sasa ni 21 au 20? ahhhgggggggg
ngoja na mimi nifannye hesabu:-
Kwamujibu wa Kikwete 2010 blog ni kuwa:-
Walio piga kura 8,626,283 – 42.84%
Kura zilizoharibika – 227,889 – 2.64%
Kura halali – 8,393,394 – 97.36%
Idadi ya kura na asilimia kwa kila chama ni kama ifuatavyo:
1. APPT Maendeleo - 96,933 – 1.12%
2. Chama Cha Mapinduzi – 5,276,827 – 61.17%
3. CHADEMA – 2,271,941 – 26.34%
4. CUF – 695,667 – 8.06%
5. NCCR Mageuzi – 26,388 – 0.31%
6. TLP – 17,482 – 0.20%
7. UPDP – 13,176 – 0.15%
sasa basi:-
96,933 + 5,276,827 + 2,271,941 + 695,667 + 26,388 + 17,482 + 13,176 = 8,398,414 kura halali za vyama.
Zilizo haribika ni 227,889, so TOTAL ya kura zote ni 227,889 + 8,398,414 = 8,626,303 JUMLA YA WATANZANIA WALIOPIGA KURA.
sasa basi ni kweli kuna TOFAUTI YA KURA 20. au ndio margin ya error? +20/-20, hawa jamaa hawaishi kuwashangaza watu unaweza kusikia hivyo.