VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,006
Mzee Tupa tupa jongea hapo Jangwani ukapate maji ya uzima
Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...
Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...
Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...
Je,niende wapi? Njia panda!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Ukoo wa panya na chama chakavu!Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...
Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...
Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...
Je,niende wapi? Njia panda!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kwni EL hataudhuria sherehe za miaka 37 ya chama chake?