Jussa: Mchezo umeisha Bunge La Katiba

Jussa: Mchezo umeisha Bunge La Katiba

Hypasonic

Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
14
Reaction score
6
The game is over! -by ISMAIL JUSSA LADHU

Kwa mujibu wa Samuel Sitta alivyotangaza jana, jumla ya Wabunge wote wa Bunge la Katiba = 629
Tanganyika = 419
Zanzibar = 210
2/3 ya 210 = 140
1/3 ya 210 = 70
Kwa hesabu ndogo tu hapo ni kwamba kuinyima Rasimu ya Vijisenti theluthi mbili (2/3) ya Zanzibar zilitakiwa zaidi ya kura 70 (kwa maana zikipatikana 71 itakuwa hapana 2/3 ya Zanzibar).
Sasa naomba tuhesabu pamoja. Miongoni mwa wajumbe 210 wa Bunge la Katiba wanaotoka upande wa Zanzibar:
Wawakilishi wa CUF = 33
Wabunge wa CUF ZNZ = 25
Wabunge wa Chadema ZNZ = 4
Wana UKAWA walotoka ZNZ miongoni mwa 67 = 5
Walopiga wazi HAPANA jana = 7
Wajumbe wawili (Mwanasheria Mkuu wa SMZ Othman Masoud na mjumbe Abdalla Abbas) hawakupiga kura = 2
Jumla = 76
Kuinyima two thirds ya Zanzibar ilitakiwa anything above 70 out of 210.
Hapa pana 76
Kwa lugha rahisi kufahamika ni kwamba Katiba inayopendekezwa haitopita maana haikupata theluthi mbili ya Zanzibar.
Hapa hatujui matokeo ya kura zilizopigwa SIRI. Pia wapo wale waliotajwa kwamba wameorodheshwa watapiga kura wakiwa nje ya Bunge Maalum. Lakini hata ukichukulia zote zitakuwa NDIO basi haziwezi kubadilisha uhalisi na ukweli wa kitakwimu uliopo hapo juu.
Kwa kifupi ni kwamba theluthi mbili ya kura za Wajumbe wote wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar HAIPO.
Sijui wale waliolazimisha kuendelea na Bunge Maalum la Katiba bila ya kupata maridhiano ya pamoja na wakapelekea kutumika mabilioni ya fedha za walipa kodi masikini wa Tanzania huku wakijua kwamba hawatopata theluthi mbili ya kura za Wabunge wote wa Zanzibar sasa watasemaje?

Source: MF
 
Anamaanisha GAME OVER muheshimiwa Sitaunawaona hawa mbona wana tangaza nje ya bunge si walikuwemo humuhumu ,naomba tuwachukulie hatua mara moja ,sina zaidi ila mheshimiwa zile kura za waliokwenda Hija bado hatujazihesabu ila kule kwenye fax karatasi zimekwama ,ni hayo tu Muheshimiwa.
 
Anamaanisha GAME OVER muheshimiwa Sitaunawaona hawa mbona wana tangaza nje ya bunge si walikuwemo humuhumu ,naomba tuwachukulie hatua mara moja ,sina zaidi ila mheshimiwa zile kura za waliokwenda Hija bado hatujazihesabu ila kule kwenye fax karatasi zimekwama ,ni hayo tu Muheshimiwa.

Waliokwenda hija ipo kwenye hiyo idadi. Ili idadi iongezeke labda muwarubuni ukaea wa zanziba. Saivi nasikia mnatishia waliosema hapana
 
hahahahahah safi sana hizi salakasi zao zitzwaponza hawa maccm let go tanganyika back now
 
Mwenyezi Mungu akitaka kukuaibisha anakufanya uitengeneza mwenyewe njia ya kukuaibishia. Hii kura ya wazi CCM ndo waliing'ang'ania mpaka tone la mwisho na sasa ndio imetumika kuwauwa. Naamini, wajumbe wangepiga kura za siri ingewawia rahisi sana kuchakachua (kwa uhuni wanaouonyesha sasa). Sasa hizi ambazo watanzania wote ni mashahidi zimekuwa kaa la moto.
 
hata uwe na mbio vipi huwezi kukiovertake kivuli chako.... kiukweli tanganyika huu ni wakati wake tuuu kujitokeza wamejitahidi kusema watakipita kivuli cha tanganyika lakini ngoma imegoma

Namhurumia 666 anatumika kwenye kiti cha enzi cha mnyama mwenye mapembe
 
Naona wa bara tumeona uzuri wa wa zenji! Wenzetu Hawa ni wana mapinduzi na wapigania haki wa kweli
 
Jamani Zenji wanajitambua tofauti kabisa na Tanganyika ya wadanyika.
 
Niliwahi kufundishwa na padre mmoja hako seminari enzi Hizo kwamba Shetani amepewa uwezo mkubw sana na mwenyezi Mungu wa kutengeneza Chungu kikubwa cha kuweza kumficha mwanadamu na kumpa nafasi ya kujitanua Lakini Mungu alimnyima Shetani uwezo mdogo wa kutengeneza mfuniko.Anapomdanganya mwanadamu kuingia kwenye Chungking hicho amenyimwa uwezo wa kuweka mfuniko.matokeo yake aliyejificha anabaki wazi.yeyote anayechungulia anamkuta yuko wazi.CCM wamechanganywa na shetani kuwa wamejificha hakuna atakayewaona kumbe wanaonekana na leo ndiyo mwisho wa CCM wala siyo 2015.KUpitia katiba hii CCM ndiyo inaondoka.Pole mzee Kinana na kijana wako Nepi
 
Anamaanisha GAME OVER muheshimiwa Sitaunawaona hawa mbona wana tangaza nje ya bunge si walikuwemo humuhumu ,naomba tuwachukulie hatua mara moja ,sina zaidi ila mheshimiwa zile kura za waliokwenda Hija bado hatujazihesabu ila kule kwenye fax karatasi zimekwama ,ni hayo tu Muheshimiwa.

Te!te! Sita asivyo na aibu anaweza kufanya lolote lile.
Mkuu tuwashukuru wazanzibar kwa msimamo wao, huku sisi bado sana hadi akina Komba waishe sio leo.
 
Mungu amempa samuel sitta roho ngumu kama ya farao ili aibu hii imkute na miccm yotee kwa ujumla.
 
ccm vueni c.h.u.p.i zenu xote. kisha mkinge miguu juu kesho ni siku yenu ya kusasambuliwa.
 
Muungano udumu milele,maana ndugu zetu wazanzibari ni wanamapinduzi haswa
 
Tunamshukuru kwa dhati kabisa Mzee 6 na timu vin'gang'anizi yote. Tena salamu zifike kwa mzee wa vijisenti na mama Migiro. bila kumsahau mwanaume muimba taarabu mwenye tumbo kubwa duniani (anajina la kamnyama). Wamefanya kazi nzuri kabisa katika uandishi wao na uendeshaji wao wa bunge la katiba ya ccm.

Sasa tunakuja kwenye mada. Atakaye simama kuwania nafasi ya urais au ubunge kwa tiketi ya chama pendwa anatakiwa asiwe mnafiki. Awe ni yule ambaye amepiga kula ya hapana au hakupiga kula kabisa tofauti na hapo tumeona kwa macho na masikio yetu tumewasikia wote wanaoutaka urais kwa kutuambia wao ni bora kuliko rais wa sasa JK kuwa JK kawazidi sana uwezo na ndio maana wametii hata ambavyo walipaswa kuvipinga kama wanauzalendo wa kweli kabisa.

Wafuatao wote wanautaka urais kwa kupitia kiti cha chama pendwa cha ndio mzee na wamepiga kula za ndio kupitisha katiba ya ccm iwe ya Tanzania pendwa. Kwa sababu hawa ni wazandiki na wanafiki tuanze kuwakataa mapema maana hawana jipya katika kuitakia mema Tanzania tuipendayo sie wazawa.

Samwel J Sita NDIO
Edward N. Lowassa NDIO
January Makamba NDIO
Dr. Hamis Kigwangala NDIO
Bernad Membe NDIO
Dr. Asha R Migiro NDIO
Prof. Anna Tibaijuka NDIO

ongezea wote unaowajua wewe wazandiki wa taifa hili.

Pia wabunge wote waliopiga kura za ndio tukutane majimboni tuwaoneshe kuwa tumewachoka.

Kwa ushauri tu chama cha NDIO bora wamwombe mzee Warioba ndio agombee urais kwa chama chao huyo atapita na watanzania wanaweza kumpigia kura tofauti na hapo ............................................ loading 99.9%
 
Back
Top Bottom