Wapenzi wa siries,
Katika kufuatilia kwangu siries hakuna na sijaona yenye stori nzuri kama jumong, si game of throne,
Breaking bad
Giant
24
Iris wala walking dead ambazo zimekuwa zinasifiwa sana hapa jukwaani, japo hii ya jumong ni ya kitambo lakini inastori ya kueleweka kuliko hizi zinazosifiwa hapa, washiriki kama
Hae musal
Geum wa
Jumong
Yeo ta bal
Lady yeum wa
Mo pal mo
Sosiono na marafiki zake na jumong ambao walikua kitaa na baadae kuwa watu muhimu baada ya jumong kuwa mfalme walinivutia sana.
Sijaona nzuri kama jumong kweli
Me nadhani unakosea kulinganisha vitu ambavyo viko tofauti
Yani ni sawa na mtu awe anaringanisha nyimbo ya hip hop na singeli ipi Kali? Au basketball team na football team
Ukute anafananishwa nani mkali Kati ya Diamond na Fid Q, Alikiba na joh makini, Barnaba na Nikki mbishi, watu itakuwa ngumu sana kukuelewa na inawezekana wakahisi hujui unachokitaka
Kwa uelewa wangu hiyo jumong ulipaswa ulinganishe na series ambazo zinafanana story/genre/culture/themes/settings
Hapo sasa utaringanisha hizo jumong/slave hunter/queen for seven days/Gu family book/love in the moonlight/six flying Dragons nk
Sasa mtu unakuja kulinganisha Jumong na Breaking Bad, hapo unakuwa unaringisha nini labda? Story tofauti, theme tofauti, genre tofauti, culture tofauti, settings tofauti
Unakuja kulinganisha Jumong na Prison Break hapo unaringanisha kipi mkuu au ubora wa picha? Kiufupi ni kwamba huwezi kuringanisha vitu ambavyo havifanani na huwezi kupata majibu sahihi
Kwa vitu ambavyo havina ufanano unaweza kulinganisha popularity/Fame/Income mfano mpira wa miguu na mpira wa mikono upi una wafuasi wengi? Jumong na GOT ipi ni series maarufu zaidi? ipi iliingiza pesa zaidi? Na sio eti ipi Kali zaidi
Kwahiyo mkuu Kwa uelewa wangu mdogo ulichofanya hapo juu hakikupaswa kuwepo