Luca Paguro
JF-Expert Member
- Mar 26, 2023
- 476
- 1,060
Imagine unaishi kwenye nchi X ambayo maji yanaweza kukatika hata siku 7 bila sababu za msingi
Na hapo nchi X ina mito mingi, maziwa mengi na bahari ipo sehemu kubwa tu, na ukichimba chini maji yapo ya kutosha lakini wananchi wake wanateseka na shida ya maji kuanzia wanazaliwa hadi wanakufa, na kinakuja kizazi kingine bado wanateseka na maji vilevile
Miji na vijiji vya nchi X barabara zake zina mashimo, hazipo maintained zimejaa michanga. Na nchi X haina miji mingi ya maana licha ya kuwa na watu wengi. Jiji lenye hadhi ya kinataifa ni moja tu kwenye nchi X tena bado jiji hilo licha ya kupendelewa kila kukicha na serikali bado lina matatizo chungu nzima
Imeichukua nchi X zaidi ya miaka 60 kufikia uchumi wa kati wa chini (low middle income) na bado vijijini shule hazina madarasa ya kutosha, watu masikini, maeneo mengine umeme ni shida lakini wanaoiongoza nchi hawajui hata kama hivyo vijiji vinaexist na vina watu wanahitaji hudumu, wao wameshajichagulia maeneo kadhaa tu wanaoyapenda ya kuyapatia maendeleo
Polisi wa nchi X wanapenda ubabe na kutishia raia ili waogopeke. Raia ni masikini na bado wanakandamizwa. Kwenye nchi X polisi wanaweza kujiamulia tu kukamata raia, wakampiga na kumuua na wasifanywe chochote. Mbaya zaidi kuna raia wachache kwenye nchi X wamelipwa kutetea mambo machafu
Kwenye nchi X elimu bado ni duni, na wala hakuna demokrasia. Ukikosoa anachokifanya kiongozi wa nchi wewe ni muasi na adui wa taifa. Ili uwe mzalendo unapaswa kumsifia kiongozi wa nchi nonstop, na kukaa kimya pale kiongozi huyo anapokosea. Ukifanya hivyo wewe ndio mzalendo wa nchi X
Jeshi la wananchi wa nchi X linalinda maslahi ya viongozi vya chama tawala badala ya kupigania wananchi, ila usishangae sana. Kama jeshi lenyewe kupata nafasi za kujiunga tu ni mpaka uwe na connection, unategemea kwamba kutakuwa na uzalendo hapo? La hasha!
Nchi X bado haina kiwanda hata kimoja cha kutengeneza magari, vifaa vya kielektroniki wala hata majiko ya gesi, au kwa Kiswahili fasaha tunaita meko ya gesi.
Nchi X inategemea kuagiza karibia kila bidhaa, well except chakula maana wangekuwa wanaagiza na chakula ingekuwa ngumu kuwatetea ๐
Kwenye nchi X kuna biashara imekuwa kwa kasi inaitwa uchawa. Hii sitaki kuielezea maana ni aibu hata kuiongelea
Nchi X bhana. Ni nchi masikini isiyo na muelekeo ila viongozi wake wana kiburi, sijui wanajivunia nini hata wakati hata hela za kujenga airport kubwa tu kwenye mji mkuu wake hawana, imebidi wachukue mkopo kutoka nje ndio wajenge airport
Nchi X hata haina mpango wa kujenga viwanda vingi vikubwa, na kwenye nchi X wanalazimisha wananchi kuamini kwamba kutengeneza ajira sio jukumu la serikali. Ila hawaelewi kwamba serikali ndio ina mchango mkubwa kwenye ajira nchini, kwa sababu serikali ndio ina uwezo wa kuandaa mazingira mazuri ya kujiajiri au kualika wawekezaji. Lakini kwenye nchi X hupaswi kabisa kuomba serikali itengeneze ajira. Ukifanya hivyo wewe ni mvivu na sio mzalendo
Kwenye nchi X huruhusiwi kufanya maandamano, na hata kitokee nini kwenye uchaguzi matokeo yanakuwa yameshapangwa kitambo. Kwa hiyo kila mwaka lazima kishinde chama kilekile. Kwenye nchi X hata kama Rais anachukiwa na wananchi kwa kiasi kikubwa bado akienda kwenye uchaguzi anashinda kwa asilimia 98. Unaweza kujiuliza inawezekanaje kudanganya kiasi kikubwa hiki hata kama ni chama tawala, jibu ni simple. Uchaguzi ulofanyika bila main opposition parties. The ruling party in country X is so clever ๐
Lakini population katika nchi X inazidi kupanda, wananchi wanazidi kutengana, uchumi wenyewe mbovu yani ni wa chini sana, ajira hakuna, uwekezaji wa maana hakuna, elimu duni, miundombinu mibovu, na sasahivi wameongezea na mauaji, sasahivi mauaji yamekuwa kwa kawaida sana especially kama ukimkosoa kiongozi wa nchi X, ni kama umejiandalia kaburi lako. Omba Mungu wasikukamate
Nchi X ina future mbovu yenye giza na population inakuwa kwa kasi, kwa hiyo si ajabu miaka ijayo watu wakaanza kuikimbia nchi X kama ilivyo kwa Nigeria, Bangladesh na nchi nyinginezo
Kiufupi nchi X inaharibika, it was once a good country ila kwa sasa imegawanyika na inaendelea kugawanyika kwa kasi. Wananchi hawataki nchi yao iharibike lakini wanaoharibu nchi wana nguvu kuliko wananchi. Kwa hiyo hakuna namna, nchi X inaangamia tu