Jumbe Tambaza: Alimsomea Nyerere dua nyota yake ikang'ara

Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,173
Points
2,000

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,173 2,000
Hapa cha uongo ilikuwa lazima uruke kiunzi ukikamatwa km kawaida yako.
Mtanganyika...
Ujuzi wangu uko katika nyanja hizo hapo chini.
Nilulize kitu kutokana na hayo nitakujibu ikiwa ninalo jibu:
 1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
 2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
 3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
 4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
 5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
 6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
 7. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
 8. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
 9. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
 10. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
 11. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
 12. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
 13. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
 14. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
 15. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
 16. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
 17. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
 18. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
 19. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
 20. Awards: Several Awards
 21. Visiting Scholar: (2011)
 22. University of Iowa, Iowa City, USA
 23. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
 24. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
 25. OTHER COUNTRIES VISITED
 26. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
6,840
Points
2,000

Titicomb

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
6,840 2,000
Hivi kuna dua zinafanya nyota ya mtu ing'are ? Hizi imani hizi
Mkuu wewe ni dini gani?
Kama mkristo au muislam nakujibu ndio zipo dua kama hizo.

Ushahidi kisa cha Yakobo (Yakubu) na kaka yake. Baba aliomba mawindo ya Esau mzaliwa wa kwanza ale kisha ambariki lakini Yakobo kwa msaada wa mama yao alimzunguka kaka yake na kumlaghai baba kisha akabarikiwa yeye.

Mfano mwingine ni baraka za sadaka za Abel na Kaini. Abel alibarikiwa sababu ya sadska bora ndipo nduguye kaini akapata wivu akamuuwa.
 

Duke Tachez

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2018
Messages
3,345
Points
2,000

Duke Tachez

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2018
3,345 2,000
ACHA NA MIMI NIFUTE WATU TONGOTONGO KIDOGO KISHA MWISHONI NITAZUNGUMZA KUHUSU HIZO DUA AZLIOFANYIWA HAYATI MWL J.K NYERERE

Maisha yamegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
1. Ulimwengu wa roho
apa namaanisha ulimwengu usionekana kwa macho ya kawaida, hapa ndipo tuaminipo ktk Mungu na Ibilisi.
2. Ulimwengu wa nyama
ulimwengu ni katika vitu vyote ambavyo tunaviona kwa macho yetu ya kawaida.
Nianze kusema kuwa, Taifa la Tanzania limefika hapa lilipo kutokana na makosa yaliyofanywa na waasisi wa hili Taifa na wale ambao wapo pia madarakani ila sana sana ni waasisi, kwanini? kwasababu muasisi wa taifa ama waasisi wa taifa ni LANGO la taifa.

Lango ni nini? Katika tafsiri ya kawaida lango ama mlango ni sehemu inayopitisha kitu ili kuingia ndani, kama tunaona katika ulimwengu wa nyama kuwa ipo mipaka ya nchi ambayo mtu, wanyama n.k huingia ndani ya nchi husika, vivyo hivyo ipo milango ama lango katika ulimwengu wa roho ambao unapitisha mambo ya rohoni ndani ya nchi.

NOTE:
Chochote ukionacho katika ulimwengu wa macho ya nyama, tambua kimeanzia rohoni. Hata katika uumbaji Mungu alianza kumuumba mwanamke na mwanaume ktk ulimwengu wa roho kisha ikaja kudhihirika ktk ulimwengu wa nyama.

Mnamo mwaka 1961, baada ya Waingereza kuiachia Tanganyika, waasisi wa hili Taifa wakiongozwa na Nyerere walitegemea saana ama niseme ni waamini wa ulimwengu wa roho ktk ufalme wa giza, hivyo walienda kwa wachawi wa nchi ama waganga ili kupata maarifa na akili ya kuiongoza nchi.
Moja ya vitu ambavyo vilitokea kwao ni kutopata tu maarifa na akili bali pia walitakiwa wakubali wachawi mazindiko ndani ya nchi, chama cha siasa TANU ambacho sasa hivi ni CCM kuzindikwa ama kuongozwa na serikali ama tawala za kuzimu Tanzania.
Nisizungumze mengi, nikatishe kwa kusema kuwa Mwl Nyerere kama kiongozi wa nchi ama muasisi wa Taifa hili, ndie alikuwa lango la kupitisha falme za giza ndani ya nchi ya Tanzania ambapo hata yeye mwenyewe hakujua kama haya anapitisha haya mambo ambayo yaliicost Tanzania kipindi kile na hata sasa. Hayati Baba wa Taifa angejua kama kupitia yeye anapitisha haya mambo wala asingekubali na kama angekuwa na nguvu ya kujinasua angefanya hivyo ila kwa bahati mbaya hakuwa nayo.

TURUDI KWEYE MADA
Dua alizosomewa Hayati JK Nyerere ndizo tunazoita ushirikina sana sana katika kusafisha Nyota, kwanini?
Mungu anapomuumba mwanadamu huwa anamuumba kwa jinsi yake nikimaanisha vinasaba, mtazamo, akili, nyota, hekima, maarifa n.k ila viongozi wengi wa nchi huwa wanapewa akili ya ziada na kupandikiziwa nyota ambazo sio za kwao. Wachawi/Waganga wana uwezo wa kutambua nyota ya mtu tangu akiwa mtoto na wana uwezo wa kutoa nyota yako na kumhamishia mtu mwingine, sio nyota tu bali hata nafsi na mengineyo.
Hayati Baba wa Taifa ni moja ya viongozi waliveshwa nyota ambazo hazikuwa ni za kwao, hizo nyota wachawi/waganga wanazimiliki sana huko kuzimu.

Embu jaribu kutafakari, endapo kweli Mwalimu Nyerere alikuwa na vinasaba vya uongozi, je katika watoto wote aliokuwa nao hakuna hata mmoja ambae ana vinasaba vya baba yake? HAKUNA, endapo uongozi wake ile hekima na maarifa na nyota yake alipewa na Mungu katika uongozi basi kati ya watoto wake wote alokuwa nao yupo mmoja walau angekuwa na characters kutoka kwa baba yake.

Watanzania tusiwasifu sana hawa wasomaji dua hususani wanaojiita wazee wa Dar es Salaam, ni washirikina wakubwa mno, maisha tunayoishi leo Watanzania ni matokeo ya maagano ya kuzimu na watawala wetu ndio maana leo hii akili za watanzania zimefungwa kutokana na yale mazindiko. Mtawala anaweza akafanya chochote na watanzania wasichukue hatua, UFISADI, WANYAMAPORI, DEMOKRASIA N.K watanzania tunalalamika kwa muda ila watawala kupitia wachawi wa nchi wanazima akili za watanzania na hawahoji tena wala hawakumbuki.
kwa leo nitaishia hapa ila ipo siku nitaandika kwa mapana mnooooooo kuhusu haya mambo, kwa wale msionielewa mnisamehe, sina kipawa cha kufindisha na haya nimeyaandika ghafla ila ipo siku nitayaandika kwa mpangilio mzuri kabisa.
Mkuu yaandike
 

elly stambuli

New Member
Joined
Jul 13, 2009
Messages
4
Points
20

elly stambuli

New Member
Joined Jul 13, 2009
4 20
Kimbe...
Itabidi ustahamili kwani ikiwa unaishi sehemu ambapo wapo Waislam
ni lazima mambo kama haya utakutananayo lakini ni ya muda mfupi.

Sidhani kama inakuudhi kusikia adhana kila siku mara tano.
H
Shajara ya Mwana Mzizima
Jumbe Muhammad Tambaza

Alimsomea Dua Nyerere, Nyota Yake Ikang’ara
Na Alhaji Abdallah TambazaJumbe Muhammad Tambaza

JUMBE Muhammad Tambaza, ni mmoja katika wapigania uhuru mashuhuri wa nchi hii ambao, historia inawataja kama ni watu waliotoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kumng’oa Mkoloni Mwingereza, katika ardhi yetu tukufu.

Hayati Mzee Tambaza, ambaye alifariki mnamo mwaka 1978 hivi, anaingizwa katika kundi moja la watu wa mwanzo kabisa waliompokea kwa furaha na upendo kijana Julius Nyerere kutoka Butiama, alipofika jijini Dar es Salaam kwa kumuunga mkono ‘mia kwa mia’, katika harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika kwenye miaka ya 1950s.

Wanaharakati wengine aliokuwa nao ni pamoja na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi wa Mwananyamala; Mzee John Rupia wa Mission Quarters; Sheikh Suleiman Takadir; Sheikh Haidar Mwinyimvua (Kisutu); Mzee Max Mbwana (Kariakoo); Zubeir Mwinshehe Mtemvu (Gerezani) pamoja na familia ya Mzee Azizi Ali (Mtoni) na ile ya Kleist Sykes (Gerezani), Dar es Salaam.

Ukoo wa Diwan Tambaza Zarara bin Mwinyi-Kitembe, ndio waliokuwa wenyeji wa maeneo ya katikati ya jiji wakati huo, wakihodhi eneo la ardhi yote ya Upanga, iliyosambaa kuanzia Daraja la Selender kuelekea Palm Beach Hotel, hadi Ikulu ya Magogoni kwa upande mmoja; na kwa upande mwengine maeneo yote kutoka Aga Khan Hospital, Ocean Road Hospital, Kivukoni Front (makaburi ya asili ya wanandugu wengine yako pale Wizara ya Utumishi, Magogoni) kwenda Mnara wa Saa pale Uhuru Street na vilivyomo ndani yake.

Habari zinasema kwamba, katika siku za mwanzo tu za kupambana na Mwingereza, wazee mashuhuri wa hapa Dar es Salaam walikutana na kuamua kumfanyia ‘zindiko’ na ‘tambiko’ la kijadi, pamoja na kumwombea dua maalumu kijana mdogo, Julius Nyerere, ili kumkinga na waovu na pia kuifanya nyota yake ing’are juu ya wote wenye nia mbaya naye; wakiwamo watawala wa Kiingereza, hasa Gavana Twinning.

Katika moja ya hotuba zake za kuaga aliyoitoa mnamo Novemba 5, 1985, Nyerere alilikumbumbuka tukio hilo na hapa chini anasimulia:

“…Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania…na mambo makubwa kama haya kama hayana baraka za wazee hayaendi… huwa magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani; tangu awali kabisa.

“Sasa siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (nyumbani kwake) akasema: ‘Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.”

Anahadithia Mwalimu na kuendelea:

“Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika… zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee… za jadi, “…walikuwa na beberu la mbuzi… wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama beberu akachinjwa huku anaambiwa Twinning ‘umekwisha’… nikaambiwa tambuka… nikavuka lile shimo na baada ya hapo nikaambiwa …basi nenda zako kuanzia leo Twinning amekwisha!”

Mwalimu alimaliza kusimulia namna alivyofanyiwa dua na tambiko nyumbani kwa Mzee Tambaza, Upanga jijini.


(Picha ya Baraza la Wazee wa TANU kutoka kitabu cha Saadan Abdu Kandoro, ''Wito wa Uhuru'')

Kutawaliwa na Wazungu kuliwakera na kuwakasirisha watu wengi sana, kutokana na kule kudharauliwa ndani ya nchi yao wenyewe na watu wengine; hasa pale walipominywa katika kupatiwa huduma muhimu kama elimu bora, matibabu na mahala pazuri pa kuishi.

Pamoja na mambo mengi mengine yaliyokuwa mabaya kutokana na kutawaliwa, yamo pia na yale ya kuwekwa kwa madaraja katika utoaji huduma muhimu. Sisi, wana wa nchi hii, hatukuwa na shule za maana hata kidogo; watu wote sisi tukasomee shule moja tu (Mchikichini) mpaka darasa la nne; kwa nini hasa kama siyo dharau?

Nyumba zetu za kukaa zilikuwa za ovyo zilijengwa kwa miti na kukandikwa udongo na juu ni makuti, tena hapa hapa mjini Dar es Salaam, sikwambii vijijini; umeme uko kwenye taa za barabarani na siyo majumbani mwetu. Tukiwasha vibatari na taa za ‘chemli za Aladin’ kwa wenye uwezo kidogo kila siku.

Hospitali ziliishia kutoa kama huduma fulani ya mwanzo tu (First Aid). Haikuwapo hospitali ya Amana, Temeke, Mnazi Mmoja, Mwananyamala wala Mbagala. Tuliponea kibahatibahati tu kwa mizizi na majani ya porini. Ukiwa na homa kali basi chemsha mwarobaini; tumbo la kuendesha chemsha majani ya mpera au mpapai nani akupe ‘antibiotic wewe’.

Hospitali ya Muhimbili, yenye maabara na vipimo pamoja na madaktari bingwa, ilijengwa mwaka 1957 - ni juzi tu - kwa heshima ya Binti Mfalme Margareth II, aliyekuwa na ziara ya kutembelea makoloni ili aje kufungua rasmi hospitali hiyo. Kiwanja kilitolewa kwa hisani ya familia ya Mzee Jumbe Tambaza, ambapo miembe ile mikubwa inayoonekana mpaka leo pale ilikuwa shambani kwa kina Tambaza.

Kwa hivyo basi, ukiacha labda homa na vidonda, magonjwa mengine yote kwetu ilikuwa ni kifo tu. Umri mkubwa wa kuishi kwa wastani ulikuwa ni miaka 30.

Mzee Jumbe Tambaza, ambaye jina lake linanasibishwa na shule maarufu ya Sekondari ya Tambaza ya jijini - hana uhusiano wowote na shule hiyo - shule ilipewa jina lake kutokana na eneo iliyopo na kwa kuthamini mchango wake katika kupigania uhuru.

Kabla ya hapo, wakati huo wa ubaguzi wa rangi na matabaka, shule hiyo na ile ya msingi iliyo jirani nayo inayoitwa Muhimbili Primary, zilikuwa mahsusi kwa vijana wa Kihindi tu – hasa Ismailia - zikijulikana kama ‘Aga Khan Schools’ na kamwe hawakuwa wakisoma Waswahili na Kiswahili pale.

Shamba la Mzee Jumbe Tambaza pale Upanga, lilianzia mbele kidogo ilipo Shule ya Jangwani Wasichana (ambayo wakati wa ukoloni ilijengwa na serikali wasome watoto wa kike wa Kihindi tu, na ile Shule ya Azania ilikuwa kwa watoto wa Kihindi wa kiume), na kutambaa moja kwa moja mpaka lilipo Daraja la Selender pale baharini.

Eneo la Majengo ya Hospitali ya Muhimbili ilikuwa mali ya Jumbe Tambaza na marehemu nduguze (Msakara, Kudura na Mwamtoro Tambaza). Kutokana na kukosekana kwa hospitali ya maana ya rufaa kwa ajili ya Waafrika (kwa sababu ya ubaguzi tu), hayati Mzee Tambaza alitoa eneo lote lile la Muhimbili ijengwe hospitali ya Waafrika ili kupunguza vifo vilivyotokana na kukosa tiba sahihi.

Kijihospitali kidogo kwa ajili ya watu Weusi kilikuwapo pale jirani na Kituo cha Kati cha Polisi (Central Police Station) jijini, ikiitwa Sewa Haji Hospital, kwa heshima ya mfadhili aliyeijenga kusaidia jamii masikini. Sewa Haji alikuwa mkazi wa Bagamoyo mwenye asili ya Kibulushi kutoka Persia. Baada ya kujengwa hospitali ya Muhimbili, jengo moja katika yale matatu makuu, likaitwa Sewa Haji kama kumbukumbu yake.

Mjini Dar es Salaam wakati huo wa kibaguzibaguzi, serikali ya kikoloni haikutenga sehemu ya kuzikia watu weusi ambao walikuwa daraja la nne. Yale makaburi mashuhuri ya Kisutu, wakati huo yalikuwa ni ya watu wenye asili ya Kiarabu tu! Mwengine yoyote, ilibidi apelekwe kijijini kwao tu nje ya mji – Kunduchi, Mbweni, Msasani, Bagamoyo, Kisarawe, Maneromango na mikoani pia.

Sasa, ili kuondoa adha hiyo na usumbufu, Babu Mzee Tambaza, alitoa bure sehemu kubwa ya eneo lake itumike kwa watu wenye kuwa na shida ya kuzika ndugu zao jijini. Makaburi ya Tambaza siku hizo yalikuwa maarufu sana kuliko yalivyo yale ya Kisutu kwa sasa. Kamwe watu weusi hawakuwa wakizikwa Kisutu, kama ilivyo wakati huu.

Kufuatia hali hiyo, Jumbe Tambaza aliwashawishi binamu zake wawili, Mwinyimkuu Mshindo na Diwan Mwinyi Ndugumbi na wao wakatoa sehemu watu waweze kuzikana kule maeneo ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa na Ndugumbi, Magomeni Makuti; makaburi ambayo mpaka leo yameendelea kutumika kuzikia watu wote.

Neno, ''Tambaza,'' limetokana na neno ''kutambaa,'' au ''kusambaa,'' eneo kubwa. Diwan Tambaza na nduguze walikuwa watawala wa sehemu mbalimbali za hapa Mzizima siku za nyuma kabla Waarabu, Wajerumani wa Wangereza kufika hapa. Nduguze wengine ni Diwan Uweje; Diwan Uzasana; Diwan Mwenye-Kuuchimba na Diwan Mwinyi Ndugumbi.

Majina hayo walijipachika wenyewe kiushindani, kujigamba na kujitukuza kuliko ndugu wengine; hivyo kimafumbo mafumbo, huyu akajiita hivi na yule akamjibu mwenzake vile; mwengine akajiita naye atakavyo, kutokana na uhodari na tawala thabiti walizoziongoza.

Majina hayo pandikizi, hata hivyo yalikuwa na maana yake kila moja; kama vile mtu aseme mimi ‘Mobutu Sese Seku Kuku Mbenju wa Zabanga’, ikiwa na maana ya ushujaa kwa ‘Batu ba Kongo na fasi ya Zairwaa!’

Sasa Diwan Tambaza alipojiita vile, nduguye Diwan Uweje akamjibu na kumwuliza hata ukiwa umesambaa ndio uweje? Mwengine naye akasema, ‘’Ah! Uliza sana wewe uambiwe.’’ Hivyo yeye akajita Diwan Uzasana. Diwan Mwenye-Kuuchimba, yeye alikuwa akitawala maeneo ya Mtoni Kijichi na Mbagala yake, akasema, ‘’Nyie wote mnacheza tu, ‘mimi ndiye mwenye kuuchimba!’’ Kwa maana ya kwamba ndio kiboko ya wote. Ilimradi hali ikawa ndiyo hiyo; na hizo ndio zama zao, kwani husemwa kila zama na kitabu chake.

Mwandishi wa makala haya, jina langu naitwa Abdallah Mohammed Saleh Tambaza. Babu yangu Mzee Saleh bin Abdallah Tambaza wa Zarara, anakuwa binamu wa Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, yaani baba zao walikuwa ndugu.

Shamba la babu yangu mimi pamoja na kaka yake Kidato Tambaza, linasambaa kuanzia Don Bosco, Makao Makuu ya Jeshi, Diamond Jubilee, Msikiti Maamur (kaburi la babu na babake babu yamo ndani ya Msikiti wa Maamur unapoingia mkono wa kulia pale ukutani), kuelekea kwenye Jamat la Wahindi mpaka Mahakamani kule Kisutu.

Miembe, minazi na mizambarau ile ya asili inayoonekana Upanga, ilipandwa na babu yangu kwa ajili ya urithi wa wajukuu zake, itakapofika zamu yao kumiliki maeneo yale.

Kwa bahati mbaya sana, Wazungu Waingereza, wakaona mandhari ile nzuri ya Upanga, hawakustahili watu weusi kuishi pale na wakawaamuru babu zangu wahame wawapishe Wahindi raia daraja pili. Hii ni baada ya wao Wazungu daraja la kwanza kuchukua eneo lote la Oysterbay (sasa Masaki). Maeneo yote hayo mawili yenye upepo mwanana ni karibu kabisa na bahari.

Kitendo cha kumhamisha mtu nyumbani kwake kwa namna ile, halafu kumpa fidia uitakayo wewe, ni dharau, dhuluma na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Wazee wale wastaarabu na wajanja hawakuwa na haja ya kuyauza maeneo yale, kwani ukiyaangalia utaona waliyapangilia ili vizazi na vizazi vya kwao viishi hapo.

Hii haihitaji mjadala wala maelezo marefu, lakini ni ushahidi tosha kwamba inaweza ikawa ndiyo sababu kubwa iliyomfanya Mzee Jumbe Tambaza awe mstari wa mbele kabisa katika kuwachukia watawala wa Kizungu na kumuunga mkono Nyerere kwa nguvu kubwa kama ile.

Mchango wa Mzee Jumbe Tambaza katika ukombozi wa nchi yetu haukutetereka hata kidogo, kwani hata pale rafiki yake mpenzi Sheikh Suleiman Takadir, alipotahadharisha watu kuwa makini na Nyerere maana ameonyesha kwamba siku za usoni angependelea zaidi jamaa zake, Mzee Jumbe hakumuunga mkono na akakubali Sheikh Takadiri atengwe na jamii kwa manufaa ya umoja wa kitaifa.

Jumbe Tambaza pia hakumuunga mkono Zubeir Mtemvu, kwenye suala la Kura Tatu ambalo ilibaki kidogo tu chama cha Tanu kingesambaratika na kuwa vipande viwili; lakini yeye alibaki na Nyerere wake mpaka dakika ya mwisho kule Tabora hadi kukasainiwa waraka wa ‘Uamuzi wa Busara’ ambao uliwapeleka TANU kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu.

Katika picha ya pamoja iliyopigwa baada ya kutangazwa ushindi wa kuingia kwenye Kura Tatu kwa chama cha TANU, anayeonekana nyuma ya Mwalimu Nyerere pale Tabora ni Mzee Jumbe Tambaza. (Rejea kitabu Mohammed Said, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes… uk 275).

Kutokana na uaminifu wao usiotetereka kwa chama chao, Mzee Jumbe Tambaza na mwenziwe Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; wazee wale wawili wa Kimashomvi kutoka Mzizima, kwa muda mrefu wamekuwa wajumbe wa kudumu (permanent seats) kwenye Kamati Kuu ya TANU bila kupigiwa kura; achilia mbali ule uwepo wao kwenye Baraza la Wazee wa TANU.

Mnamo mwanzo wa miaka ya mwanzoni 1950, Mzee Tambaza alitumbukizwa tena kwenye mgogoro mkubwa na serikali pale ilipokuwa inajenga upya Barabara ya Umoja wa Mataifa kutokea Faya kuelekea Daraja la Selander, ilipoamuliwa kwamba sehemu ya eneo la makaburi iondoke kupisha ujenzi huo.

Hayati Mzee Tambaza, alifungua kesi mahakamani dhidi ya serikali, kesi ambayo inatajwa kama moja ya kesi nzito (landmark cases) sana kutokea hapa nchini na Afrika Mashariki iliyogusa imani ya Dini ya Kiislamu; kwamba je, ni halali au si halali kufukua makaburi ya watu waliokufa?

Kesi ya Makaburi, kama ilivyokuja kujulikana, iliunguruma kwa muda mrefu na kujaza kurasa za mbele za magazeti wakati huo, kutokana na mabishano makali ya hoja (cross examinations) mahakamani baina ya mawakili wa pande mbili hasimu.

Wakati serikali ikiwatumia masheikh wazawa wa hapa waliosema kwamba inakubalika kufukua makaburi, Jumbe Tambaza aliwatumia masheikh wakubwa kutoka Mombasa na Zanzibar, akiwemo aliyekuwa Kadhi wa Zanzibar Abdallah Saleh Farsy kupinga hoja hizo.

Kwa kishindo kikubwa, Mzee Tambaza alishinda kesi ile na ikabidi barabara ile ipindishwe pale kwenye mteremko wa kutokea Faya na kuyaacha makaburi na vilivyo ndani yake kama yalivyo. Haraka haraka, Hayati Mzee Tambaza akafanya maamuzi ya kujenga msikiti ambao haukuwapo mahala hapo kabla ya tukio hili, kuepusha kujirudia.

Huyo ndiye Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, mwanaharakati wa kupigania uhuru wa taifa hili wa kupigiwa mfano, aliyetetea na kutoa vyake kusaidia wanyonge wenziwe katika jamii yetu katika kipindi cha manyanyaso ya utawala dhalimu wa Malkia wa Uingereza. Alimfanyia madua na matambiko ya jadi Mwalimu Nyerere ili nuru yake ing’are kama mwezi na jua!

Ewe Mola Mghufirie madhambi yake – Ameen.
HISTORIA HII NI NZURI SANA. IMESAHAULIKA KABISA
 

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,502
Points
2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,502 2,000
Miaka fulani ya nyuma kulikuwa na mashindano ya kila mwaka ya mpira pale Don Bosco. Timu mbalimbali za mitaani na hata za sekondari zilikuwa zinashiriki mfano Kibasila, Azania, nk.

Maeneo ya Muhimbili walikuwa na timu yao. Wale jamaa nahisi walikuwa wanalala kwenye yale makaburi kabla ya game zao. Wachezaji wengi walikuwa wanaishi palepale karibu na yale makaburi, naamini baadhi wana uhusiano na huyu Babu. Walikuwa wakija kuna harufu fulani ilikuwa inatawala uwanja mzima.

Najua kuna watu wamo humu wanajua ninachokisema.
 

Forum statistics

Threads 1,379,785
Members 525,565
Posts 33,756,551
Top