Jumuiya ya madola kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 mwezi huu

Jumuiya ya madola kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 mwezi huu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Jumuiya ya Madola imeipokea na kukubali dhamira ya Serikali ya Tanzania juu ya kupokea na kuwezesha ziara pamoja na kazi za Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Dkt. Lazarus Chakwera ambaye pamoja na msafara wake utachunguza uminywaji wa kidemokrasia na kutofuatwa kwa utawala wa kisheria kufuatia matukio ya kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Hayo yamesemwa baada ya kikao cha 72 cha Kamati Maalum ya Jumuiya ya Madola inayoshughulikia masuala ya demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu miongoni mwa nchi wanachama(CMAG) ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Professa Palamagamba Kabudi alikutana na kamati hiyo na kufanya mazungumzo.

Taarifa ya CMAG iliyotolewa baada ya kikao chake cha Machi 7, 2026 imesema “CMAG pia ilikaribisha dhamira ya Tanzania ya kumpokea na kuwezesha ziara pamoja na kazi za Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu mwezi Machi 2026.”

Disemba 2025 katika mkutano wake wa 71 wa CMAG ulioongozwa na Dkt. Ian Borg Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Malta uliamua kuiweka Tanzania katika ajenda maalum ya kikao cha machi yakizingatiwa masharti manne yaliyotolewa katika kikao kilichoijadili Tanzania Disemba 2025.

Tanzania-election-crackdown-hassan-11172025-1.jpg

Tanzania ilitakiwa kutoa nafasi iliyokamilika bila kikwazo kwa Msafara Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuweza kukutana na wadau wote katika nafasi za mwanzo. Pia kuondolewa kwa vikwazo kwenye uhuru wa kukusanyika na kujieleza, makundi maalum na vyombo vya habari.

Pamoja na hayo masharti mengine ni Kufanyika kwa jukwaa la mashauriano kati ya vyama vya siasa ili kukubaliana mfumo wa pamoja wa hatua za kuendelea mbele kuelekea uchaguzi ujao. Uchukuaji wa hatua za kisheria na kiutawala zilizo wazi ili kuwawajibisha wahusika wa vitendo vya vurugu na athari zake, pamoja na kutoa fidia kwa waathirika pale inapofaa.

Ujumbe huo utakaoongozwa na Dkt. Lazarus Chakwera Rais Mstaafu wa Malawi unatarajiwa kufika nchini mwezi huu wa tatu huku miongoni mwa hadidu za rejea itakazotumia ikiwa ni taarifa ya Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi ambayo imeundwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia Soma: Jumuiya ya Madola (Commonwealth) yasikitishwa na yanayoendelea Tanzania

1772970980811.png

1772971026951.png

Attachments

London
Makao Makuu
Jumuiya ya Madola

Kikao cha 71 CMAG Desemba 2025 Taarifa ya Kuhitimisha ya
1772970804372.jpeg

Jumuiya ya Madola

Muktasari wa Mkutano wa Sabini na Moja wa Kundi la Mawaziri la Jumuiya ya Madola

5 Desemba 2025

1. Kundi la Mawaziri la Jumuiya ya Madola (CMAG) lilifanya mkutano wake wa sabini na moja mnamo Desemba 5, 2025. Mkutano huo wa maalum ulifanyika kwa njia ya mtandao na kuongozwa na
Mheshimiwa Dkt. Ian Borg, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Malta. Mawaziri na wawakilishi kutoka nchi za Antigua na Barbuda, Botswana, Kanada, Grenada, Malaysia, Mauritius, Samoa, na Zambia walihudhuria.

2. Kundi hilo la mawaziri wajumbe lilisisitiza tena umuhimu wa kuzigatiwa makubaliano ya maadili na kanuni za msingi za Jumuiya ya Madola kama ilivyoainishwa katika Mkataba (charter) wa Jumuiya ya Madola.

3. Mawaziri walisisitiza kuunga mkono Ofisi bora ya Katibu Mkuu, utaratibu wa kulinda na kukuza maadili na kanuni za Jumuiya ya Madola.

4. Mawaziri walionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu vitisho vinavyoongezeka dhidi ya demokrasia, utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, haki za binadamu, na nafasi ya kidemokrasia inayokabiliwa na
nchi nyingi ndani ya familia yetu ya Jumuiya ya Madola. Wanachama walithibitisha tena kwamba taasisi za kidemokrasia na miundo ya utawala thabiti, na heshima kwa utawala wa sheria na haki za binadamu, ni muhimu kwa maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi,
usalama na kwa ajili ya kukuza amani.

5. Kundi lilipokea ripoti kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mbunge).

6. Kuhusu suala la Tanzania, Mawaziri walielezea wasiwasi wa pamoja wa Jumuiya ya Madola kuhusu ripoti za uvunjwaji wa maadili na kanuni za msingi za Jumuiya ya Madola, ikiwa ni pamoja na heshima ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, demokrasia, utawala wa sheria, na utawala bora. Wanachama walielezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali iliyoripotiwa kuzorota kabla na baada ya uchaguzi (October 2025).

7. Mawaziri walimpongeza Katibu Mkuu kwa tathmini ya haraka ya hali hiyo na uamuzi wake wa kutoa ushirikiano wa Ofisi zake Bora kupitia uteuzi wa Mjumbe Maalum nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Lazarus Chakwera, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Malawi.

8. Kundi liliamua kwamba Tanzania iwekwe kwenye Ajenda Rasmi ya CMAG kwa mkutano ujao Machi 2026, kwa uamuzi wa CMAG kuhusu Tanzania. Uamuzi wa CMAG utategemea kutimiza masharti, vigezo na kanuni zifuatazo:

a. Kwamba Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu apewe uwezo wa ufikiaji kamili na huru kwa wadau wote husika haraka iwezekanavyo;

b. Kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya uhuru wa kukusanyika na kujieleza, asasi za kiraia na vyombo vya habari;

c. Kufanyika kwa jukwaa la mashauriano kati ya vyama ili kukubaliana kuhusu mfumo wa pamoja kuhusu njia ya kuelekea uchaguzi ujao;

Page 1

d. Utekelezaji wa michakato ya kisheria na kiutawala iliyo wazi ili kuwawajibisha wale wote wahusika wa(violence) vurugu na matokeo yake na kuwalipa fidia waathiriwa, inavyofaa.

9. Kundi limeomba Serikali ya Tanzania impatie Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, kwa ajili ya taarifa ya kikao kijacho cha CMAG, hadidu za rejea za Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa na Serikali . (Iliyo chini ya wenyekiti wa Jaji Chande)

10. Kundi lilimwomba Katibu Mkuu kutoa ripoti kamili kuhusu maendeleo yaliyopatikana kuhusu masharti hayo hapo juu kwa CMAG katika mkutano wake ujao.

11. Mawaziri walimwomba Katibu Mkuu aendelee kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuendelea kuunga mkono kazi yake ya kuwezesha kuimarisha sera zinazoimarisha utawala wa sheria, (ugatuzi wa mihimili) mgawanyo wa madaraka, kuheshimu katiba, na utawala bora kama ilivyoainishwa katika Hati ya Jumuiya ya Madola .

12. Kundi pia liliihimiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata / kupewa usaidizi wote wa kiufundi unaopatikana kutoka Jumuiya ya Madola ili kuongeza amani , utulivu wa kidemokrasia , na utawala bora .

13. Kundi la mawaziri wajumbe lilipokea na kumshukuru Katibu Mkuu kwa ripoti zake kuhusu masuala muhimu kwa CMAG.

14. Ilikubaliwa kwamba mkutano ujao wa CMAG utaitishwa mnamo tarehe 7 Machi 2026 katika Wiki ya maadhimisho ya Jumuiya ya Madola huko London.

Page 2

MWISHO

Imetolewa:

5 Desemba 2025
 
The 72nd Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG) met in London today ahead of the 26th Commonwealth Foreign Affairs Ministers Meeting (CFAMM) and next week’s Commonwealth Day celebrations.

The Group was formed in 1995 to be a custodian of the fundamental political values of the Commonwealth. It is made up of a rotating group of Foreign Ministers from eight countries, drawn from different regions, plus the Foreign Minister of the Commonwealth Chairperson-in-Office, the host of the previous Commonwealth Heads of Government Meeting.

Held on Saturday 7 March, the meeting was chaired by Honourable Dr Ian Borg, Deputy Prime Minister and Minister for Foreign Affairs and Tourism of Malta. Ministers and distinguished representatives from Antigua and Barbuda, Botswana, Canada, Grenada, Malaysia, Mauritius, Samoa and Zambia were also in attendance.

CMAG meetings are convened by the Commonwealth Secretary-General, with the Commonwealth Secretariat providing support
 
1772971308660.jpeg

Concluding Statement of the Seventy-Second Meeting of the
Commonwealth Ministerial Action Group

7 March 2026

1. The Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG) held its Seventy-second meeting on Saturday, 7 March 2026. The meeting was chaired by the Honourable Dr Ian Borg, Deputy Prime Minister and Minister for Foreign Affairs and Tourism
of Malta. Honourable Ministers and distinguished representatives from Antigua and Barbuda, Botswana, Canada, Grenada, Malaysia, Mauritius, Samoa, and
Zambia were in attendance.

2. CMAG reaffirmed its commitment to the fundamental values and principles of
the Commonwealth as enshrined in the Commonwealth Charter – including democracy, rule of law, human rights, separation of powers and freedom of
expression and reiterated the importance of the Commonwealth’s support for
the territorial integrity and sovereignty of all member states.

3. CMAG welcomed the report from the Secretary-General on her Good Offices engagements with member states, a mechanism to protect and promote
Commonwealth values and principles.

4. Ministers expressed deep concern about the growing threats to democracy, the rule of law, judicial independence, human rights, and democratic space. CMAG reaffirmed that resilient democratic institutions and governance structures, and
respect for the rule of law and human rights, are pivotal for sustainable and inclusive economic development, security and for fostering peace.

5. CMAG had a positive exchange with the Minister of Foreign Affairs, Cooperation, Integration and the Diaspora of the Gabonese Republic, Her Excellency, Ms Marie-
Édith Tassyla-Ye-Doumbénény, and commended Gabon on its continued progress on the path of democratic transition. CMAG decided to keep Gabon on its Formal Agenda and encouraged the Secretary-General to offer technical support to the Gabonese Government to further deepen the rule of law, democratic stability,
separation of powers and good governance.

6. CMAG had a productive engagement with Honourable Professor Palamagamba J.
Kabudi, Minister of State (Special Duties) of the United Republic of Tanzania and urged Tanzania to take the necessary steps in support of its stated commitmen

Page 1

to the Commonwealth Charter and its political values. CMAG decided to retain Tanzania on its Formal Agenda and encouraged the Government of Tanzania, to
advance, with the support of the Secretariat, on the areas outlined in CMAG’s Seventy-first Meeting in December 2025. CMAG welcomed Tanzania’s commitment to receive and facilitate the visit and work of the Secretary- General’s Special Envoy in March 2026. CMAG looks forward to a robust assessment from the Special Envoy and in particular on issues raised by CMAG.

7. CMAG also addressed other matters of interest.

8. On Pakistan, CMAG decided that the Secretary-General will continue her Good Offices and engage with Pakistan to ensure the implementation of the
recommendations of the 2024 Commonwealth Observer Group. CMAG will consider a Secretary-General report on Pakistan for a decision at its next meeting.

9. On Uganda, CMAG addressed recent reports on the human rights and political environment in Uganda and decided that Uganda be placed on the Formal Agenda
of CMAG. CMAG decided that the Secretary-General will engage her Good Offices with Uganda. CMAG will consider a report of the Secretary-General at its next
meeting.

10.CMAG applauded the work of the Secretary-General to promote sustainable development, democracy, good governance, stability, and peace in the
Commonwealth Family.

11. It was agreed that the next regular meeting of CMAG will be convened in November 2026 in Antigua and Barbuda.

7 March 2026

Page 2
 
TOKA MAKTABA

Kikao cha 71 CMAG Desemba 2025 Taarifa ya Kuhitimisha ya
1772971421636.jpeg

Jumuiya ya Madola

Muktasari wa Mkutano wa Sabini na Moja wa Kundi la Mawaziri la Jumuiya ya Madola

5 Desemba 2025

1. Kundi la Mawaziri la Jumuiya ya Madola (CMAG) lilifanya mkutano wake wa sabini na moja mnamo Desemba 5, 2025. Mkutano huo wa maalum ulifanyika kwa njia ya mtandao na kuongozwa na
Mheshimiwa Dkt. Ian Borg, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Malta. Mawaziri na wawakilishi kutoka nchi za Antigua na Barbuda, Botswana, Kanada, Grenada, Malaysia, Mauritius, Samoa, na Zambia walihudhuria.

2. Kundi hilo la mawaziri wajumbe lilisisitiza tena umuhimu wa kuzigatiwa makubaliano ya maadili na kanuni za msingi za Jumuiya ya Madola kama ilivyoainishwa katika Mkataba (charter) wa Jumuiya ya Madola.

3. Mawaziri walisisitiza kuunga mkono Ofisi bora ya Katibu Mkuu, utaratibu wa kulinda na kukuza maadili na kanuni za Jumuiya ya Madola.

4. Mawaziri walionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu vitisho vinavyoongezeka dhidi ya demokrasia, utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, haki za binadamu, na nafasi ya kidemokrasia inayokabiliwa na
nchi nyingi ndani ya familia yetu ya Jumuiya ya Madola. Wanachama walithibitisha tena kwamba taasisi za kidemokrasia na miundo ya utawala thabiti, na heshima kwa utawala wa sheria na haki za binadamu, ni muhimu kwa maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi,
usalama na kwa ajili ya kukuza amani.

5. Kundi lilipokea ripoti kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mbunge).

6. Kuhusu suala la Tanzania, Mawaziri walielezea wasiwasi wa pamoja wa Jumuiya ya Madola kuhusu ripoti za uvunjwaji wa maadili na kanuni za msingi za Jumuiya ya Madola, ikiwa ni pamoja na heshima ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, demokrasia, utawala wa sheria, na utawala bora. Wanachama walielezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali iliyoripotiwa kuzorota kabla na baada ya uchaguzi (October 2025).

7. Mawaziri walimpongeza Katibu Mkuu kwa tathmini ya haraka ya hali hiyo na uamuzi wake wa kutoa ushirikiano wa Ofisi zake Bora kupitia uteuzi wa Mjumbe Maalum nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Lazarus Chakwera, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Malawi.

8. Kundi liliamua kwamba Tanzania iwekwe kwenye Ajenda Rasmi ya CMAG kwa mkutano ujao Machi 2026, kwa uamuzi wa CMAG kuhusu Tanzania. Uamuzi wa CMAG utategemea kutimiza masharti, vigezo na kanuni zifuatazo:

a. Kwamba Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu apewe uwezo wa ufikiaji kamili na huru kwa wadau wote husika haraka iwezekanavyo;

b. Kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya uhuru wa kukusanyika na kujieleza, asasi za kiraia na vyombo vya habari;

c. Kufanyika kwa jukwaa la mashauriano kati ya vyama ili kukubaliana kuhusu mfumo wa pamoja kuhusu njia ya kuelekea uchaguzi ujao;

Page 1

d. Utekelezaji wa michakato ya kisheria na kiutawala iliyo wazi ili kuwawajibisha wale wote wahusika wa(violence) vurugu na matokeo yake na kuwalipa fidia waathiriwa, inavyofaa.

9. Kundi limeomba Serikali ya Tanzania impatie Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, kwa ajili ya taarifa ya kikao kijacho cha CMAG, hadidu za rejea za Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa na Serikali . (Iliyo chini ya wenyekiti wa Jaji Chande)

10. Kundi lilimwomba Katibu Mkuu kutoa ripoti kamili kuhusu maendeleo yaliyopatikana kuhusu masharti hayo hapo juu kwa CMAG katika mkutano wake ujao.

11. Mawaziri walimwomba Katibu Mkuu aendelee kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuendelea kuunga mkono kazi yake ya kuwezesha kuimarisha sera zinazoimarisha utawala wa sheria, (ugatuzi wa mihimili) mgawanyo wa madaraka, kuheshimu katiba, na utawala bora kama ilivyoainishwa katika Hati ya Jumuiya ya Madola .

12. Kundi pia liliihimiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata / kupewa usaidizi wote wa kiufundi unaopatikana kutoka Jumuiya ya Madola ili kuongeza amani , utulivu wa kidemokrasia , na utawala bora .

13. Kundi la mawaziri wajumbe lilipokea na kumshukuru Katibu Mkuu kwa ripoti zake kuhusu masuala muhimu kwa CMAG.

14. Ilikubaliwa kwamba mkutano ujao wa CMAG utaitishwa mnamo tarehe 7 Machi 2026 katika Wiki ya maadhimisho ya Jumuiya ya Madola huko London.

Page 2

MWISHO

Imetolewa:

5 Desemba 2025
 
Ni jambo zuri kuona wanapewa nafasi ya uchunguzi na vilevile wapewe access yeyote wanayoihitaji kutoka katika serikali katika uchunguzi wao
 
Wangalau tume hii wengi watakuwa na imani nayo kwenye kutoa ushahidi, na sio ile tume ya kuficha uovu wa serekali chini ya jaji Chande.
 
Kwa upande wangu sioni kama kutakuwa na jipya kwa hii tume. Mfano ikitokea tume hii ikabaini makosa ya Serikali itafanya nini hatma yake?
Huku ni kupoteza pesa na muda tu kwani tume hii nayo haina uwezo wa kuiwajibisha Serikali
 
Pamoja na kwamba hii inaweza kuwa ni hatua na ngazi ya kutafuta uwajibikaji, naona kama Jumuiya ya Madola haina meno ya kutosha kufanya yale ambayo kweli yataleta mabadiliko yanayotamaniwa na wengi. Hawa sanasana watatoa matamko ya kukemea, watasitisha misaada na kukatisha ufadhili wa masomo.

Kwa maoni yangu, CCM wanahitaji wakabiliane na wale walio na meno zaidi, kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ICC pamoja na misimamo ya wazi ya nchi kama Marekani.

Wengine hawa kama Jumuiya ya Madola ni kama CCM wamejipanga kudili nao maana wanajua mambo ya diplomasia yana kubembelezana kwingi na muda unavyozidi kuchelewa ndiyo kule ground wanaset mambo sawa kwa jinsi yanavyoweza kuwasaidia.
 
EMBUTUSAHAUHAAYAMAMBO WATU BADO WANA MAUMIVU JAMAN
 
a. Kwamba Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu apewe uwezo wa ufikiaji kamili na huru kwa wadau wote husika haraka iwezekanavyo;
Hizi tafsiri za maandishi zinazotokana na utumiaji wa Akili Unde/Akili Mnemba zinaharibu sana mtiririko wa taarifa kwa lugha ya Kiswahili.
 
Pamoja na kwamba hii inaweza kuwa ni hatua na ngazi ya kutafuta uwajibikaji, naona kama Jumuiya ya Madola haina meno ya kutosha kufanya yale ambayo kweli yataleta mabadiliko yanayotamaniwa na wengi. Hawa sanasana watatoa matamko ya kukemea, watasitisha misaada na kukatisha ufadhili wa masomo.

Kwa maoni yangu, CCM wanahitaji wakabiliane na wale walio na meno zaidi, kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ICC pamoja na misimamo ya wazi ya nchi kama Marekani.

Wengine hawa kama Jumuiya ya Madola ni kama CCM wamejipanga kudili nao maana wanajua mambo ya diplomasia yana kubembelezana kwingi na muda unavyozidi kuchelewa ndiyo kule ground wanaset mambo sawa kwa jinsi yanavyoweza kuwasaidia.
Ninakubaliana nawe kuhusu hawa Commonwealth. Hawa hawana lolote kwa msaada wa kuleta mabadiliko chanya ndani ya taifa letu. Sana sana ni kutoa lawama zisizoelekezwa popote pa maana; na kazi kubwa itakuwa ni kuwapa bega waovu waliosababisha maovu.

Kuhusu hao wengine uliowataja, Baraza la Usalama, hilo halipo kabisa, kwa nchi kama Tanzania wakati huu. Tanzania imeshuka hadhi sana kati ya mataifa, Hakuna anayeshtushwa na kinachotokea hapa.

ICC inabidi sasa nao wasiwekewe matumaini. Wamekaa kimya mno na swala lenyewe wakisubiri lipowe na watu wasahau. Huko naweza kusema bila ya shaka yoyote nako hakuna mategemeo yoyote.

Marekani? Marekani ya Trump iiwazie Tanzania? Hapo patakuwepo na muujiza maalum, ambao sifikirii kwamba utawezekana.
Hata Samia akiamua kuendelea kuua tena waTanzania kwa sababu zozote zile, hiyo Marekani ya sasa usiweke matumaini juu yake.

Sasa ngoja nirudie kwa mara nyingine tena, ninalojuwa linawezekana kabisa kufanyika na kubadili hali ya Tanzania bila ya wasiwasi kubwa.

Mabadiliko ni lazima tuyatafute sisi wenyewe; raia wa taifa hili.
Tunachotakiwa kuomba msaada juu yake ni kinga tu dhidi ya mitutu ya bunduki tunayoelekezwa wakati tunapodai HAKI zetu.
Hawa watu wa nje wanao uwezo wa kutusaidia kulinda uhai wetu tusidhuriwe wakati tukitafuta HAKI.

Hawa wa nje wanaweza kutusaidia vipi dhidi ya mitutu?
Waiangazie Tanzania macho kwa karibu zaidi. Kila tendo linalofanywa na waovu liwe linamulikwa na wahusika wa moja kwa moja wanaanikwa wazi

Wasitishe misaada inayowawezesha waovu wanaotukandamiza kutuumiza zaidi

Wakitusaidia kwa njia hizo na nyingine nyingi, ninayo hakika waTanzania wenyewe kazi hii ya kuondokana na utawala duni huu tutaifanya haraka na kwa ufanisi zaidi..

Mabadiliko hayo yanayotokana na sisi wenyewe ni ya maana zaidi kwetu na kwa taifa letu kuliko kusubiri tufanyiwe toka nje.
 
Sasa kama hadidu rejea ni tume iliyoundwa na Samia huo ni upuuzi mtupu.
Ndiyo maana sina matumaini na ngonjera hizi.

Hawa tayari wanafanya kazi na serikali haramu, kuisaidia kujiimarisha zaidi kukaa madarakani bila kujali uharamu wake.
Wangalau tume hii wengi watakuwa na imani nayo kwenye kutoa ushahidi, na sio ile tume ya kuficha uovu wa serekali chini ya jaji Chande.
Hakuna nafuu yoyote hapo, mkuu 'Tindo'.
jiridhishe tena kusoma taarifa hiyo iliyotolewa.

Haina matumaini yoyote ya mabadiliko hapa.

Tayari wanazungumzia "uchaguzi ujao"! Kwa maana kwamba hali iliyopo iendelee kama ilivyo.

Sote tunajuwa CCM kuendelea kuwepo hadi uchaguzi ujao maana yake ni nini.

Watuache sisi wenyewe tuyamalize haya.

Wakitaka kuwa na msaada kwetu, kuna njia bora zaidi za kutusaidia ili tuyamalize haya matatizo yetu sisi wenyewe.
 
Wangalau tume hii wengi watakuwa na imani nayo kwenye kutoa ushahidi, na sio ile tume ya kuficha uovu wa serekali chini ya jaji Chande.
Tatizo itafanya kazi na government people. Na hapo kutakuwa na uptoshwaji mkubwa wa kilichotokea.
Haya ni maoni sijajua itafanya kazi vipi independently kwa anaye ju anifahamishe
 
Yaani mauaji yafanyike Oct 29 na wao waje kuchunguza mwezi MARCH😲😲😲, NADHANI HAWAIJUI CCM!
 
Ninakubaliana nawe kuhusu hawa Commonwealth. Hawa hawana lolote kwa msaada wa kuleta mabadiliko chanya ndani ya taifa letu. Sana sana ni kutoa lawama zisizoelekezwa popote pa maana; na kazi kubwa itakuwa ni kuwapa bega waovu waliosababisha maovu.

Kuhusu hao wengine uliowataja, Baraza la Usalama, hilo halipo kabisa, kwa nchi kama Tanzania wakati huu. Tanzania imeshuka hadhi sana kati ya mataifa, Hakuna anayeshtushwa na kinachotokea hapa.

ICC inabidi sasa nao wasiwekewe matumaini. Wamekaa kimya mno na swala lenyewe wakisubiri lipowe na watu wasahau. Huko naweza kusema bila ya shaka yoyote nako hakuna mategemeo yoyote.

Marekani? Marekani ya Trump iiwazie Tanzania? Hapo patakuwepo na muujiza maalum, ambao sifikirii kwamba utawezekana.
Hata Samia akiamua kuendelea kuua tena waTanzania kwa sababu zozote zile, hiyo Marekani ya sasa usiweke matumaini juu yake.

Sasa ngoja nirudie kwa mara nyingine tena, ninalojuwa linawezekana kabisa kufanyika na kubadili hali ya Tanzania bila ya wasiwasi kubwa.

Mabadiliko ni lazima tuyatafute sisi wenyewe; raia wa taifa hili.
Tunachotakiwa kuomba msaada juu yake ni kinga tu dhidi ya mitutu ya bunduki tunayoelekezwa wakati tunapodai HAKI zetu.
Hawa watu wa nje wanao uwezo wa kutusaidia kulinda uhai wetu tusidhuriwe wakati tukitafuta HAKI.

Hawa wa nje wanaweza kutusaidia vipi dhidi ya mitutu?
Waiangazie Tanzania macho kwa karibu zaidi. Kila tendo linalofanywa na waovu liwe linamulikwa na wahusika wa moja kwa moja wanaanikwa wazi

Wasitishe misaada inayowawezesha waovu wanaotukandamiza kutuumiza zaidi

Wakitusaidia kwa njia hizo na nyingine nyingi, ninayo hakika waTanzania wenyewe kazi hii ya kuondokana na utawala duni huu tutaifanya haraka na kwa ufanisi zaidi..

Mabadiliko hayo yanayotokana na sisi wenyewe ni ya maana zaidi kwetu na kwa taifa letu kuliko kusubiri tufanyiwe toka nje.
Ninachosema ni kwamba inahitajika kupata taasisi au nchi ambayo kauli yake itakuwa ni kinga na nguvu ambayo wananchi wataitumia kujitokeza kupambana dhidi ya wahuni wa CCM.

Kauli ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ina nguvu hata ya kisheria kimataifa pale mlengwa anapokaidi. Unaposema "Waiangazie Tanzania macho kwa karibu zaidi", nani unadhani anaweza kufanya hivyo zaidi ya UNSC au Marekani? Tunaona Jumuiya ya Madola, EU, AU, SADC wote wametoa matamko na hata baadhi kusitisha misaada ila haijatosha kuwaamsha wananchi. Ila kupitia kwa azimio la UNSC, hata wananchi wakiamua kupambana wenyewe, hayo macho ya dunia unayosema, kweli yatakuwa yanaiangazia Tanzania na nchi inaweza kuadhibiwa isipofuata maekelezo.

Kwa jinsi ninavyosoma mienendo ya siasa za dunia kwa sasa ni kwamba Marekani tayari amelenga kuikamata Afrika. Anachofanya kwa sasa ni kumdhoofisha kwanza China (kupitia kwa Venezuela na sasa Iran). Wakati ukifika, akija kufanya yake huku Africa, China atakuwa hana jinsi, ataona bora aunge mkono maazimio ya UNSC na ndiyo hapo nguvu itatumika ikiwa na baraka za UN.

Mtanzania bado ni muoga, hajui kujipambania, hana maarifa ya jinsi anavyokandamizwa na hata anapojua uonevu unaomzunguka, anakosa utashi na mbinu sahihi za kupambana. Bila msukumo wa nje tusahau kabisa kuondoka kwa CCM.
 
Back
Top Bottom