alipoingia madarakani alimwambia aache ujambazi kwa sababu alikuwa anashirikiana na Mahita kwa hiyo ili isionekane kwamba serikaliinawajua majambazi aliambiwa aache.

Ni aibu sana.
 
Huyu ni jambazi na anajulikana kikwete alipoingia madarakani alimwambia aache ujambazi kwa sababu alikuwa anashirikiana na Mahita kwa hiyo ili isionekane kwamba serikaliinawajua majambazi aliambiwa aache. Ni aibu sana.

Na hii skendo huenda ikayeyuka tena kama barafu............
 
Huyo jamaa ni untouchable mmesahau hata yule mpambe wake 'Banjoo' aliachiwa kisa kulikuwa hakuna ushahidi wa kujitosheleza.Jama baada ya kufanya tukio kwa kuiba MAWE kwenye sefu,baada ya kuishoot na pistol at close range.Mna habri alikuwa Dodoma jana Na je alifuata nini?
 
Huyu jamaa alisababisha Kamanda Kombe asipandishwe cheo kwasababu alishindwa kumlinda.Kuna mambo mengi yamejificha nyuma yake ambayo mwananchi wa kawaida akiyajua atawashangaa sana watawala wetu.Ilikuwa ikijulikana wazi Nyari angeshinda rufaa yake iwapo Muungwana angeshinda kiti cha urais.

Huyo jamaa ni untouchable mmesahau hata yule mpambe wake 'Banjoo' aliachiwa kisa kulikuwa hakuna ushahidi wa kujitosheleza.Jama baada ya kufanya tukio kwa kuiba MAWE kwenye sefu,baada ya kuishoot na pistol at close range.Mna habri alikuwa Dodoma jana Na je alifuata nini?

lakini alisota sota rumande, na kale ka mwili cjui sasa hivi anajishughulisha na nini, nikiwa arusha hiyo group nilikuwa naifahamu, nilidhani baada ya ile purukushani walishaacha haya mambo? na Yuegen nae cjui anajishughulisha na nini, arusha yenyewe ndogo wakifanya leo kesho habari zimesambaa town...sasa akigombea huo udiwani si ndio balaa yena, ndio mana anaenda kugombea huko kwa wanzake wanao subiri "kuishi" angegombea hapo town cdhani kama angepata huyu...kazi ipo oct.
 
kweli wewe wa kumunyumba....Eugene siku hizi yupo Dar anakula pesa ya serikali kwa kuwa karibu na dadae (dereva wake).... si unajua dada yake ni waziri (namuhifadhi) aliona atakula shaba (kwa kula wake za watu) akaona akipe...
 
Nakubaliana na wewe kabisa!!!! Kweli mwenye kazi yake haachi hata siku moja. Baada ya ile kasheshe aliyoipata bado tu anaendelea na tabia yake ile ile? Ama kweli hii ni hasara kubwa.
 
Nakubaliana na wewe kabisa!!!! Kweli mwenye kazi yake haachi hata siku moja. Baada ya ile kasheshe aliyoipata bado tu anaendelea na tabia yake ile ile? Ama kweli hii ni hasara kubwa.

Huyu jamaa hapa Arusha kidha mtu anamjua ni jambasi mkubwa. Kinachomlinda ni hiso noti sake...
 
Anatoka msiwe na wasiwasi ni kwa muda tu ukiona kakamatwa ujue wakuu wa polisi wameishiwa wanataka pesa zake hiyo iko known
 
kweli wewe wa kumunyumba....Eugene siku hizi yupo Dar anakula pesa ya serikali kwa kuwa karibu na dadae (dereva wake).... si unajua dada yake ni waziri (namuhifadhi) aliona atakula shaba (kwa kula wake za watu) akaona akipe...

kunyumba kabisa Preta, Yuegen alikuwa bfrd wa frnd wangu, nilishawaona mara nyingi na huyo dada yake, afadhali ameokoa jahazi mana alikuwa anaelekea pabaya, bado handsome? nawafahamu sana hawa majamaa....na Banjoo sasa hivi anajishughulisha na nini na kale kamwili kapata pata hata nyama jamani.
 
Anatoka msiwe na wasiwasi ni kwa muda tu ukiona kakamatwa ujue wakuu wa polisi wameishiwa wanataka pesa zake hiyo iko known

hakuna polisi anatakapesa yake huyo mtu! Alilitukana jeshi la poilisi kwa kuwaambia "iongei na mbwa naongea na mwenye mbwa"
 
Back
Top Bottom