Jumuiya ya kimataifa haiyaoni yanayotendeka Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya ya kimataifa haiyaoni yanayotendeka Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima wa Kuku, Nov 15, 2011.

 1. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kwa masikitiko makubwa nashangazwa na ukimya huu wa jumuiya ya kimataifa pamoja na washirika wake wakuu kama Marekani na Uingereza wakinyamazia vitendo vya kihuni vinavyofanywa na serikali ya CCM kwa makusudi ya kuua upinzani ili wajitengenezee mazingira ya kubaki madarakani kiimla.

  Nionavyo ni kuwa wameamua kunyamaza kimya kwa ajili ya shosti wao aliyetayari kuwapa rasilimali za nchi yetu kwa manufaa yake binafsi. Haieleweki nchi nyingine kakitokea kajambo kadogo wanaojiita wakuu wa jumuiya hiyo inayoongozwa na Ban Ki Moon akisaidiwa na Dr. Asha Rose Migiro wakiwa wamenyamaza kimya kabisa hata kutoa comment nyepesi tu ya kukemea. Ina maana gani? Ikifanywa ni ccm ruksa, ikifanywa dhidi ya wasio ccm ni laana.

  Nimegundua kwa siku hizi yafuatayo:
  1. Hakuna maslahi ya nchi kupigiwa kelele -anayepiga kelele anaitwa adui na kuitiwa polisi wa kumdhibiti
  2. Kudhibiti kwa kutumia nguvu kila anayedai haki -kuanzia mikopo ya vyuo vikuu, haki ya kudai Umeya wa Arusha umechakachuliwa, wananchi wa Mwanza Mbeya na Iringa (miji iliyo ngome za upinzani) kuendelea kunyanyaswa na majeshi ya polisi
  3. Vitisho vya wazi kwa maelekezo uvurugaji nchi
  4. wakuu wa mikoa na wilaya kutumiwa kwa maslahi ya chama tawala
  5.Zuio la mikutano ya chama cha demokrasia na maendeleo kwa kisingizio cha Al-shabaab (hawajawahi kutuchokoza, ila mkuu wa nchi ameamua kuingiza chokochoko kwa kisingizio cha Kenya) bila ya kujua ukweli wa siasa za Kenya/Somalia (akidhani suala pale ni ugaidi)
  6. Sasa suala la katiba ambalo linachezewa na wabunge wasio na uchungu na nchi yetu kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
  Kwa hiyo:

  1. Lazima jumuiya hiyo ya kimataifa ijue kuwa Tanzania ni ya watatnzania na tunastahili kufaidi mali zetu na ni lazima watoe matamko juu ya ukiukwaji mkubwa wa Demokrasia unaondelea sasa
  2. Wamkemee Kikwete waziwazi waache unafiki wao wa kutaka Uranium kwa kisingizio cha URAFIKI wao na kwa kumtumia JK
  3. Wananchi wa Tanzania sasa wameamka na hawataki tena ujinga uliokuwa unafanywa na ccm kwa miaka 50 bila kuleta maendeleo ya maana.
  4. Sasa watanzania wakiandamana kwa ajili ya katiba hakuna bunduki itakayoweza kuwazuia kufanya wanalotaka.

  Kama basi Kikiwete amechoka na amani ya nchi yetu, aendelee na ushenzi huu anaoufanya kutumia polisi.

  Tumechoka tuko tayari kufia rasilimali zetu!

  Nawasilisha
   
 2. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Jumuia ya kimataifa huwa inaona mafuta tu hayo mambo mengine hawajui!
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Tunatakiwa kuwasha moto kwanza waone na wasikie tunapigania nini.kinachotakiwa cku ya maandamano lazima kuandaa vyombo vya kimataifa vya habari mfano AL-JAZEERA, CNN, BBC, theCitizen9 ya kenya kamera zao zielekwezwe bongo na coverage lazima iwe kubwa ili ku-draw attention ya kina Obama.hapo utapapenda
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jumuiya ya kimataifa huwa haiwasikilizi wahuni km cdm ambao wasio fuata sheria !
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wao kwanza wanaona mnazinduka kudai katiba mpya. Kwa hiyo huenda kuna mkono wao nyuma ya hii katiba mbovu!!
   
 6. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Haoooo hata hawana aibu, eti wanapiga magoti kwa NATO waje wapige mabomu Dar Es Salaam na kuua zaidi ya watanzania laki 7. Isitoshe tutapata bill ya $480 bilioni.

  Hawa CHADEMA siwaelewi wanavyofikiria, ni chama kwenda nacho man to man mpaka kififie kama ua lililokosa maji.
   
 7. Bright Smart

  Bright Smart JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Jumuiya ya kimataifa waje kufanya nini bongo wakati nchi imeshafulia kila kitu(resources) wameshachukua kiulaiiiini wakati wa utawala wa awamu ya pili, tatu, na nne ndo wanamalizia vichache vilivyobakia sasa kwanini waje kujiingiza hasara ambayo haitawapa faida yoyote in the future, labda waje kwa ajili ya mlima kilimanjaro hata hivyo na wenyewe umeshalost ndo maana wakaupangusa katika NEW SEVEN WONDERS OF NATURE, yaani bongo nchi ya mbu tu...
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Jamani Jumuoa ya kimataifa huwa haingilii mambo yanayoonekana yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Hii ndiyo siri kubwa ya CCM na serikali yake, inachokifanya ni kutengeneza mazingaombwe kuwa taratibu zinafuatwa!!

  Ili kuonyesha otherwise, lazima waone jinsi tulivyochukizwa na mambo yao!! Hapa ndipo huwa ninawapa hishma waarabu!! Jamani Jukwaa la katiba liko wapi, tengeneza utaratibu watu tuingie kazini!!! Haki itakuja tu kwa lazima!!
   
 9. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wahuni ni wale wanaowaletea shida na ugumu wa maisha WANANCHI,na hao si wengine bali ni CCM,ila nyie ngojeni tu,bado kidogo tu mtaisoma,huko Mbeya,Arusha etc ni ishara kwamba WATANZANIA tumechoka na linakuja kubwa zaidi ya hayo..PUMBAVU NYIE!
   
Loading...