Jumla ya vikosi vya kiusalama tanzania....

Jumla ya vikosi vya kiusalama tanzania....

Status
Not open for further replies.
Sungu sungu pia wapo, sinza kuna jamaa mcongo alikodi chumba basi ndani ya wiki wazee wa uhamiaji wametia timu, bahati alikua na kibali cha kuishi
 
Kweli mkuu unahaki ya kufahamu majibu yako.Lakni mimi cjui.
 
Mbona mnatoka povu mara niishie kula bata mara itanisaidia nini...
Mbona tunaufahamu mkubwa kuhusu USA na wapo wazi why mnapenda mambo ya sirisiri tu afu utendaji F.....
Kujua ina maana kubwa sana kwangu maana nakatwa kodi kuwalipa hao...

Umenena vyema
 
Akili za maji taka hizi,,,hivi ni kweli umekosa cha kujadili unakuja kuleta mada eti watu wajadili usalama wa taufa?kweli watu hamna woga,,si mjadili rasimu ya warioba?
 
Mimi ni mzalendo kwa Taifa langu, kuna lawama nyingi kuhusu usalama wa Taifa ila naamini ndani ya usalama wa Taifa kuna department nyingi sana labda kama haitohathiri idara ya usalama na sheria za nchi mwenye uelewa wa ndani atupe ufahamu kama illivyo Marekani ninazijuwa taasisi zao karibu zote za kiusalama.

Nasikitika sana kwa maofisa usalama baadhi ninaowajuwa mpaka najiuliza hivi hii idara iko serious kwenye kuchukuwa watu wa kwenda depo? au wengine wanachukuliwa ili wawe makarani tu ndio maana huwa hawajari swala la IQ?

Naomba mchango wa Pasco Mzee Mwanakijiji na wale wote wenye kuyajuwa mambo kwa upana.
 
Last edited by a moderator:
Akili za maji taka hizi,,,hivi ni kweli umekosa cha kujadili unakuja kuleta mada eti watu wajadili usalama wa taufa?kweli watu hamna woga,,si mjadili rasimu ya warioba?

Kila mtu rasimu wakati destiny yake ushaijua mchakato umetekwa...

Kuna mambo mengi zaidi ya kujua na ukijua kitu ni rahisi idara inayohusika kama kitu kikitokea iwajibike ipasavyo sio sa hv kila kitu wanasingiziwa TISS wakati navyoelewa lazima kUwe na wigo mpana wa kiusalama nchini mwetu....

CIA anawajibika ki CIA
FBI kiFBI
Secret service vivyo hvyo
Marine nao kivyao....

Bongo je?????
 
Akili za maji taka hizi,,,hivi ni kweli umekosa cha kujadili unakuja kuleta mada eti watu wajadili usalama wa taufa?kweli watu hamna woga,,si mjadili rasimu ya warioba?
Hapa tunajadiri idara ya usalama wa Taifa na hatujadiri usalama wa taufa, hebu tupishe kajifunze kuandika kwanza mbulula wewe.
 
Mimi ni mzalendo kwa Taifa langu, kuna lawama nyingi kuhusu usalama wa Taifa ila naamini ndani ya usalama wa Taifa kuna department nyingi sana labda kama haitohathiri idara ya usalama na sheria za nchi mwenye uelewa wa ndani atupe ufahamu kama illivyo Marekani ninazijuwa taasisi zao karibu zote za kiusalama.

Nasikitika sana kwa maofisa usalama baadhi ninaowajuwa mpaka najiuliza hivi hii idara iko serious kwenye kuchukuwa watu wa kwenda depo? au wengine wanachukuliwa ili wawe makarani tu ndio maana huwa hawajari swala la IQ?

Naomba mchango wa Pasco Mzee Mwanakijiji na wale wote wenye kuyajuwa mambo kwa upana.

Asante mkuu kwa kuliweka dukuduku langu katika lugha iliyonyooka!!! Nadhani umedadavua vyema kuliko nilivyojieleza....

Usalama wana kazi kubwa sana na nawafahamu baadhi ingawa wao huwa hawajui nawajua na siwaambii najua...ila si kila kitu wao tu....
 
Nitatosheka sana akitokea wa kutueleza vitengo na kazi za maana hii idara imeingiliwa na kosa kubwa ni ajira kutotangazwa basi hadi mahouse girls wao wanawaingiza idarani ni ujinga mtupu.

ila nina uhakika usalama wa Taifa wanaomlinda Rais wao wako poa na hakuna shida kabisa na wanafanya kazi yao vyema, pia najuwa wako usalama wa Taifa wanaotoka Jwtz hawa nawaaminia sana wako poa kabisa, ila shida yangu hawa makarani wanaowekwa kwenye vicomputer walichukuliwa kwa vigezo gani? very hopeless, tena wale wa kike ndio janga unaweza kumtafuna na kumpiga picha za utupu, inasikitisha sana.
 
Hapa tunajadiri idara ya usalama wa Taifa na hatujadiri usalama wa taufa, hebu tupishe kajifunze kuandika kwanza mbulula wewe.

Huwezi kujadili kitu ambacho hukifahamu na wala hujawai kukiona kama kipo. acha uvuvuzela!
 
Hayo ndio maneno!
Lakini sio kusema mtu afatilie familia, kazi na bata!

sijamanisha kwamba huyu mtoa mada afwatilie familia na bata, Mfumo wetu wa maisha nd ulivyotengenezwa hivyo. hayo mengine tuwaachie wao ambao wana majukumu hayo.
 
Nitatosheka sana akitokea wa kutueleza vitengo na kazi za maana hii idara imeingiliwa na kosa kubwa ni ajira kutotangazwa basi hadi mahouse girls wao wanawaingiza idarani ni ujinga mtupu.

ila nina uhakika usalama wa Taifa wanaomlinda Rais wao wako poa na hakuna shida kabisa na wanafanya kazi yao vyema, pia najuwa wako usalama wa Taifa wanaotoka Jwtz hawa nawaaminia sana wako poa kabisa, ila shida yangu hawa makarani wanaowekwa kwenye vicomputer walichukuliwa kwa vigezo gani? very hopeless, tena wale wa kike ndio janga unaweza kumtafuna na kumpiga picha za utupu, inasikitisha sana.

Nakuonea huruma sana, seems umehamka na hangover ya jana tena ya pombe kali, Kijana idara ni zaidi ya uijuavyo na uisikiavyo. usijadili kitu ambacho unasikia kutoka kwa ma "informer". marekani wanakutisha na movie zao wanazo tengeneza ili tujue wapo vizuri kiasi gani. Ok fwatilia kazi iliyofanyika Commoro kabla ya jeshi kwenda nd utajua, kama Govt ikiamua ile kitu iandikiwe "script" iwe movie basi actors watoke huko marekani nd uta appreciate, WE ARE BETTER THAN THIS!. Huwa vitu haviwekwi wazi ata siku moja! piga gambe ukalale...TANZANIA KWANZA!
 
Badala ya kujibu hoja unajambajamba, mimi hapa kwa muda huu natumia simu ningekuwekea link, kazi za Usalama wa Taifa Marekani ziko online na zinaombwa kwa wote wenye sifa, ila ukiweza tu kuijaza fomu yao yote kiukamilifu ni kama umeshaipata hiyo kazi tayari
 
Mimi ni mzalendo kwa Taifa langu, kuna lawama nyingi kuhusu usalama wa Taifa ila naamini ndani ya usalama wa Taifa kuna department nyingi sana labda kama haitohathiri idara ya usalama na sheria za nchi mwenye uelewa wa ndani atupe ufahamu kama illivyo Marekani ninazijuwa taasisi zao karibu zote za kiusalama.

Nasikitika sana kwa maofisa usalama baadhi ninaowajuwa mpaka najiuliza hivi hii idara iko serious kwenye kuchukuwa watu wa kwenda depo? au wengine wanachukuliwa ili wawe makarani tu ndio maana huwa hawajari swala la IQ?

Naomba mchango wa Pasco Mzee Mwanakijiji na wale wote wenye kuyajuwa mambo kwa upana.

Hakuna ofisa unayemjua ww labda wale makanjanja wanao vizia wageni wawataperi na kuwasumbua wahindi wa k/koo bt hakuna unachojua kijana! mtu anachukuliwa kutegema na field anayotakiwa, inayomfiti hivyo usione makarani ukawadharau.....! tuna mambo mengi ya kujadili juu ya jamii yetu ya kitanzania hasa ujenzi wa jamii mpya.
 
Si ofisa wa kumjuwa tu bali ofisa ninayemla uroda. pole kwa kukaririshwa.
 
Badala ya kujibu hoja unajambajamba, mimi hapa kwa muda huu natumia simu ningekuwekea link, kazi za Usalama wa Taifa Marekani ziko online na zinaombwa kwa wote wenye sifa, ila ukiweza tu kuijaza fomu yao yote kiukamilifu ni kama umeshaipata hiyo kazi tayari

siyo kila unachosoma kwenye internet au kukiona lazima ukiamini... Elewa kila nchi ina taratibu zake katika kufanya mambo yake. Taratibu za familia yako na yangu ni tofauti hivyo tumia mifano hii hai utafahamu siku.!
 
Kabla hamjataka kujua idadi ya vikosi vya usalama, hebu someni makala hii iwape ufahamu wa TISS kisha tusonge mbele...

Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali. Wadadisi wa masuala ya kijasusi wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lilipo, Naelewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.
Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.

Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote kuanzialeadership,watendaji,teknolojia na sheria.

Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,

Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,

Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"

Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.

Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,

Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo nafikiri ihuishwe sheria hii imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii hawajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa ya kivyama.

Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kiakanda(regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi.TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni more sophisticated katika kufanya information sharing wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani,Uingereza,Pakistan,Is rael,Afrika Kusini,China,India na Canada

Ingawa miakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekua sensitive zaidi kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa(Power Interests) lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima tungeanza na kanda yetu ya Maziwa makuu,Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii nikwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa tajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI yakutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma.

Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na power struggle hapa east afica ambao ni Kenya.Hatujaweza vya kutosha kwenye Economic intelligence kule Kenya inagawa wao wamewekeza hapa kwetu.Leo hii Kenya ina-export TANZANITE,Wana-Export gold n.k.Balance of trade kati ya Tanzania na Kenya ni subject of Economic intelligence.tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiinteligesnsia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie possible scenarios na move za washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi hapa EAC au ukanda kupitia economic power house(Kenya) katika ukanda huu?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu yetu.Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekua zikinunuliwa kwa wingi na kuwa smuggled kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi wetu na ku-frustrate fisical na monetary policy zetu?
Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe modern zaidi
Malengo ya TISS kulingana na trend ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri(si utabiri wa majini/tunguri bali utabiri wa kisayansi),Kupenya,na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu,na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye Nyanja za kimataifa(jamii nyingine)

Malengo makuu yanatakiwa kujikita katika:

Mosi,Kuongeza nafasi na umuhimu wa idara ya mahakama na vyombo vya kutoa haki.Lengo hapa linatakiwa kuwa juu ya kuunganisha idara za mahakama,wizara ya mambo ya ndani na vitengo vyake kwa kuzingatia upeanaji wa taarifa huku haki za msingi za kiraia zikilindwa pamoja na uhuru wake tofauti na ilivyo sasa ambako TISS inatuhumiwa kutumika kuhujumu haki za kiraia kwa visingizio lukuki.Lengo kuu liwe kulinda haki na uhuru wa watu bila kuathiri maslahi ya jumla.Hili linahitaji ushirikiano kuanzia serikali kuu,mikoa,wilaya,majimbo ya uchaguzi,kata na hata ngazi ya mitaa pamoja na sekta binafsi

Pili,Utengenezwe utamaduni mpya wa kuahamasisha mawazo mbadala na matumizi ya weledi(professionalism/expertise):Kubadili utamaduni ndani ya TISS ni muhimu sana ili kuepuka mimosa ya kimkakati. It is necessary to create an intellectual culture that promotes discussion as well as dissenting opinion. It will require the use of collaborative technology, where subject expertise is maximized, increased cross-agency communication, and the exploration of alternative analysis

Tatu,Kurahisisha zaidi ukusanyaji wa taarifa za kintelijensia:TISS haina budi kuwa mbele katika matumizi ya teknolojia na pia ku-update wataalamu wake kitaaluma na katika matumizi ya zana za kisasa zaidi ili kurahisisha ukusanyaji huo kutoka Open-sources na kutoka Human-sources

Nne,Kuajiri watu kulingana na uwezo na taaluma zao na pia kuajiri watu ambao tayari wana ajira kwenye vitengo vingine lakini walipwe vizuri kwa ajili ya kazi ya usalama ili kupunguza gharama za kupachika watu wapya katika idara,mashirika na taasisi nyeti nchini.Pamoja na hili kitu cha muhimu watu hawa ni lazima wawe na sifa zinazofanana (common attributes) katika ujanja,uwezo wa hali ya juu na haraka katika utendaji huku maadili ya juu kabisa katika vigezo vya utendaji katika idara hii vikizingatiwa

Tano,TISS ibadili utamaduni wa kuhitaji-kujua kwenda Kuhitaji-kutoa taarifa(changing from the culture of need-to-Know to need-to-share):Ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kila ngazi ni lazima mtazamo wa idara hii ubadilike na suala la kutoa taarifa liwe ndiyo njia kuu ya kufanikisha malengo ya idara katika ngazi zote kwa hiyo kuna haja ya kuangalia jinsi taarifa zinavyofika kwa ubora unaotakiwa,kwa usahihi na kwa muda muafaka na hili ni muhimu na litasaidia zaidi kuwa karibu na watunga sera(policy makers)

Sita,Kuimarisha na kupanua zaidi uhusiano kati ya TISS na washirika wa ndani ya nchi na vitengo vingine vya kijasusi vya mataifa ya nje:Hii ni kwa kuwa tunaweza kuwa na common threats kwenye uchumi,kiitikadi,kiutamaduni,k iulinzi n.kHata hivyo taarifa za kijasusi kutoaka kwa washirika wetu ni lazima ziangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na pia tuwe na taarifa zetu ambazo tunaweza kulinganisha na taarifa za washrika wetu.Hizi kwa kijasusi zinaitwa ‘Corroboration codification’
Saba,kitengo kidogo kabisa cha mwisho ndichokinachotakiwa kuwa na acces ya taarifa nyeti lakini kitengo hicho kiwe scrutinized kwa hali na mali.Hata hivyo nitajadili kuhusu juu ya mfumo wetu mbovu wa counterintelligence

Nane,Kujenga mfumo ambao ni uniform zaidi katika utekelazi kisayansi na kiteknolojia,Ni lazima sasa idara iwe centralized katika kutoa maelekezo na iwe more decentaliced katika utekelezaji kwa mtindo ambao unaitwa ‘pyramid execution’.unified research itumike ili kuongeza ushirikiano na idara mbali mbali

Tisa,Mfumo wa kupongeza na kuzawadia utumike kuongeza performance

Kumi,mtindo wa kutumia miongo utumike lakini zaidi kwa haraka mtindo wa kutumia siku utumike badala ya miaka.Kwa mfano 720 days plan itumike badala ya miaka 2,180 days pla itumike badala ya 6 months plan kwa ajili ya monitoring na kuepuka urasimu na uvivu usio wa lazima

Pia ni vyema kutokana na power struggle ya ukanda tuunde vitengo vya ujasusi vya nje.kitengo hiki kifanane kwa muundo ingawa kutakua na marekebisho kidogo lakini kifanane na kitengo cha RAW cha india ambacho kiliundwa baada ya vita ya India na China.kabla ya hapo kulikua na kitengo cha IB ambacho kilikua na miaka 120 lakini hicho kilitumika kuchunguza watu zaidi na taasisi za kisaiasa.waingereza walikitumia kuwachunguza akina Mahatma Gandhi,Azad na Nehru zaidi.Kitengo cha RAW kinatumika kwa ajili ya military Intelligence na financial intelligence.Kuna haja ya kupima maofisa ubalozi wetu wanaopelekwa nje pamoja na Mwambata wa jeshi katika balozi zetu(defence attaché) kulingana na sera yetu.

Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa, kiuchumi na machafuko ya kiroho.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.
 
zacha, Matola na Mhandisi Mzalendo,

Sioni haja ya kulumbana, kimsingi naona kila mmoja ana hoja sema kinachokosekana ni namna tu ya kuziweka vizuri zikaeleweka.

Matola na Mhandisi Mzalendo

Kama nimewaelewa vizuri hawana tatizo na idara yetu ya usalama, ila wasichokipenda ni ule utaratibu wanaoutumia kuajiri na kiwango cha uwazi wa habari zao. Naomba niweke wazi hapo, uwazi tunaouongelea hapo sio mikakati yao wala habari za mipango yao ya ndani. Kwa mfano, idara na vitengo vyao. Sifa za muombaji kwa kila idara, vitu gani vinaweza kukufanya usipate kazi kwao, ukifanya kazi kwao unatakiwa uwe mtu wa aina gani. Hayo ni kwa uchache tu.Na ikiwezekana matangazo ya ajira kwa baadhi ya nafasi za kazi ambao kazi zao ni za kawaida. Huu usiri naweza kusema kwa aina moja ama nyingine umechangia sana kupunguza ushindani kwenye ajira na kusababisha watu wasio na sifa kupata nafasi huko bila kujali vigezo na sifa walizonazo.

Zacha anaongelea kwamba hatutakiwi kujua sana habari za usalama wa taifa. Ni kweli kuna haja ya usiri, lakini ni kwa kiasi gani? Ndio maana kwenye masuala ya information kuna classification. Nani aone habari gani na nani asizione. Mbona CIA au MI5 wametoa vitabu vya historia zao japo ni za mwanzoni lakini wameelezea jinsi idara zao kwa nini zilianzishwa, na chanamoto zilizopitia na maboresho yaliyofanyika.Wakasema hawawezi kutoa habari za karibuni zaidi kwa sababu za kiusalama.

Kuna haja na umuhimu wa wananchi kuelewa japo kwa uchache chombo chetu muhimu kama hichi kinavyoendeshwa, hii haimaanishi kila kitu kuwekwa hadharani. Need to know basis inahusika sana. Na vile vile itasaidia kuondoa hofu na sintofahamu inayogubika usiri wa uendeshaji wa hicho chombo kupelekea wajanja wachache kutumia fursa hiyo kujinufaisha kitapeli.
 
Last edited by a moderator:
Kila mtu rasimu wakati destiny yake ushaijua mchakato umetekwa...

Kuna mambo mengi zaidi ya kujua na ukijua kitu ni rahisi idara inayohusika kama kitu kikitokea iwajibike ipasavyo sio sa hv kila kitu wanasingiziwa TISS wakati navyoelewa lazima kUwe na wigo mpana wa kiusalama nchini mwetu....

CIA anawajibika ki CIA
FBI kiFBI
Secret service vivyo hvyo
Marine nao kivyao....

Bongo je?????
CIA wanahusika na intelegensia nje ya mipaka ya marekani
FBI hao wanausika na intelegensia ndani ya nchi,hapa wezi wa mitandao hawaruki kambi,wauwaji kama serial killers mafisadi wote wanachunguzwa na fbi na wana vitengo tofauti
SECRET SERVICE hawa wanalinda viongozi wakuu kama rais na waziri mkuu na familia zao.
MARINE hawa ni jeshi la maji
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom