Jumong...

Ningewaona kina jumong wa maana kama wangefanya kama kina 2nd chance. Nani anataka kikorea? Ukizama kusoma pale chini unapitwa na matukio
 
Mimi pia ni mshabiki wa hizi series za Jumong. Korea wako juu sana katika film industry pia ingawa mara nyingi film zinazopata umaarufu ni za kutoka Hollywood na Hong Kong.
 
Kwa yeyote yule anayetaka kujifunza uongozi na majukumu yake, atazame tamthilia ya Jumong, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Laiti hawa watu wa Ubalozi wa Korea wangeleta nakala halisi za DVD za tamthilia hii, zikauzwa mjini, tungenunua na kuzitazama. Lakini wamechelewa, Wachina tayari wameshadurufu nakala haramu, zinauzwa mjini.

Sio kwamba tunapenda kununua nakala haramu, ambazo ni mwendelezo wa wizi, la hasha. Wenye kupewa madaraka ya kuitangaza tamthilia hii hawana UPEO wa kutafuta soko lake. ITV sio kila kitu, kwani kwanza wameishushia hadhi tamthilia hii.... kuipanga saa 5 usiku wakati watu wengi wameshalala, na marejeo yake wakati wa mchana wakati watu wengi hawapo nyumbani, ni sawa na kusema HATUTAKI WATU WATAZAME.

Mimi huwa nasubiri mpaka saa 5 usiku, kwa kuwa najifunza mengi. Lakini ntaenda kuitafuta dukani, nitanunua.

Alamsiki.

./Mwana wa Haki
 
Aisee,hii tamthilia ni masterpiece,ni kweli wengi hawaielewi vizuri lakini ni nzuri mno.Wakorea wanajitahidi sana katika tamthilia zao.Mi nilianza kwanza kuvutiwa na Winter sonata,jewel in the palace,af na merchant of josian na all in ambazo zilikua zinaoneshwa ktk chnl yao inaitwa Arirang.Ni nzuri sana.
 
My love wangu anaipenda mno,nilikuwa natafuta cha kufanya kila inapofika manake mtagombana ukichange station,nikanza kuifuatilia imenibidi nimtafute ALIBABA nimeanza Season 1 iko poa bana,by the way hivi ni kwanini wadada ndio wamekua wakwanza kuichangamkia???
 
 

Tupo wengi.

Omarilyas
 
Hii kitu Jumong iko tight sana, yani hata nirudi maji vipi
bora tu nikae atleast nimuone peaaa Chumong or chief general oi

hahahah hakuna bunduki humo, ni mapanga/majambia nshaa tu.

lakini Jumong is very interesting, korea wameprove wako juu sana ingawa
hawazungumzi kingereza.
 

hii ndo inaonyeshwa channel gani

ila nahisi kama huwa naotea tea hilo jina sehemu
 

ndugu yangu ni kweli tamthilia ni nzuri hata mimi huwa najitahidi nisizikose jewel na Jumong ubaya wa tamthili ni kuwa ukiianza kuiangalia ukaipenda unakuwa mtumwa wa kila siku lazima uangalie.
 
Nimempenda sana Ye Soya! Ameonesha uaminifu sana kwa Mumewe Chumong,kama mnakumbuka Chumong alimkatia kipande cha sword na kumuachia na yeye akabaki na kingine kama alama ya mtoto wake Yuri atapokuwa mkubwa.Uaminifu wa aina hii jamani inavutia sana yaani miaka kumi na tano Ye Soya bado anamkumbuka Mumewe siyo mchezo!
Nimempenda sana Ye Soya kwa kweli,ame act vizuri sana eneo lake na vilevile ana mvuto! Hahahaha!!
 

kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…