Jumapili hii: imani inapokuwa mzigo

Jumapili hii: imani inapokuwa mzigo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,456
Reaction score
872,092
usicheze na imani za watu, usicheze na vitu vinavyogusa hisia za watu, imani za dini mbalimbali zimeteketeza maelfu kwa maelfu ya watu wasio na hatia, kibwetere wa uganda na applewhite wa heaven gate church ni mifano michache. hapa kwetu tunailea hii kansa, kuna mengi hayapo sawa tunayachunia, kuna imani zingine kazi yao ni kuponda na kukashifu imani za wengine, lakini kuna hawa watu wanaopenda sana kuwepo kwenye mikusanyiko ya watu wakiwa na spika wakihubiri habari za imani zao wanatoka jasho wanapiga kelele ni zogo tupu, kuna nabii tito yeye anatembea na chupa ya bia na vipeperushi akihimiza watu watende zambi, kuna wale wanaowatuma watoto wapite kwenye mabar na sehemu za starehe kuwaomba wateja michango ya kujenga nyumba za ibada! list ni ndefu kuna mitume na manabii vitu wanavyohubiri ni mzigo mkubwa kiimani.
 
Mi thijamuelewa bado. Nilithani kuna jambo limetokaea kanithani kwake. Ajipange vidhuli.
 
Mkuu,

As long hawajakashifu dini za wengine na hawakulipua kwa mabomu, basi FANYA YAKO!
 
Unaongelea ni ni hasa?

Tewe kwa faida yako na wengine ni hivi 1.huwezi kuwahubiria watu kuwa wataenda peponi kwa kujitoa uhai, soma habari za kibwetere na wengineo 2. huwezi hubiri kuwa pombe ni haramu halafu wakati huo huo utume watoto wapite kwenye mabar wakaombe michango ya kujenga nyumba ya ibada. 3. huwezi hubiria watu waoe wake wengi na kuzaa na mahouse girl ati ni amri ya mungu, athari zake unazifahamu? ndoa kuvunjika na watoto wa mitaani kuongezeka. soma tena kwa makini kisha tafakari kwa makini
 
Mkuu,

As long hawajakashifu dini za wengine na hawakulipua kwa mabomu, basi FANYA YAKO!

hujui naongelea nini, imani mizigo zimeleta majanga makubwa duniani uharibifu wa mali na vifo vya watu wengi kwa pamoja, tumepoteza wasomi mahiri na nguvu kazi kubwa kwa imani hizi, kigogo round about kama unaelekea jangwani mbele kidogo kulia kuna kanisa pale ukipita kila siku kuna watu wako pale wanaimba, kazi watafanya saa ngapi? familia watazihudumia saa ngapi? mchango wao kwa nchi kiutendaji ni upi? tafakari
 
.
IMG-20190226-WA0000.jpeg


Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom